Suluhisho la Kudumu la Kero Zote za Muungano, na Dawa ya Kutibu Sumu ya Ubaguzi wa Utanganyika na Uzanzibari ni Kuwa na Serikali Moja ya JMT?

Intonjanda?Kweli wewe msugunsu-mnyamwezi.Hapo bado haujaitaja Ntalikwa.
 
Raia yeyote atakayeonekana kutokutii ina maana Yuko tayari kupambana.
Ngoja tumpate Rais ambaye atakuwa Dikteta Mzalendo Muadilifu ili Wananchi wote tunyooshwe pamoja na majizi ya mali za Nchi 👁

Huyo Rais akipatikana atawale kwa miaka isiyopungua 30 bila kuwepo uchaguzi wa Rais 👁

Ni maono tu 👁😇🤠
 
Mkuu Tindo , huu muungano wetu adimu na adhimu una dhima ndani yake ambayo ni kama spell fulani, ukiuzungumzia tuu muungano in a negative way with intention ya kuuvunja, unavunjika wewe!, yanakukuta ya kukuta!.

Unamjua huyo aliyesema "muungano kama koti la kuazima lilikubana unalivua" ni nani na kilimkuta nini baada ya kutamka maneno hayo?.

Unakumbuka kilichumkuta Abudul Jumbe?.
Hakuna anayelazimisha serikali moja, aliyetaka serikali moja ni Karume!
Wazo la kuwa na Serikali moja lilikuwa ni wazo la Karume
View attachment 2999472
Lakini ni Nyerere ndiye alikataa!
P
 
Ndio maana nimekuambia ni muungano wa shuruti sio wa ridhaa. Ukiona muungano unalindwa kwa kupoteza uhai wa wanaouhoji au wasio ridhia, huo sio muungano bali kafara. Kizazi hiki sio Cha kuongozwa na makafara ya hao wazee washirikina tena. Narudia ile kauli yangu, muungano huu hauna miaka 20 mbele lazima uvunjike, vinginevyo muundo ubadilike.
 
Ukitaka 1 au 3 hilo ni jambo jipya Kabisa linalopaswa kuanzia Upya kwa Wananchi wa Tanzania na Wananchi wa Zanzibar
Siyo jambo jipya bhana..
Mbona hilo lilishafanywa kupitia rasimu ya Katiba ya Warioba, na maoni ya wananchi wengi yalikuwa ni serikali 3?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…