Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
Haya yanahusiana vipi na bandiko #31Nguruvi3,
Hiyo si lugha ya ghadhabu hata kidogo.
Nimekualika au nimekutaja?
Jina la Abdulwahid Kleist Sykes ndiyo hilo sasa mmefahamu na Mwalimu alikisoma kitabu tena alipelekewa na kijana aliyeoa katika familia yake ambae mimi ni rafiki yangu.
Baada ya kukisoma Mwalimu alizungumza na huyu rafiki yangu.
Prof. Haroub Othman aliomba miadi na Mwalimu wazungumze kuhusu kitabu changu na cha Ali Muhsin Barwani, "Conflict and Harmony in Zanzibar."
Prof. kamuomba Mwalimu na yeye aandike kutujibu.
Hivi sasa rafiki zangu wananiweka katika shinikizo niandike kitabu kingine kuhusu haya na mengine yaliyotokea kutoka kitabu cha Abdul Sykes na mihadhara niliyofanya kueleza upya historia ya TANU.
Wewe unanirudisha nyuma nimjadili Mwalimu Nyerere ambae tayari nimeshaandika historia yake.
Mwaka jana radio, televisheni na magazeti walinipa uwanja kuadhimisha miaka 50 ya kifo cha Abdul Sykes naamini ulibahatika kusoma mfululizo wa makala zilizochapwa na Raia Mwema alizoandika bint yake Aisha "Daisy"Sykes.
Daisy aliwaeleza vizuri sana Abdul Sykes, Hamza Mwapachu na Julius Nyerere alivyokuwa akiwaona nyumbani kwao wakati ule 1950s yeye bint mdogo akisikiliza mazungumzo yao.
Kila wafikapo wageni kwangu haya ndiyo wanayoshinikiza niandike.
Wewe unanirejesha kwenye kitabu kinachokwenda toleo la nne tena unataka tufanye mjadala.
Mag3 unaona? Hii ndiyo ngano anayozomesha mzee wetu.
Pascal Mayalla alisema yapo ya kweli na yapo ya ''urongo'' a.k.a ngano
Mohamed, ukinialika uwe tayari mvumilivu na mwenye stara, mimi sikai juu ya jamvi kusikiliza tu na kumeza kila kinachotupwa!
Kwa Taarifa yako lile bandiko la Kleist alivyokuja Pangani lina makosa pitia usahihishe!
Mag3 , Mkubwa narudi mtoni kuchutama...