Suluhisho la kulipa fidia ya mabilion nje ya nchi ni kubadili jina la nchi

Naunga mkono hoha turudi tu TANGANYIKA madeni tuyakimbie ,tujitoe na Zanzibar.
 
Naunga mkono hoja, lakini tusitegemee watu wale wale vyama hivi hivi vilivyopo kufanya hayo mabadiliko.....wanahitakika vijana wenye mtazamo mpya mfano wa Ibrahim Traoré wenye uthubutu na kibri cha kufanya wanachokiamini.

Kwa bahati mbaya sana sioni hata mmoja mwenye mwelekeo wa kimapinduzi iwe jeshini, vyama vya siasa wala vyuo na mashuleni. Naona kundi la watu waoga wasiojiamini, waliotayari kusifia matendo au kauli za watawala.....

Tujipe muda labda baada ya miaka 50 kuanzia sasa... Yanafanyika tunayoyatamani bila ya mimi na wengi wengi humu kuyashuhudia. 🤓
 
Ni mawazo yangu ya kijinga tu blo na kuchokoza mada😁
 
Kwanza ccm na virusi vyake vyote ikufe na kufutika kwenye uso wa dunia
 
Bora wazo la jamaa ninaweza kusema sababu ni impossible huenda alikuwa analeta utani (tongue in cheek) wewe jibu lako linaonyesha ni vipi tutaendelea kuliwa mpaka Kingdom Come..., yaani mikataba ya kipuuzi ambayo watu wameingia kabisa wakijua kwamba ikivunjwa watalipwa wao na majambazi wenzao tuendelee kulipa ? Yaani badala ya kulaumu walioingia hio Mikataba ya kipuuzi tunalalamikia wale ambao wamepata guts na kuamua kuachana na huu upuuzi ?

Yaani kwa mantiki yako hata zile Rada za kina mzee wa Vijisenti walivyotaka tuingie na kuingiza nchi kwenye madeni tungelipa tu na kuendelea nayo sababu ni mkataba ndio ulisema hivyo...
 
Mshana Jr
Tulisahau kuweka LTD kwenye jina letu Ili madeni yafe nalo.😂.
Kuhusu mawakili wetu ni janga la kitaifa hata Nimrod Mkono waliyekuwa wanamuajiri alikuwa anawatumia wazungu wasio na uchungu wa nchi hii huku akiweka bonge la Cha juu.
 
suluhisho ni rahisi Sana. Tuanze kuwanyonga Kama huko china au Kwa style ya Jerry Rawlings au ikishindikana Kabisa tuwachukulie sheria mkononi Kama vibaka mtaani Kwa waziri yeyote aliye- sign mkataba wa magumashi…
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…