Suluhisho la kulipa fidia ya mabilion nje ya nchi ni kubadili jina la nchi

Suluhisho la kulipa fidia ya mabilion nje ya nchi ni kubadili jina la nchi

Bado tunaendelea kupigwa kwenye kesi za fidia na makampuni ya kigeni.. Tunalipa mabilioni ya shilingi na mabilion ya dola kwa makosa ya watu wachache tuu.. Mostly kutoka chama chawala
Hakuna hata kesi moja tuliwahi kushinda..
Mikataba tuliyosaini kimagumashi inatutesa sasa.. Waliosaini kwa niaba yetu wapo na wanaendelea kula bata..hawana wasiwasi kabisa.. Na ni hao hao kati yao kwenye hizo fidia nao wana cha kwako😳🤬🤬🤬
Washeria wetu wa serikali
Ni vihiyo
Hawana uzalendo
Wananunulika
Ni mbumbumbu wa sheria za kimataifa na uwekezaji
Ni waoga
Mwisho wa siku tunaoumia ni sisi wananchi wa kawaida

Sasa imetosha.. Tumevumilia imefika mwisho.. Taifa linalodaiwa ni Taifa na nchi ya Tanzania
Hili lina lina nuksi
Hili jina lina sifa mbaya
Hili jina lina migogoro Mungu
Hili jina lina madeni mengi sana
Kuna shida gani tukiachana nalo sasa?
Turudi kwenye Tanganyika yetu..
Ni jina zuri
Linapendeza
Halina kashfa
Halina madeni
Halina nuksi
Halimilikiwi na chama chawala
Tubadili jina kutoka Tanzania kwenda Tanganyika.. Na madeni yote yatakoma.. Maana anayedaiwa ni Tanzania sio Tanganyika
Marehemu hadaiwi bali husamehewa madeni..
View attachment 3140428
Naunga mkono hoha turudi tu TANGANYIKA madeni tuyakimbie ,tujitoe na Zanzibar.
 
Naunga mkono hoja, lakini tusitegemee watu wale wale vyama hivi hivi vilivyopo kufanya hayo mabadiliko.....wanahitakika vijana wenye mtazamo mpya mfano wa Ibrahim Traoré wenye uthubutu na kibri cha kufanya wanachokiamini.

Kwa bahati mbaya sana sioni hata mmoja mwenye mwelekeo wa kimapinduzi iwe jeshini, vyama vya siasa wala vyuo na mashuleni. Naona kundi la watu waoga wasiojiamini, waliotayari kusifia matendo au kauli za watawala.....

Tujipe muda labda baada ya miaka 50 kuanzia sasa... Yanafanyika tunayoyatamani bila ya mimi na wengi wengi humu kuyashuhudia. 🤓
 
Screenshot_20241101-131027~2.jpg
 
Eti ukibadili jina la nchi madeni yanafutika. Hizi fikra ndizo zinafanya hayo makampuni ya nje yanawakupua mabilioni.
Dawa ni kufata makubaliano kwenye mkataba. Hata kama upande mmoja tunataka kuvunja huo mkataba pia ziko taratibu zake ndani ya mkataba kuhakikisha haki kwa wote.
Pia dawa ya deni nikulipa sio kulialia na kukwepa kwa Sheria za ndani ya nchi. hukonje pia kuna Sheria za kimataifa kwa hiyo hakuna kukwepa
Ni mawazo yangu ya kijinga tu blo na kuchokoza mada😁
 
Naunga mkono hoja, lakini tusitegemee watu wale wale vyama hivi hivi vilivyopo kufanya hayo mabadiliko.....wanahitakika vijana wenye mtazamo mpya mfano wa Ibrahim Traoré wenye uthubutu na kibri cha kufanya wanachokiamini.

Kwa bahati mbaya sana sioni hata mmoja mwenye mwelekeo wa kimapinduzi iwe jeshini, vyama vya siasa wala vyuo na mashuleni. Naona kundi la watu waoga wasiojiamini, waliotayari kusifia matendo au kauli za watawala.....

Tujipe muda labda baada ya miaka 50 kuanzia sasa asa... Yanafanyika tunayoyatamani bila ya mimi na wengi wengi humu kuyashuhudia. 🤓
Kwanza ccm na virusi vyake vyote ikufe na kufutika kwenye uso wa dunia
 
Eti ukibadili jina la nchi madeni yanafutika. Hizi fikra ndizo zinafanya hayo makampuni ya nje yanawakupua mabilioni.
Dawa ni kufata makubaliano kwenye mkataba. Hata kama upande mmoja tunataka kuvunja huo mkataba pia ziko taratibu zake ndani ya mkataba kuhakikisha haki kwa wote.
Pia dawa ya deni nikulipa sio kulialia na kukwepa kwa Sheria za ndani ya nchi. hukonje pia kuna Sheria za kimataifa kwa hiyo hakuna kukwepa
Bora wazo la jamaa ninaweza kusema sababu ni impossible huenda alikuwa analeta utani (tongue in cheek) wewe jibu lako linaonyesha ni vipi tutaendelea kuliwa mpaka Kingdom Come..., yaani mikataba ya kipuuzi ambayo watu wameingia kabisa wakijua kwamba ikivunjwa watalipwa wao na majambazi wenzao tuendelee kulipa ? Yaani badala ya kulaumu walioingia hio Mikataba ya kipuuzi tunalalamikia wale ambao wamepata guts na kuamua kuachana na huu upuuzi ?

Yaani kwa mantiki yako hata zile Rada za kina mzee wa Vijisenti walivyotaka tuingie na kuingiza nchi kwenye madeni tungelipa tu na kuendelea nayo sababu ni mkataba ndio ulisema hivyo...
 
Mshana Jr
Tulisahau kuweka LTD kwenye jina letu Ili madeni yafe nalo.😂.
Kuhusu mawakili wetu ni janga la kitaifa hata Nimrod Mkono waliyekuwa wanamuajiri alikuwa anawatumia wazungu wasio na uchungu wa nchi hii huku akiweka bonge la Cha juu.
 
suluhisho ni rahisi Sana. Tuanze kuwanyonga Kama huko china au Kwa style ya Jerry Rawlings au ikishindikana Kabisa tuwachukulie sheria mkononi Kama vibaka mtaani Kwa waziri yeyote aliye- sign mkataba wa magumashi…
 
Back
Top Bottom