Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Laki...Abdul Sykes alichukua uongozi wa AA kwa kutumia vurugu na ubabe, hakukuwa na uchaguzi uliomuweka madarakani, nadhani hii ndio sababu iliyomfanya ashindwe kirahisi na Nyerere kwenye uchaguzi wa TAA. Abdul alikuwa kijana sana hakuwa na busara za uongozi
Kiukweli hii historia sikuwa naijua wewe ndio umenifungua mambo mengi, lakini pale kwenye mapungufu ndio na sisi tunarekebisha, mfano ni Abdul Sykes alipochukua madaraka kwa wapinduzi ya vurugu na ubabe, hukutujulisha, hapa ndio tunarekebisha.Laki...
Kabla ya mimi kueleza jinsi Schneider Abdillah Plantan alivyosimama kidete kumtoa kaka yake Thomas Saudtz Plantan katika uongozi wa TAA mwaka wa 1950 ili vijana Abdul na Dr. Kyaruzi wachukue uongozi kuna yeyote alikuwa anaijua historia hii?
Laki...kiukweli hii historia sikuwa naijua wewe ndio umenifungua mambo mengi, lakini pale kwenye mapungufu ndio na sisi tunarekebisha, mfano ni Abdul Sykes alipochukua madaraka kwa wapinduzi ya vurugu na ubabe, hukutujulisha, hapa ndio tunarekebisha
Ndugu Mzee Said,hapa kwa taarifa hii inaondoa vipi ukweli kwamba Mwalimu alianza siasa/harakati kabla ya kukutana na kina Sykes na timu yao?May Day,
Unazijua Nyaraka za Sykes?
Mimi zimeniwezesha kuandika kitabu kizima kuhusu historia ya TAA na TANU na uhuru wa Tanganyika.
Kubwa zaidi zimeniwezesha kumjua Nyerere kuanzia siku ya kwanza anafika nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa wa Aggrey na Sikukukuu mwaka wa 1952 akiongozana na Joseph Kasella Bantu.
Nyaraka hizi na kumbukumbu za Sykes zimeniwezesha kujua historia ya Chief David Kidaha Makwaia na Abdul Sykes katika juhudi ya kumpata kiongozi wa kuongoza TAA na kuunda TANU kati ya mwaka wa 1951 na 1953.
Ungejuaje kama Chief Kidaha alimtangulia Nyerere katika kufikiriwa kuongoza TANU kama si kumbukumbu hizi?
Ulikuwa unajua kuwa baada ya juhudi hizi kushindwa ndiyo Hamza akamtaka Abdul amsaidie Nyerere kuingia katika uongozi wa TAA 1953 katika kikao kilichofanyika nyumbani kwa Hamza Mwapachu Nansio na kuhudhuriwa na Abdul na Ali Mwinyi Tambwe?
Wazalendo hao wawili hapo juu wana historia ya kusisimua ukiisikia kwani hawa wawili ndiyo waliomleta Julius Nyerere katika ulingo wa siasa za TAA Dar es Salaam.
Ukijua historia za wazalendo hawa utakuwa umefungua mlango mpya katika historia ya Mwalimu Nyerere, TANU na historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.
Hivi ushaiuliza kama nisingefunguliwa nyaraka hizi historia ya uhuru ingekuwaje si ingejaa nusu ukweli kama ilivyo katika kitabu kilichoandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni?
Naamini unajua kuwa Nyaraka za Sykes hivi sasa zinaonyeshwa katika Kavazi la Mwalimu Nyerere kama nyaraka za kuaminika kuhusu historia ya Mwalimu Nyerere.
Angalia na jaribu kusoma hiyo barua ya mwaka wa 1953 na angalia ni nani walikuwa viongozi wa TAA kuelekea kuunda TANU:
![]()
NYARAKA ZA SYKES KATIKA KAVAZI LA MWALIMU NYERERE
Nyaraka kutoka kwa Kavazi la Mwalimu Nyerere ikionesha nyaraka kutoka jalada za Ally Sykes Angalia uongozi wa TAA 1953 pamoja na Mwali...mohamedsaidsalum.blogspot.com
May Day,Ndugu Mzee Said,hapa kwa taarifa hii inaondoa vipi ukweli kwamba Mwalimu alianza siasa/harakati kabla ya kukutana na kina Sykes na timu yao?
Au inakanusha vipi kwamba Mwalimu alikuwa anawasiliana na watu wa Dar kuhusu siasa/harakati za uhuru?
Nadhani tunapopishana ni hivi unavyoegemea sana kwenye nyaraka za Sykes au maelezo ya kundi moja. Hivi ni nani mwingine aliandika tofauti na Sykes?
Hakuna anayebeza mchango au nafasi ya kina Sykes na wenzake, ila bado kuna wengine nyuma waliokuwa na mchango na labda hawakupata nafasi ya kuandika kama Bw sykes, na hawa ndio wamekuwa mara kwa mara wakitajwa kama Wazee wa Dar, huenda hawakuwa na nafasi/uwezo kama kina Sykes ila sidhani kama ni sawa kuwapuuza na kung'ang'ana na kina Sykes na timu yao pekee.
Mwalimu alikuja Dar tayari akiwa anajua anataka nini, kutambulishwa kwa kina Sykes labda ilikuwa ni bahati tu na sidhani kama bila hivyo ingemzuia Mwalimu kuendelea na mission zake. Sasa kwa kuwa sykes haonyeshi/hakusema kama Mwalimu alikuwa na mawasiliano kabla ndio uitake na jamii yote iamini hivyo...kuna Wazee waliokuwa wanawasiliana na Mwalimu na sio kina Sykes.
Kingine kisichoeleweka kutoka kwako na nyaraka za Sykes ni hivi unavyoonyesha kana kwamba Mwalimu alitafutwa tu na kupewa kazi lakini huonyeshi yeye Mwalimu alikuja na nini hata kama Dar alikuwa mgeni, ugeni wa Dar sio ugeni wa siasa au mipango.
Mwalimu aliitwa au alikuja kufundisha Pugu?ni dhahiri wazee wa TAA walimuandaa Nyerere kuwa kiongozi wao toka yuko Tabora baada ya kuridhishwa na uwezo wake wa kiuongozi, wakamuita dar na kupokewa na familia ya Sykes, Hata akina Sykes walivyompokea Nyerere Dar walikuwa wanajua ndio kiongozi wao ajae wa TAA,
Laki...ni dhahiri wazee wa TAA walimuandaa Nyerere kuwa kiongozi wao toka yuko Tabora baada ya kuridhishwa na uwezo wake wa kiuongozi, wakamuita dar na kupokewa na familia ya Sykes, Hata akina Sykes walivyompokea Nyerere Dar walikuwa wanajua ndio kiongozi wao ajae wa TAA,
Mohamed,ngano ni tamthilia iliyosadifu(series). Uongo ni neno linaloonyesha kinyume cha ukweli, si tusi"Mohamed Said, post: 33552747, member: 12431"]
Hii ndiyo sababu ghadhabu zako unazielekeza kwangu kwa maneno makali ya ''ngano,'' ''uongo,'' na lugha za kejeli kama ''ngumi na ''mateke,'' nk.
Tarehe 3/3/1945 ni siku ofisi ipofunguliwa, fair enough!Nyerere hakuwa kiongozi wa TAA Tabora 1945.
Tarehe 3 Machi, 1945 African Association mjini Tabora ilifungua ofisi yake ikiwa na na viongozi wafuatao: Hamisi Simbe (Rais), Ramadhani Nasibu (Makamu wa Rais), M. K. Hemed (Katibu), Chamng'anda Usingizi (Mwenyekiti), Fimbo Mtwana (Mweka Hazina) na Rashidi Mussa (Mkaguzi wa Hesabu).
Rejea # 2 hapo juuJulius Nyerere, wakati huo akifundisha St. Mary's School, alishuhudia sherehe za uzinduzi wa African Association.
Nguruvi3,Mag3 kulikoni? Wengine ''tulichutama mtoni kujisetiri, tukichelea kukimbizana ''
Sisi watu wa Pwani adabu zetu ni kuitika mwito tunapoitwa na Wakubwa kama wewe
Mohamed, utaweza kuwa na stara tuongee kidogo? Ni muda ati
Mwito wako niliupata, niliuitika kwa ukimya kwani wito ulijaa indhara
Naomba tuongee kwa point kwa maana ya hoja kwa hoja bila kuleta hadithi nje ya point
Mohamed,ngano ni tamthilia iliyosadifu(series). Uongo ni neno linaloonyesha kinyume cha ukweli, si tusi
''Ngumi na mateke'' inaturudisha katika kitabu chako (Nyakati za Abdulwahid Sykes) ambako umeeleza Abdul na wenzie kuvamia ofisi na kuchukua madaraka kwa nguvu.
Hakukuwepo na kanuni wala Katiba na kwa mantiki yako maneno nguvu na kuvamia hujafafanua ikiwa waliwachapa wazee wao viboko, waliwatia madole ya macho ama...
Hadi hapo utakapofafanua, sioni matumizi ya 'ngumi na mateke'' ya Mag3 kama yana matatizo. Mag3 amekuwa specific wewe umetumia lugha laini, mantiki yenu ni ile ile Tarehe 3/3/1945 ni siku ofisi ipofunguliwa, fair enough!
1. Hao viongozi walidumu katika madaraka kwa muda gani?
2. Mwalimu aliingia katika uongozi lini na kwa utaratibu gani
Rejea # 2 hapo juu
3. Mwaka 1945 kulikuwa a matawi mangapi ya chama wakati huo Tanganyika
4. Mkutano mkuu wa mwaka 1948 Dar es Salaam nani alihudhuria kutoka tawi jipya Tabora(3/3/1945) miongoni mwa Waanzilishi uliowataka hapo juu.
Tuanzie hapa halafu tutaendelea kuteta jamvini.
Ah Mohamed, ghadhabu za nini asbuhi hii Sheikh. Pata funda la maji muungwanaNguruvi3,
Unaniita tujadili kitabu kilichochapwa miaka 21 iliyopita?
Mbona mlikuwa kimya hamkujadili kitabu cha historia ya TANU (1981)kilichoandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni kilichowafuta wazalendo waasisi wa TANU?
Unataka tujadili historia ya TANU leo baada ya miongo miwili tena tujadili historia ambayo nyote nyie hamkuijua ila baada ya kuandikwa na mimi?
Mimi nawasihi mbakie na ile historia yenu iliyomfuta Abdul Sykes.
Hiyo ndiyo historia rasmi lazima tuiheshimu.
kweli mkuu, Nyerere alivyotoka Tabora, alikuja Dar kufundisha Pugu, tatizo Mohamed Said anatuambia alikuja dar kwa ajili ya kuingizwa TAA, hapo ndio nikachanganya,Mwalimu aliitwa au alikuja kufundisha Pugu?
Habari za Mzee Said ni za kusoma kwa tahadhari.kweli mkuu, Nyerere alivyotoka Tabora, alikuja Dar kufundisha Pugu, tatizo Mohamed Said anatuambia alikuja dar kwa ajili ya kuingizwa TAA, hapo ndio nikachanganya,
Nguruvi3,Ah Mohamed, ghadhabu za nini asbuhi hii Sheikh. Pata funda la maji muungwana
Majuzi si ulinialika hapa kwa indhara, kipi kimebadilika tena
Kwani tumeanza leo mimi na wewe! Kuanzia 2010 tupo kitako jamvini na kwa maneno yako mwenyewe! Wiki mbili zilizopita ukanialika. Mbona hamaki?
Mzee Said, tukae kitako watu wazima tuyazungumze kwa stara
Turejee bandiko #31 sheikh!
Laki,kweli mkuu, Nyerere alivyotoka Tabora, alikuja Dar kufundisha Pugu, tatizo Mohamed Said anatuambia alikuja dar kwa ajili ya kuingizwa TAA, hapo ndio nikachanganya,
May Day,Habari za Mzee Said ni za kusoma kwa tahadhari.
Mohamed Said, uko hapa kwa ajili ya kutupa darsa kuhusu wapigania uhuru wa tanganyika waliosahaulika, umebadili fikra za watu wengi sana kwa elimu yako, wengine ndio tumeujua mchango wa akina Sykes kupitia wewe, kwa heshima uliyojijengea naomba ujibu maswali ya nguruvi3 hapo juu ili tuendelee kupata elimu hii adhimu, inawezekana ukawa mkombozi kwa kutupa historia ya kweli na siku moja kitabu cha Sykes kikaja kutumika kwenye mitaala ya elimu mashuleni, tafadhali usikwepe maswali tupe majibu tuendelee kujifunzaLaki,
Sijasema maneno hayo.
Laki...Mohamed Said, uko hapa kwa ajili ya kutupa darsa kuhusu wapigania uhuru wa tanganyika waliosahaulika, umebadili fikra za watu wengi sana kwa elimu yako, wengine ndio tumeujua mchango wa akina Sykes kupitia wewe, kwa heshima uliyojijengea naomba ujibu maswali ya nguruvi3 hapo juu ili tuendelee kupata elimu hii adhimu, inawezekana ukawa mkombozi kwa kutupa historia ya kweli na siku moja kitabu cha Sykes kikaja kutumika kwenye mitaala ya elimu mashuleni, tafadhali usikwepe maswali tupe majibu tuendelee kujifunza