Sultani wa Zanzibar alikaa Tanganyika kwa siku 5 kabla ya kuelekea Uingereza kwa hifadhi ya kisiasa

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
SULTANI JAMSHID ALIYOISHI DAR ES SALAAM KAMA MKIMBIZI AKIJITAYARISHA KWENDA NCHI YA TATU ILI TANGANYIKA ISIWE NA MGOGORO NA ZANZIBAR.

Mchezo huu hauhitaji hasira, mtu ni kwao, karibu sana Sultan Jamshid.

TOKA MAKTABA:
AIISHUKURU SERIKALI YA TANGANYIKA KWA KUMPA NJIA YA KUPITA KUELEKEA UGHAIBUNI

Hapa clip fupi akitoa shukrani kwa serikali ya Uingereza kumpatia hifadhi na pia serikali ya Tanganyika kwa kumpa ruhusa kupita Dar es Salaam baada ya mapinduzi ili afanye taratibu za kwenda Uhamishoni

View: https://m.youtube.com/watch?v=TKE2C5svBLo

Maafisa nchini Kenya walifikiri kwamba kuingia kwa Sultan Mombasa kunaweza kusababisha hali tete ya usalama na misukosuko ya Waarabu wanaoishi Mombasa; hivyo, iliamuliwa kutompa kimbilio, wala kwa wasaidizi wake; badala yake, iliamuliwa waelekee Dar es-salaam.

Jijini Dar es-Salaam, Sultani na msafara wake waliwekwa katika kizuizi cha nyumbani katika nyumba mbili za serikali zinazolindwa na polisi na ziko katika eneo la kifahari la Oyster Bay.

Nyumba moja ilitengwa kwa HM. Sultani na familia yake huku wa pili akikalisha wasaidizi wake. Walikaa Dar es Salaam kuanzia tarehe 13 hadi 18 Januari 1964, siku ambayo walisafiri kwa ndege kuelekea Uingereza.

Nilipata heshima ya kukutana na HM. Sultan Jamshid - ambaye hakuwa amejiuzulu - huko Uingereza, na alinielezea jinsi hali mbaya, tarehe 12.01.1964, ilimlazimu kuondoka katika nchi yake anayoipenda. Alisema: karibu saa 6 asubuhi, mtu ambaye alimfahamu, Haj Hussain, alikuja kwenye Ikulu na kumtaka aondoke kwenye Ikulu kwa usalama wake. Sultani alikataa kwa ujasiri, akisema kwamba hataondoka nchini na kuruhusu raia wake kuliwa na kundi la watu; na kwamba kama hakutakuwa na chaguo ila kufa, basi angependelea kupigana hadi kufa miongoni mwa watu wake. Taarifa hii ilithibitishwa na Mervyn Smithyman, Katibu Mkuu wa Marehemu Waziri Mkuu wa Zanzibar, katika taarifa yake ya tarehe 16 Januari 1964. HM. Sultani anashikilia kuwa: Balozi Hilal Al Barwani, alikuja baada ya Haj Hussain kuondoka Mahali hapo na kufanikiwa kumshawishi aondoke Ikulu pia. Barwani alimweleza Sultani kwamba haikuwa kwa maslahi yake tu kufanya hivyo bali kwa maslahi ya utawala, nchi, kiti cha enzi na watu wote kwa wakati mmoja....

Nilipata heshima ya kukutana na HM. Sultan Jamshid - ambaye hakuwa amejiuzulu - huko Uingereza, na alinielezea jinsi hali mbaya, tarehe 12.01.1964, ilimlazimu kuondoka katika nchi yake anayoipenda. Alisema: karibu saa 6 asubuhi, mtu ambaye alimfahamu, Haj Hussain, alikuja kwenye Ikulu na kumtaka aondoke kwenye Ikulu kwa usalama wake. Sultani alikataa kwa ujasiri, akisema kwamba hataondoka nchini na kuruhusu raia wake kuliwa na kundi la watu; na kwamba kama hakutakuwa na chaguo ila kufa, basi angependelea kupigana hadi kufa miongoni mwa watu wake. Taarifa hii ilithibitishwa na Mervyn Smithyman, Katibu Mkuu wa Marehemu Waziri Mkuu wa Zanzibar, katika taarifa yake ya tarehe 16 Januari 1964. HM. Sultani anashikilia kuwa: Balozi Hilal Al Barwani, alikuja baada ya Haj Hussain kuondoka Mahali hapo na kufanikiwa kumshawishi aondoke Ikulu pia. Barwani alimweleza Sultani kwamba haikuwa kwa maslahi yake tu kufanya hivyo bali kwa maslahi ya utawala, nchi, kiti cha enzi na watu wote kwa wakati mmoja.... Soma zaidi kwenye:
 
1735386710046.jpeg

Jamshid bin Abdullah Al Busaidi GCMG Sultani wa mwisho kutawala Zanzibar. Alizaliwa: 16 Septemba 1929 (umri wa miaka 95), Zanzibar Tanzania.

Jamshid bin Abdullah Al Busaidi GCMG is a Zanzibari royal who was the last reigning Sultan of Zanzibar. Born: 16 September 1929 (age 95 years), Zanzibar Tanzania.
 
13 Jan 2000 — Zanzibar President Salmin Amour has granted amnesty to former ruler of the island, Sultan Jamshid bin Abdullah

Uhamishoni Uingereza, mwaka 2000 rais wa Zanzibar Dr. Salimin Amour almaaruf Komandoo, ampatia uhuru Jamshid bin Abdullah kurejea Zanzibar.​

Jamshid bin Abdullah alitoroka Zanzibar kwa kutumia merikebu ya kifahari baada ya wanamapinduzi kuliteka kasri lake.

Wiki mbili baadaye Gazeti la The New York Times liliripoti kwamba hali ya kifedha ya Sultan nchini Uingereza haikuwa nzuri hivyo ilimlazimu kuondoka katika hoteli ya kifahari aliokuwa akiishi karibu na kasri la Buckingham hadi hoteli ya Modest iliopo karibu na eneo la Bayswater.
Jamsheed na mkewe Sheikha Anisa na wanawe 1964 mjini London

Chanzo cha picha,Getty Images
Maelezo ya picha,Jamsheed na mkewe Sheikha Anisa na wanawe 1964 mjini London
Gazeti hilo linasema kwamba mwezi Mei 1964, serikali ya Uingereza ilimpa Sultan huyo paundi elfu moja.

Fedha hizo zilimsaidia kuishi katika nyumba moja iliokuwa katika barabara tulivu, katika eneo la SouthSea, Hampshire.

Mwaka 2000 , aliyekuwa rais wa Zanzibar Salimin Amour almaaruf Komandoo alimpatia msamaha na uhuru Jamshid bin Abdullah kurejea Zanzibar .

Rais wa serikali ya Mapinduzi Dkt. Salmon Amour wakati huo alisema kwamba Jamshid alikuwa huru kurudi Zanzibar lakini sio kama sultan bali kama raia.

Na kwa zaidi ya miaka 56 alioishi katika hoteli hiyo iliopo karibu na ufukwe wa bahari nchini Uingereza , Sultan huyo hakuvutia watu.
Jamsheed

Chanzo cha picha,Getty Images

Mwandishi Ned Donovan, aliyekuwa akifuatilia hadithi hiyo ya Sultan alisema: Sikupata mkaazi hata mmoja ambaye alifahamu uwepo wake , hakuzungumza na vyombo vya habari , aliishi maisha ya kunyamaza sana .

Fahamu uhusiano wa Zanzibar na Oman
Zanzibar ipo katika bahari hindi mashariki mwa pwani ya bara Afrika. Kisiwa hicho kiliungana na Tanganyika bara lakini kina rais wake na bunge ambalo linfahamika kama baraza la wawakilishi.

Baada ya kuwa kituo cha utumwa , kilivutia wakaazi wengi waliokuwa Waafrika, Waarabu, Wazungu na Wahindi.

Asili ya watu visiwani Zanzibar ni mchanganyiko wa Waafrika walio wengi, Waarabu wa Omani na Yemen mbali na Wahindi. Asilimia 98 ya wakaazi wa kisiwa hicho ni Waislamu.

Zanzibar hujulikana kama kisiwa cha karafuu kutokana na wingi wa zao la karafuu . Wakati Waarabu wa Omani walipokiteka kisiwa cha Mombasa kutoka kwa Wareno 1698, Zanzibar na Pemba zilikua chini ya watawala wa Kiarabu kutoka Omani, na baada ya zaidi ya karne moja waliondoka na kukiwacha kisiwa hicho chini ya utawala wa wakaazi.
Sultan wa kwanza kuishi Zanzibar alikuwa Saeed bin Sultan baada ya kukitembelea kisiwa hicho mara kadhaa baada ya mwaka wa 1830, wakati huo akipanua ushawishi wake katika pwani ya Afrika ya mashariki.
Baada ya kifo chake 1856 , utawala wa Sultan uligawanywa kati ya wanawe wawili , mmoja akiwa Oman na mwengine akisalia Zanzibar, na kisiwa hicho kilikuwa chini ya utawala wa Uingereza baada ya kifo cha sultan Bargash bin Said.
 
TAMKO LA RAIS DKT. SALMIN AMOUR mwaka 2000

“Kwa moyo wa ustaarabu na maridhiano, ninayo furaha kutangaza kuwa alitoa msamaha kwa Mfalme (Sultani) Jamshid bin Abdallah bin Khalfan, ambaye aliikimbia nchi baada ya mapinduzi,” Amour. alisema katika hotuba yake ya kuadhimisha miaka 36 ya mapinduzi ya Zanzibar. "Yuko huru kurejea nyumbani - si kama mfalme, lakini raia wa kawaida - na serikali iko tayari kumsaidia kutulia," Amour alisema.
Jamshid ambaye sasa ana umri wa miaka 69, aliitawala Zanzibar kwa takriban miezi sita kabla ya kung’olewa madarakani Januari 12, 1964. Alirithi kiti cha enzi kutoka kwa baba yake Ahmed bin Abdallah bin Said, ambaye alifariki dunia baada ya kutawala kwa miaka mitatu.

TOKA MAKTABA :

kumsalimia na kumjulia hali yake.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi akiagana na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Salmin Amour Juma, baada ya kumaliza mazungumzo alipofika nyumbani kwake Migombani Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar kwa ajili ya kumsalimia na kumjulia hali yake.(Picha na Ikulu)
 
Maridhiano na kusahemeana ndiyo uungwana mkubwa.

Komandoo Dkt. Salmin Amour wakati wa maadhimisho ya miaka 36 ya Mapinduzi Matukufu mwaka 2000 alitoa msahama na kufutilia mbali tamko la kumpiga marufuku Sultan Jamashid kurudi Zanzibar

Toka maktaba :
1 April 2024

View: https://m.youtube.com/watch?v=jFWhuVLkTYw
 
Hatuwataki Masultani iwe huyu Mwarabu au yule Mchaga wa CHADEMA tunasema NO! NO! NO!.

Hah Hah wanasiasa wanasema hakuna maridhiano wakiwa majukwaani, lakini uso kwa uso wakiwa wapinzani wawili huongea kwa kusema usisikize yale nilosema jukwaani au katika press conference. Tega masikio haya nayokwambia tukiwa wawili bila mihemko ya jukwaani

View: https://m.youtube.com/watch?v=nvlieD3r1Fo&pp=ygUUU2FsbWluIEFtb3VyIGhvdHViYSA%3D
Siasa na utawala inatakiwa utulivu wa maamuzi. Mtu kwao hata komandoo Dkt. Salmin Amour pamoja na siasa zake za 'kimapinduzi daima' , tunaona alitambua kuwa haki ya mzaliwa wa Zanzibar haifutiki.

View: https://m.youtube.com/watch?v=g4RV-O9-ats&pp=ygUUU2FsbWluIEFtb3VyIGhvdHViYSA%3D
 
Zanzibar+Oman=...............
Sijui Mhe. Nyerere aliwaza nini kuwaunga na Bara hawa jamaa
 
SULTANI JAMSHID ALIYOISHI DAR ES SALAAM KAMA MKIMBIZI AKIJITAYARISHA KWENDA NCHI YA TATU ILI TANGANYIKA ISIWE NA MGOGORO NA ZANZIBAR.

Mchezo huu hauhitaji hasira, mtu ni kwao, karibu sana Sultan Jamshid.

TOKA MAKTABA:
AIISHUKURU SERIKALI YA TANGANYIKA KWA KUMPA NJIA YA KUPITA KUELEKEA UGHAIBUNI

Hapa clip fupi akitoa shukrani kwa serikali ya Uingereza kumpatia hifadhi na pia serikali ya Tanganyika kwa kumpa ruhusa kupita Dar es Salaam baada ya mapinduzi ili afanye taratibu za kwenda Uhamishoni

View: https://m.youtube.com/watch?v=TKE2C5svBLo

Maafisa nchini Kenya walifikiri kwamba kuingia kwa Sultan Mombasa kunaweza kusababisha hali tete ya usalama na misukosuko ya Waarabu wanaoishi Mombasa; hivyo, iliamuliwa kutompa kimbilio, wala kwa wasaidizi wake; badala yake, iliamuliwa waelekee Dar es-salaam.

Jijini Dar es-Salaam, Sultani na msafara wake waliwekwa katika kizuizi cha nyumbani katika nyumba mbili za serikali zinazolindwa na polisi na ziko katika eneo la kifahari la Oyster Bay.

Nyumba moja ilitengwa kwa HM. Sultani na familia yake huku wa pili akikalisha wasaidizi wake. Walikaa Dar es Salaam kuanzia tarehe 13 hadi 18 Januari 1964, siku ambayo walisafiri kwa ndege kuelekea Uingereza.

Nilipata heshima ya kukutana na HM. Sultan Jamshid - ambaye hakuwa amejiuzulu - huko Uingereza, na alinielezea jinsi hali mbaya, tarehe 12.01.1964, ilimlazimu kuondoka katika nchi yake anayoipenda. Alisema: karibu saa 6 asubuhi, mtu ambaye alimfahamu, Haj Hussain, alikuja kwenye Ikulu na kumtaka aondoke kwenye Ikulu kwa usalama wake. Sultani alikataa kwa ujasiri, akisema kwamba hataondoka nchini na kuruhusu raia wake kuliwa na kundi la watu; na kwamba kama hakutakuwa na chaguo ila kufa, basi angependelea kupigana hadi kufa miongoni mwa watu wake. Taarifa hii ilithibitishwa na Mervyn Smithyman, Katibu Mkuu wa Marehemu Waziri Mkuu wa Zanzibar, katika taarifa yake ya tarehe 16 Januari 1964. HM. Sultani anashikilia kuwa: Balozi Hilal Al Barwani, alikuja baada ya Haj Hussain kuondoka Mahali hapo na kufanikiwa kumshawishi aondoke Ikulu pia. Barwani alimweleza Sultani kwamba haikuwa kwa maslahi yake tu kufanya hivyo bali kwa maslahi ya utawala, nchi, kiti cha enzi na watu wote kwa wakati mmoja....

Nilipata heshima ya kukutana na HM. Sultan Jamshid - ambaye hakuwa amejiuzulu - huko Uingereza, na alinielezea jinsi hali mbaya, tarehe 12.01.1964, ilimlazimu kuondoka katika nchi yake anayoipenda. Alisema: karibu saa 6 asubuhi, mtu ambaye alimfahamu, Haj Hussain, alikuja kwenye Ikulu na kumtaka aondoke kwenye Ikulu kwa usalama wake. Sultani alikataa kwa ujasiri, akisema kwamba hataondoka nchini na kuruhusu raia wake kuliwa na kundi la watu; na kwamba kama hakutakuwa na chaguo ila kufa, basi angependelea kupigana hadi kufa miongoni mwa watu wake. Taarifa hii ilithibitishwa na Mervyn Smithyman, Katibu Mkuu wa Marehemu Waziri Mkuu wa Zanzibar, katika taarifa yake ya tarehe 16 Januari 1964. HM. Sultani anashikilia kuwa: Balozi Hilal Al Barwani, alikuja baada ya Haj Hussain kuondoka Mahali hapo na kufanikiwa kumshawishi aondoke Ikulu pia. Barwani alimweleza Sultani kwamba haikuwa kwa maslahi yake tu kufanya hivyo bali kwa maslahi ya utawala, nchi, kiti cha enzi na watu wote kwa wakati mmoja.... Soma zaidi kwenye:

Unamaanisha hili gaidi liliua,tesa na kuuza wazee wetu utumwani?laanatulah,na sijui kwanini lipo hai hadi leo.
 
Utumwa ulimalizwa kabla ya mwaka 1900 na waingereza. Zanzibar haikuwa na watumwa baada ya hapo na pia raia wa Zanzibar yote hawakuwahi kuwa watumwa ila wale waliouzwa na mchifu kule kwa waungwana Congo ya Mashariki ndiyo wallet wa kwa misafara hadi Bagamoyo kisha kuwekwa sokoni Zanzibar.

Tukumbuke ununuzi wa watumwa ilikuwa biashara inayofanywa na waarabu, wareno, wamatumbi wa maeneo yote ya Afrika, waingereza, waDachi n.k wakapelekwa toka masoko yaliyopo Angola, Senegal, Sofala, Zanzibar n.k maeneo mbalimbali duniani kwenda Brazil, Haiti, Marekani ya Kaskazini, Ottoman Empire yote n.k
 
SULTANI JAMSHID ALIYOISHI DAR ES SALAAM KAMA MKIMBIZI AKIJITAYARISHA KWENDA NCHI YA TATU ILI TANGANYIKA ISIWE NA MGOGORO NA ZANZIBAR.

Mchezo huu hauhitaji hasira, mtu ni kwao, karibu sana Sultan Jamshid.

TOKA MAKTABA:
AIISHUKURU SERIKALI YA TANGANYIKA KWA KUMPA NJIA YA KUPITA KUELEKEA UGHAIBUNI

Hapa clip fupi akitoa shukrani kwa serikali ya Uingereza kumpatia hifadhi na pia serikali ya Tanganyika kwa kumpa ruhusa kupita Dar es Salaam baada ya mapinduzi ili afanye taratibu za kwenda Uhamishoni

View: https://m.youtube.com/watch?v=TKE2C5svBLo

Maafisa nchini Kenya walifikiri kwamba kuingia kwa Sultan Mombasa kunaweza kusababisha hali tete ya usalama na misukosuko ya Waarabu wanaoishi Mombasa; hivyo, iliamuliwa kutompa kimbilio, wala kwa wasaidizi wake; badala yake, iliamuliwa waelekee Dar es-salaam.

Jijini Dar es-Salaam, Sultani na msafara wake waliwekwa katika kizuizi cha nyumbani katika nyumba mbili za serikali zinazolindwa na polisi na ziko katika eneo la kifahari la Oyster Bay.

Nyumba moja ilitengwa kwa HM. Sultani na familia yake huku wa pili akikalisha wasaidizi wake. Walikaa Dar es Salaam kuanzia tarehe 13 hadi 18 Januari 1964, siku ambayo walisafiri kwa ndege kuelekea Uingereza.

Nilipata heshima ya kukutana na HM. Sultan Jamshid - ambaye hakuwa amejiuzulu - huko Uingereza, na alinielezea jinsi hali mbaya, tarehe 12.01.1964, ilimlazimu kuondoka katika nchi yake anayoipenda. Alisema: karibu saa 6 asubuhi, mtu ambaye alimfahamu, Haj Hussain, alikuja kwenye Ikulu na kumtaka aondoke kwenye Ikulu kwa usalama wake. Sultani alikataa kwa ujasiri, akisema kwamba hataondoka nchini na kuruhusu raia wake kuliwa na kundi la watu; na kwamba kama hakutakuwa na chaguo ila kufa, basi angependelea kupigana hadi kufa miongoni mwa watu wake. Taarifa hii ilithibitishwa na Mervyn Smithyman, Katibu Mkuu wa Marehemu Waziri Mkuu wa Zanzibar, katika taarifa yake ya tarehe 16 Januari 1964. HM. Sultani anashikilia kuwa: Balozi Hilal Al Barwani, alikuja baada ya Haj Hussain kuondoka Mahali hapo na kufanikiwa kumshawishi aondoke Ikulu pia. Barwani alimweleza Sultani kwamba haikuwa kwa maslahi yake tu kufanya hivyo bali kwa maslahi ya utawala, nchi, kiti cha enzi na watu wote kwa wakati mmoja....

Nilipata heshima ya kukutana na HM. Sultan Jamshid - ambaye hakuwa amejiuzulu - huko Uingereza, na alinielezea jinsi hali mbaya, tarehe 12.01.1964, ilimlazimu kuondoka katika nchi yake anayoipenda. Alisema: karibu saa 6 asubuhi, mtu ambaye alimfahamu, Haj Hussain, alikuja kwenye Ikulu na kumtaka aondoke kwenye Ikulu kwa usalama wake. Sultani alikataa kwa ujasiri, akisema kwamba hataondoka nchini na kuruhusu raia wake kuliwa na kundi la watu; na kwamba kama hakutakuwa na chaguo ila kufa, basi angependelea kupigana hadi kufa miongoni mwa watu wake. Taarifa hii ilithibitishwa na Mervyn Smithyman, Katibu Mkuu wa Marehemu Waziri Mkuu wa Zanzibar, katika taarifa yake ya tarehe 16 Januari 1964. HM. Sultani anashikilia kuwa: Balozi Hilal Al Barwani, alikuja baada ya Haj Hussain kuondoka Mahali hapo na kufanikiwa kumshawishi aondoke Ikulu pia. Barwani alimweleza Sultani kwamba haikuwa kwa maslahi yake tu kufanya hivyo bali kwa maslahi ya utawala, nchi, kiti cha enzi na watu wote kwa wakati mmoja.... Soma zaidi kwenye:

Kwanini hajakimbilia kwao Oman
 
Back
Top Bottom