Sukuma liwe kabila tambulishi la mtanzania

Sukuma liwe kabila tambulishi la mtanzania

Jamani kwema?

Mambo yasiwe mengi ngoja niende kwenye Jambo lenyewe,Katika hekaheka nazopewa na mwalimu ulimwengu wiki hii nimejikuta nipo usukumani ndani kabisa,nimekutana na kina Ngosha original achana na Hawa kina Ngosha wa mjini kina Shimba ya Buyenze ,kiukweli nimefurahi Sana kufika huku nikaona hivi kwa Nini watanzania wote tukiwa nje ya nchi si tujiite tu WASUKUMA?
Nimejifunza vichache kwa siku mbili nilizokuwapo hapa

1.WAKARIMU SANA
Hawa watu wanahitaji kuolewa hongera,imagine nimefikia nyumba ya wageni,kufika saa moja usiku nijiandaa nitoke nikatafute chakula Nasikia nagongewa mlango,kufungua namkuta dada aliyetupokea na sahani mkononi ananikabidhi, nikamwambia hapana utakuwa umekosea sijaagiza chakula akaniambia hapana nimepika nimekuletea mgeni wali na "sansa"nikajiuliza hiyo sansa itakuwa nyama ya porini ngoja nipokee,kufungua nikakuta mboga ya majani imeungwq karanga kuonja hakika ilikuwa tamu Sana,Asubuhi nataka kutoka kaniambia dada Subiri unywe uji na matobolwa,nikajua hayo matobolwq yatakuwa sijui ni maandazi,nikasema ngoja Nile tu,nikazugazuga nikasema sawa basi nikapewa uji na viazi vitamu Ila vimeandaliwa tofauti vilikuwa vitamuu kumbe ndio mabolwa,,basi nikala nikasema huyu hajui watoto wachalamila kwa Ganda la ndizi...Ila kesho nikiondoka nitampa wekundu mmoja nimependa ukarimu wake

2.WANASHANGAA SANA
Jamani Hawa watu wanashangaa kuliko kawaida,Yaani wanashangaa Hadi na Mimi nikaanza kujishangaa

3.WANAPENDA LUGHA YAO
Yaani watu wanapenda lugha yao hatari,eti wananisalimia kingosha🙄🙄🙄 mimi najua Sasa nabaki natoka macho tu

4.WANAPENDA BAISKELI
Jamani na miongo yangu kadhaa hapa duniani nilikuwa sijui baiskeli Zina matajiri ya kila rangi,jamani kina baiskeli huku Zina matajiri mekundu,ya Njano,ya kijani,ya purple ya blue,hizo baiskeli zimepambwa na maua,usiku zinawakawaka Kama Xmas tree na zimefungwa redio... baiskeli huendeshwa na watu wa rika na jinsia zote

5.REDIO ZA MKONONI
Jamani Kila mtu kabeba kiredio mkononi kinaimba kisukuma,sijajua hao wasanii wa hizo nyimbo zao wako wapi..huku sijasikia Amelowa Wala Salome yaani unaeza dhania hauko Tanzania

6.WADADA
Ama kiukweli wadada zao wanaushirikiano Sana,timu niliyoongozana nayo kikazi na furaha sana maana wameambiwa wajisikie nyumbani 🤦🤦🤦yaani huku ningekuja na swahiba wangu bwana mzabzab angelowea huku

7.WAKAKA
Sijui ni wapenzi Sana wampira au lah,Kila kijana kavaa jersey,Kuna jezi za kika Ligue huku kuanzia la Liga,bundesliga,CAF Hadi za wale waliovunja uwanja juzi,yaani kwenye Vijana 20 wasiovaa watakuwa watatu
8.MAJI
Jamani bunge la bujeti mwaka hii lielekeze fedha za kutosha kwenye wizara ya maji ndugu zetu wapate maji safi na Salam,kweli huku Kuna maji hayana tofauti na chai ya maziwa.
9.UTANI
Jamani Hawa watu wanataniana jamani ukisikia na Ile lafudhi yao utacheka mpaka machozi

Jamani Wana mambo mengimengi Sana,nashauri raisi ajae awe tu NGOSHA maana ni taifa kubwa
Maswalj atajibu huyo ndugu yao hapo juu Sina mtandao
Kuna fact umeweka za wasukuma ni sahihi...

1. Ushamba
2.kushangaa
3.ukarimu
4.Redio mkononi
5.wanapenda baiskeli
6.wanapenda lugha Yao
7.Waoga
9.Imani za kishirikina
10.kupenda nguo za special na kung'ara 😊
11.kupenda ugali wa Dona
 
haah sawa kumbe nitaoa kwa wakurya tu sasa huko mashemeji watanichanganya!
Wakurya wana hulka ya hasira hasira yaan MWANAMKE anaweza kukuchokoza makusudi Ili umpige ukimpiga NDIO anajua kua unampenda Kwa dhati......🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣😂😂😂😂
 
Labda ulionyesha dharau kwao. Ukiwadharau ndio utawajua!!
mimi nilifka pale kama mgeni, nikawasalimia vizuri tu, (hawakupokea salam) nikaona isiwe tabu nikaenda hatua ya pili (nikaeleza shida yangu), lakin cha ajabu walikaushia kama vile hawanisikii! Walichosema; "huyu jamaa anajifanya wa mjini sasa ngoja tumuone" waliongea mengi kwa kisukuma nilielewa machache sana. Dah wasukuma ni wanoko!
 
Duniani kote iko hivyo. Ukienda Ujerumani usijaribu kuwasalimia kwa Kiingereza hawatakujibu kabisa hasa mitaani na wanaweza kukutenda. Jitahidi kila ukienda sehemu ambayo wanatumia lugha yao jifunze lugha yao hasa salamu.
kiswahili ni lugha ya kila mtanzania, niliongea lugha ya taifa wala sikuongea kifaransa! Na wale sio kwamba hawajuwi kiswahili bali ni dharau na ubinafsi uliotukuka[emoji815]
 
Mimi nimekupa somo la intel basi kama hutaki baki hivyo hivyo!
nimekwambia niliongea lugha ya taifa ili tuelewane (nyerere hakuwa mjinga), sio kwamba mimi sikuwa na uwezo wa kuchapa kihaya. Mkuu nimekuelewa lakini wale walionyesha dharau wazi wazi!!

mimi nimekupa somo la intel basi kama hutaki baki hivyo hivyo!
nawewe kama hujaelewa nenda hivyo hivyo!
 
" Baiskeli zina matajiri ya kila rangi "
" kuna baiskeli zina matajiri mekundu, ya njano, kijani, ya purple na ya bluu "

Mkuu hizo statement hapo juu zilivyo ndo umemaanisha hivyo au [emoji848]
 
" Baiskeli zina matajiri ya kila rangi "
" kuna baiskeli zina matajiri mekundu, ya njano, kijani, ya purple na ya bluu "

Mkuu hizo statement hapo juu zilivyo ndo umemaanisha hivyo au [emoji848]
[emoji38]sjuwi alikuwa na haraka za wapi! Mm nadhani alisema
baiskel zina matajiri ya kila rangi
badala ya "matajiri wana baiskeli za kila rangi"
 
Back
Top Bottom