Ndugu RNA, naomba kukupa taarifa:-
1. Hayo 'makundi' yako kwenye DNA ya CCM. Kwenye awamu ya pili yaliongezeka na kujitanua.
2. Wakifika serikalini (kundi au watu wao "wakishinda") huwa "genge au mtandao". Hayo yameiumiza na kuifasadi sana nchi yetu kwa miaka zaidi 30 sasa.
Kwenye damu ya hayo makundi/mitandao hakuna chembe ya uadilifu wala uzalendo - ni ubinafsi tu.
Fuatilia historia hasa kuanzia miaka ya tisini (1990s).
3. Makundi/Magenge hayo yote kifupi HAYANAGA ITIKADI. Never!
Dhana yao ni masalahi yao tu!
Kinachowaunganisha au kuwagombanisha ni maslahi yao sio Itikadi. Ndio maana bado wote wako CCM, na wanatoana roho humo humo.
Kawaida huwa yanaongozwa na kauli "..sasa ni zamu yetu kula....zamu...zamu"
Lakina kwa nje yatazungumza lugha na ahadi tamu za kisiasa.
4. Leo ukihalalisha kundi ambalo liko bench, au ambalo 'sio zamu yao'; una maanisha "vita kamili ndani ya CCM". Hiyo vita itatishia uhai wa CCM kama chama na huenda ukaifuta CCM toka kwenye ulingo wa siasa jumla.
5. Kweli, hayati Magufuli naye alikuwa na makundi yake; na alipitishwa kugombea mwaka 2015 kwa njia na utamaduni huo huo.
'Alichokosea' (akidhani angetawala maisha) ni kutumia nguvu za dola ku deal na magenge hasimu na lake. Hapo alivunja "miiko na mipaka" inayotawala huo mchezo wao mchafu', zamu zamu.
Ndio maana ilibidi 'anunue' watu toka "nje" mfano akina Bashiru na Polepole.
Na akapanua wigo wa kundi (voters base) kwa kutumia ukanda.
Hivyo utaona bayana kuondoa/kuua hayo makundi ni kuiua CCM - na hiyo sio hasara kwani faida zitakuwa nyingi kwa muktadha wa Taifa letu.
Ubaya wa hoja yako, RNA, uko hivi - ukihalalisha leo kuwapa Sukuma Gang na wengine vyeo; kesho yatazuka magenge zaida, tena yenye silaha na wapiganaji kabisa (mfano Somalia, Sudan, Philippines nk) nao watataka wapewe 'mgao wao'.
Tayari tunaibiwa na kupata hasara kama nchi lakini wewe unashauri tuhalalishe uharamia na uhujumu uchumi. HAPANA!
Ndio maana tunataka Katiba Mpya ili kuondoa haya madudu. Uko uchafu na ubovu mwingi sana nchini lakini Katiba Mpya itatupa nafasi na nguvu ya kuyashughulikia.
Apparently; walioko madarakani wanajua na kuelewa haya ninayoyasema kuliko watawaliwa!