Pasco,
Tumia mantiki kidogo tu.
Utanunua mtumwa wa kukutumikia umuue?
Awali nilikuambia kuwa hizo picha za watumwa ulizoweka
si za Zanzibar.
Huo unaosema ni uongo uliotungwa na wamishionari waliokuwa
Afrika katika taarifa zao Ulaya ili waongezewe fedha za misaada.
Pasco,
Soma ulijue somo ndipo ujadili.
Hapa tunazungumza ''atrocities,'' zilizofanywa katika na baada ya
mapinduzi miaka michache iliyopita na bado hii leo tuna tatizo la
Mazombie.
Historia unayotaka kuileta wewe ni ya miaka 200 iliyopita.
Mkuu Maalim, kwa heshma na taadhima, nakuomba kwanza acha chuki zako na wamisionari, pili hata kama lengo lako ni kuutetea Uislamu, lakini mara moja moja kuwa mkweli toka ndani ya nafsi yako, kwa sababu naamini kabisa unayajua fika madhila yaliyowapata ndugu zetu Wamatumbi wakati wa kipindi chote cha utumwa chini ya Wavamizi Waarabu na utawala wao dhalimu!. Hizo picha japo ni za kuchorwa, kiukweli kilichowapata ni kibaya kuliko hata hicho kilichochorwa!. Chini ya utawala dhalimu wa Waarabu, watumwa wote wanaume walihasiwa!, hicho kizazi chote cha machotara, ni Wanaume dhalimu wa Kiarabu kuwaingilia kwa nguvu watumwa wa kike ambao walinunuliwa mahsusi kama wajakazi, na pale waliposhika ujauzito, wamiliki walikuwa huru, kuwaua kwa kuwatoboa matumbo, kutoa, kiumbe ambacho ndicho kilizikwa, na mwili wa mtumwa ulifukiwa tuu kama mzoga!.
Jee wajua kuwa hata baada ya kupigwa marufuku kwa biashaa haramu ya watumwa duniani kote, biashara hii iliendelea kufanyika Zanzibar kwa siri?!. Jee wajua kuna njia za chini kwa chini zimechimbwa Bagamoyo na Zanzibar ambapo watumwa walifichwa kwenye mapango na kupitishwa chini kwa chini hadi baharini?
Jee ulikuwa unajua kuwa kila Sultani, wake zao na watoto zao, walipokufa, walizikwa na watumwa hai?!. Jee wajua kwenye jengo la Beit Al Ajab, kwenye kila milingoti hapo, ndani walimuweka mtumwa hai mwanamume?!. Jee wajua waliofanikisha kukomesha biashaa ya Utumwa Zanzibar ni akina nani?!. Kwa kusaidia tuu, waliokomesha biashara hii dhalimu Zanzibar ni wamisionari, ambao waliingia kabisa mkatataba na Sultani dhalimu wa Zanzibar, ndipo ikukubaliwa kuwa watumwa wote wenye kutaka kuwa huru, lazima wagombolewe kwa wale matajii wao kulipwa fedha, ambapo hao wamisionari, waliwalipia fedha kuwagomboa, na ndipo wakaanzisha kanisa la kwanza kabisa Afrika Mashariki, lilianzia Zanzibar, na waumini wa kwanza, ni watumwa waliogombolewa!. Pitia hapa
'Missionaries and Muslims in East Africa
A report on slavery and the slave trade in Zanzibar, Pemba ...
AFRICAN REVOLT| Slave Revolt | Zanzibar Revolt ...
The impact of the slave trade on Africa - Le Monde ..
Jee wajua kitu walichofanyiwa Waarabu dhalimu hawa baada ya yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, ilikuwa ni katika kujibu tuu au payback ya "what goes around, comes around?!", ila hapa naomba kukiri wazi, kuwa sio Waaabu wote kabisa walikuwa madhalimu kwa kuwatenda vibaya watumwa wao!, wako Waarabu ambao waliwatendea wema watumwa wao, na wamisionari walipotaka kuwagomboa, watumwa hao walikataa kwa ridhaa zao, hivyo wakaendelea kubaki utumwani kwa ridhaa zao wenyewe!.
Wako Waarabu, waliwapenda watumwa wa kike, japo waliwanunua kama vijakazi kwa ajili ya kuwafanya watumwa wa mapenzi, lakini wapo waliotokea na kuwapenda kwa mapenzi ya dhati, wengine wakawaoa na kuwa masuria, na wakawazalia watoto!. Namfahamu mmoja wa watoto wa Sultani ambaye alizaliwa na suria, na yungalipo hai hadi leo!.
Hizi ni picha za Zanzibar!, ni picha za kupigwa kweli, na nyingine japo ni za kuchorwa, lakini zinaonyesha ukweli halisi!.
Pasco