Suluhisho la kulipa fidia ya mabilion nje ya nchi ni kubadili jina la nchi

Ila nchi za kiafrika kudaiwa tunajitakia tu wenyewe, laiti kama AU ingekuwa serious hakuna nchi ingedaiwa.

Me ningekuwa ndy mwenyekiti wa AU ningetoa tamko kwamba kama Nchi za ulaya ziliitawala Bara la Africa na wakafanya human and resources exploitation pamoja na torturing kwa watu. Bila kuwalipa fidia Raia wa nchi dhidi ya ukatili huu, basi hizo fedha za mikopo zikawe fidia ya kile kilichoitwa ukoloni na unyonyaji.

Hakuna nchi ya ulaya ambayo haijajengwa na rasilimali kutoka afrika.
Hakuna fidia yeyote tuliyoipata na UN haiwezi kuibua hoja katili kama hizi.

Kukandamizwa tunajitakia ila njia za kujikwamua ni nyingi wakuu.
 
kuna methali isemay mzigo wa mpumbavu haishia begani unajua maana yake? Ndo nchi yetu ilivo kwa sasa.
 
Mkuu mimi sio mwanasheria ila ninasoma sana vitabu mbalimbali vikiwemo vya sheria. Kuhusu chama cha TLS kusaidia serikali nadhani wewe mwenyewe ni shahidi kumekua na ujinga mwingi sana unafanyika wakati wa vetting ya yupi anafaa kuwekwa kwenye maamuzi na yupi hafai. Ukileta hoja za kuisaidia nchi unaonekana mpinzani na wapinzani hawana nafasi katika hii nchi.
 
dah asee inasikitisha mno, huu mfumo wa utawala umeoza.

It’s better tusisitize viongozi waingie kwa mikataba katika ofisi zao akishindwa kutimiza mahitaji ya mkataba afutwe na alipe kila gharama aliyopewa la si hivyo atumikie kifungo maana uchaguzi tu hauwezi kuondoa huu uozo jamani.

Me inaniuma sana taifa halina taswira tena ni kama mgodi wa marehemu kila mtu anajichotea tu atavyo.

Tuwaajiri hawa watu kwa mikataba em fikirieni hii hoja yangu please jamani.
 
Hoja yako ni nzuri pia nimeona uzi wa mwenzetu mmoja kuhusu serikali kutoa ajira za mikataba kwa miaka 10. Ni jambo zuri nadhani wenye mamlaka watapita na kuchukua yaliyobora kwa ustawi wa taifa letu
 
Hoja yako ni nzuri pia nimeona uzi wa mwenzetu mmoja kuhusu serikali kutoa ajira za mikataba kwa miaka 10. Ni jambo zuri nadhani wenye mamlaka watapita na kuchukua yaliyobora kwa ustawi wa taifa letu
Kaka kwenye ule uzi nimeongea mno nimebishana na watu mno, hawajui tu vile najiskia niona taswira mbovu hivi ya taifa letu, natamani kuona mabadiliko na maendeleo sana kaka na inawezekana tukiamua kwani lazma kumuumiza mwananchi ili kuishi vizuri viongozi!?

Kwani mishahara si wanapata lakini kwanini watufanyie ukatili hivi!?
 
Waziri wa Fedha wa sasa Mwigulu Nchemba, aliwahi kusema HATUTAGONGEWA MILANGO YETU KULIPA HILI DENI wasi wasi wetu ni nini?

Hatupaswi kujadili deni la TAIFA, analipa Yeye na Rais.Samia.
 
Waziri wa Fedha wa sasa Mwigulu Nchemba, aliwahi kusema HATUTAGONGEWA MILANGO YETU KULIPA HILI DENI wasi wasi wetu ni nini?

Hatupaswi kujadili deni la TAIFA, analipa Yeye na Rais.Samia.
Tuliingizwa cha wahuni trust me.. Maana cha wahuni kichambio gunzi
 
Ni nani yuko tayari kubanduka kwenye mkondo wa ulaji?
 
hata tukibadili jina DANJANIA kuwa DANGANYIKA tabu iko pale pale.lazima tutalipa tu DENI LA TAIFA.
 
mi napendekeza iitwe nchi ya Kilimanjaro,
tuachane na majina Tanganyika au Tanzania
herufi za mwanzo za haya majina ni vitu vinavyologwa sana na kupigwa sana au kuibiwa sana
 
Sizani kama mikataba iliovunjwa ilikua inakasoro ya kisheria kwa pande zote.
Tatizo ni pale wanasiasa wanapo ingilia na kutumia ubabe kuivunja au kubadili.
 
Kama huna ujasiri wa kuwa kama Ibrahim Traore ni heri uufyate tu.

Kondoo uutowe wapi ujasiri wa Mujahid?
 


Tatizo ni viongozi wa chama chetu tawala wana sign mikataba mibaya kwa kuhogwa halafu ukija uongozi mpya wanavunja mikataba ili wahogwe wenyewe na sio waliopita mwekezaji akataa kuhonga mara mbili. Baada ya hapo wanafuta mkataba bila kufuata sheria kwa “manufaa ya umma” sasa ni manufaa gani kama tunalipa mabilioni! Hii ndiyo ramani nzima

Kwahiyo mikataba yenyewe unakuta ilikuwa mibaya lakini wameshahongwa sana. Chenge ndiye alikuwa mwanasheria msomi na mla rushwa mkubwa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…