Suluhisho la vita ya Mashariki ya kati ni kwa Wapalestina kutulia au kuhama kabisa pale Gaza

Israel wana haki, na waarabu ni wanafiki saizi wanaopata tabu ni wagaza, Ayatollah yupo Iran kanyanyua miguu juu, palestina ishafutika hata kwenye ramani haipo.

Waamue hivo vipande viwili vya gaza na west bank waunganishe ndani ya Israel wote wawe raia wa Israel tu
 
Asante sana kwa kunijibu kwa hekima na kujenga hoja muhimu.

Mimi nimesema ili amani iwepo pasipo kutaka kuchimba nani mwenye haki na nani mbaya. Choko choko yoyote ya kivita inayoanzishwa na wapelestina inapelekea kufa kwa waisrael wachache zaidi lakini inaishia kufa kwa wapalestina wengi wengi, Israel kuchukua eneo kubwa zaidi, miji mingi ya wapalestina kukaliwa kimabavu na mateso ya kimaisha kuzidishwa maradufu.

Sote tunajua kwa sasa Israel
1. Ametawala eneo kubwa.
2. Ana nguvu kubwa ya kijeshi.
3. Amedhamiria kuangamiza kila kimelea wa Hamas
4. Hana tena huruma wala simile dhidi ya mpalestina yoyote anasimama mbele yake kupambana naye.
5. Amepata sababu ya kutaka kulifuta kabisa taifa la Palestina kwa mtutu wa bunduki pale Gaza.

Sasa katika mazingira hayo, nini suluhisho la amani pale Gaza?
Kuendelea kulaani tu?
Wapalestina kuendelea kukaza shingo?

Dawa ni wapalestina wakae kwa utulivu pale Gaza (wakose uhuru lakini amani waipate) ama wahame kabisa Gaza (wakose makazi yao ya asili lakini maisha yao yaendelee popote).
 
1980s wapalestina waliwahi fukuzwa Jordan kwa kuunda nchi ndani ya nchi na king Hussein ndio wakaenda Lebanon nako huko msala tu pia wakafukuzwa kwenda Tunisia waarabu wamewachoka aise
 
Vita vikisitishwa misaada itaanza kuingia pande zote mbili !
Mabilioni ya dollar yatamiminwa huko kwa wakubwa wa pande zote mbili kwa ajili ya wananchi wao walioathirika na hiyo vita !!
Pesa nyingi kama kawaida zitaishia kwenye mifuko ya wajanja wakubwa wa pande zote mbili !!
Kufa kufaana lakini pamoja na yote hayo Two states solution ndio mpango mzima !!
Raia wema wa pande zote mbili hawaitaki hiyo vita maana inawaumiza sana! Tusijidanganye kwamba wanaoumia ni wapalestina pekee !
Chukulia mfano hapa Bongo wanapozuka Panyarodi tu shughuli inavyokua pevu mitaani !
Binadamu yeyote yule akiishi kwenye Nchi ambayo usalama wake ni mdogo huwa ni mateso sana na hakuna anayefurahia maisha ya kukimbia kimbia au ya kujificha kwenye mahandaki kila ving’ora vinapolia !!
 
Palestina haikaliwi kwa ubavu

hata macho hayaoni.
katika nchi ambayo mipaka yake imezungumzwa wazi wazi kwenye vitabu vya dini na kihistoria ni ISRAEL
Acha uongo mipaka ya Israel kwenye Bible ipo huko Iraq kabisa mto Euphrates na Tigris Kama mnafuata Bible si mfuate ramani ya Bible why mnakua na unafiki.
Israel nchi ile ni ya JEWS
Acha uongo hao wayahudi walikuta watu wanaishi sio kwamba walikuta ardhi ipo wazi, na kingine ardhi alipewa Abraham ambaye ni baba wa mataifa mengi sio Israel pekee. Why mnajimilikisha?
Hao hao UN wanaunga mkono ushoga je ni sahihi kisa UN ndio kasema? Hao UN walisema Iraq ana silaha za nyuklia which haikuwa kweli je anaaminika vipi kuwa wakati wote yupo sahihi?
 
Sahihi kabisa
 
wapalestina waliwahi fukuzwa Jordan kwa kuunda nchi ndani ya nchi na king Hussein ndio wakaenda Lebanon nako huko msala tu pia wakafukuzwa kwenda Tunisia waarabu wamewachoka aise
Vipi wayahudi kuna nchi gani waliwahi kuishi bila kufukuzwa? Walichinjwa kuanzia Moscow mpaka Paris, na fungakazi ikawa Germany na Poland maana walikua hawafanyi kazi zaidi ya biashara ya kukopesha na kuchukua riba kubwa
 
We kweli hamnazo.
Tukija kutawala Zanzibar na kuwakaba koo, wewe utaondoka tu kwa vile umezidiwa?
 
Acha uzito wa kufikiri, Golan heights, Sinai na maeneo ya Jordan unajua chanzo cha Israel kukalia maeneo hayo?

Maeneo ya Jordan na Sinai yalirudishwa je unajua chanzo na sababu za kuyaachia maeneo hayo?

Toa mahaba yako hapo na ujinga mnaojazana huko madrasa ok, kama hujui unauliza kwa ustarabu braza then unaeleweshwa ok
 

Sahihisho hakuna taifa la palestina,bali kuna wapalestina. Sawa sawa na kusema kuna taifa la zanzibar huta lipata duniani ila kuna wazanzibar ndani ya Taifa la tanzania.
 
Vipi wayahudi kuna nchi gani waliwahi kuishi bila kufukuzwa? Walichinjwa kuanzia Moscow mpaka Paris, na fungakazi ikawa Germany na Poland maana walikua hawafanyi kazi zaidi ya biashara ya kukopesha na kuchukua riba kubwa
Tatizo lako moja tu ndugu wewe ni mzito kufikiri, huko hakukuwa Uyahudini ok, kulikuwa ni ugenini, Uyahudini ndio pale Israel na sasa wamesimama kwao so wapalestina watulie
 

Mkuu umesahau hao wapalestina ndio waliokataa ile mipaka iliyowekwa na UN mwaka 1947,wakiungana n waarabu kukataa kabisa uwepo wa wayahudi hapo middle east,
 
Nimekusoma na kukuelewa.
Nataka kukuuliza haya maswali.
1. Hizi unadhani katika mazingira haya, wapalestina wanaweza kushinda hii vita?

2. Toka wapalestina waanze chokochoko za kupambana na Israel mpaka sasa, wapalestina wamefanikiwa kwa lipi katika kurudisha ardhi yao, kuishi kwa uhuru na kuepusha maafa kwa raia wa kipalestina?

3. Nini kitaendelea kwa wapalestina ikiwa vita hii itaendelea kwa muda mrefu zaidi?

4. Hivi unadhani ipo siku Israel kwa hiari yake tu au kushinikizwa kwa maneno ataamua kuandoka na kuyaacha hayo maeneo ya Gaza kwa wapalestina?

5. Hivi unaamini hilo eneo lina thamani kubwa kimaisha (kuishi kwa raha, furaha, amani, uhuru na mafanikio ya kiuchumi) kwa wapelestina kuliko sehemu zingine duniani?
 

Haya yote usingeyaandika kama
Hamas wasinge fanya ugaidi,sasa israel akirudisha mapigo manaanza kujifanya wachambuzi mara iran anamakombora mara sijui gaza ina gasi asilia,mlikua wapi kabla ya hamasi kufanya ugaidi kuleta huu uchambuzi wa kifala.

Kwa taarifa yako usa na washirika wakiamua kweli kumtandika iran hata hao urusi na china hawatamuunga mkono,mabepari huwa na lengo moja tu.
 
1980s wapalestina waliwahi fukuzwa Jordan kwa kuunda nchi ndani ya nchi na king Hussein ndio wakaenda Lebanon nako huko msala tu pia wakafukuzwa kwenda Tunisia waarabu wamewachoka aise
Huko ni kwa waarabu wenzao na wanafanya fujo hadi wanafukuzwa sembuse huku kwa weusi ambako sisi wenye nchi wanatuona Kama manyani.
Hao wabakie huko huko nadhani kuna laana fulani inawazunguka.

Ni watu wa vita kila kukicha, Kama sio ya Kisiasa basi ni ya Kidini.
Unawakaribisha siku mbili tatu wanaanza kumpigania Mungu wao.
 
Ila Allah kweli kama yupo angeshawakomboa wapalestina zamani. Anavyoabudiwa kwa nidhamu, mashindano na kutajwatajwa kila wakati kwa ajili ya wapalestina yani angeshaifutilia mbali taifa teule Israel.
🤣🤣🤣🤣
 
Unataka kulinganisha haya yanayoendelea ukanda wa Gaza na mengine duniani, tukienda hivyo tutatoka nje ya mstari.

Nimesema kadri ambavyo Palestina anacharuka na kuua waisrael ndivyo ambavyo Israel huongeza makali ya kuua, kuteka, kutesa, kujitanua na kutawala Palestina. Vice versa is true.

Sasa kama Palestina ameamua kupambana kivita na Israel, hakuna mtu kulaumu wala kumhurumia mpalestina pale anapouwawa na kuteswa, maana amechagua upande.

Suala la nani ana haki ya umiliki wa eneo na kukaa pale, toka mwanzo nimesema sio lengo la hii mada. Lengo la hii mada ni amani iwepo Gaza.
 
🤣🤣
Kimya sahivi suwasikiii kabisaa
 
🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…