Suluhisho la vita ya Mashariki ya kati ni kwa Wapalestina kutulia au kuhama kabisa pale Gaza

Yaani mtu ana justify kuteka ardhi ya mwingine kisa history ya 3000 years ago? Hivi kila mtu akidai ancestral land mfano Baganda wadai mpaka mwanza na Kagera patakalika?
Kuna watu wa ajabu sana,unakuta mtu hata history hasomi na current situation hana uelewa but yupo front kutoa recommendations kutokana na hisia zake za kiimani.
Watu ni wajinga sana.
 
Ahsante mkuu.

Wayahudi wapo wa aina tatu , wayahudi wa kutoka Ulaya yaani Diaspora Jews (ambao ndo wenye matatizo na wapalestina hadi kesho) na hawa ni wale wa Ashkenaze na jamii zao zilitokea Ulaya ya mashariki na Ulaya ya kati kama nilivyoeleza hapo juu na nchi walizotoka ni pamoja na Poland.

Wayahudi wa aina ya pili ni wale wa kihispania (mji wa Majorca) na kireno (kitongoji cha Belmonte) ambao wao wametapakaa katika maeneo ya Ulaya Magharibi katika nchi za Uholanzi (wamejaa Amsterdam), Italy , Hispania yenyewe, Ureno, Uingereza, Ujerumani (mji wa Hamburg wamejaa pale) na pia wapo Canada na Marekani.

Pia mfano mwingine wa hawa wayahudi wapo pale Uingereza katika vitongoji kama Stamford Hill na Golders Green na wana shule zao kabisa ambazo ni watoto wao tu husoma humo.

Haya makundi mawili yana uhusiano mkubwa na yalianza kukutana ili kuzoeana ili kuimarisha jadi na tamaduni zao kutokana na kwamba waote watokea barani Ulaya.

Kundi la tatu na la mwisho ni wayahudi weusi ambao watokea mashariki y akati na Afrika Kaskazini na waitwa Mizrahimu hawa wameanzia kutoka Ethiopia hadi Morocco wapo kule. Pia kwenye kundi hili wamo wayahudi wa kutoka Irak, Libya, Algeria, Yemen, Iran, Uturuki na Tunisia.

Kama nilivyosema hapo juu ni hawa wayahudi wa kutoka barani Uklaya (Diaspora Jews) walipoanza kujaa katika eneo ambalo lilikuwa likitawaliwa na Uingereza baada ya kumpokonya Ottoman kutoka kwa mfalme Suleiman ndipo zogo lilipoanza.

Mwaka 1916 Mwingereza akaingia mkataba wa siri "Triple Entente" na Mfaransa ili achukue sehemu kusini ya Himaya ya Ottoman ambayo ilijumuisha sehemu ya kusini ya Israeli ya leo yenye mji wa Beersheba na Ashdod na vitongoji kama Ashkelon. Sehemu zingine ambazo zilikuja kuwa chini ya Uingereza ni Palestina, Jordan na kusini mwa Iraq.

Tukirudi nyuma kuna suali kwamba je katika hii sehemu hawakuwepo wayahudi?

Jibu ni kwamba wayahudi walikuwepo kabla ya kuanzishwa kwa taifa la Israeli mwaka 1948 waloitwa wayashuvi na walikuwa ni idadi ndogo sana ambayo haikuwatisha wapalestina. Hawa ni wahamiaji wa kiyahudi walotokea Himaya ya Urusi katika mji wa Kharkiv wa nchi ya Ukraine ya leo ambao walihamia mahala hapo mwaka 1882 na kuanzisha makazi na mashamba na mji wao ukaitwa Rishon Lezion.

Maana ya neno Rishon Lezion ni "First to Zion" hivyo hapo utaelewa mtiririko wa mwanzo wa kuhamia mahala hapo kwa wayahudi hawa.

Ni mwishoni mwa karne ya 19 ndipo mchakato wa kuanzisha taifa la Israeli ulianza ndo yaitwa "Rise of Zionism" ambapo hawa (Diaspora Jews) wengi walianza kufikiria kujimilikisha ardhi ambayo mwanzoni walikuwa wakiikodi. Sababu kubwa ya kuanzisha taifa la Israeli ni kwamba hadi kufikia mwaka 1948 wayahudi hawa walikuwa tayari wamefikia idadi ya zaidi ya 600,000.

Ndo waingereza kwa hila wakakimbia kesi huku wakiacha mgogoro ulokuwepo baina ya wapalestina na hawa wayahudi wahamiaji na mwaka 1948 taifa la Israeli likatangazwa rasmi. Jerusalem ni mji wa wapalestina na ambao israeli kwanza waliteka Jerusalem ya magharibi baada ya vita vya mwaka 1948 na waarabu na baadae baada ya vita ya 1967 wakateka sehemu ya Jerusalem ya mashariki ukiwemo mji wa kale na kuchukua mazima hadi leo.

Suluhisho la msingi hapa ni kurudi mipaka ya mwaka 1948 ambapo wapalestina na jerusalem yao watakuwa taifa kamili na Israeli na Tel Aviv watakuwa na taifa lao.

Bila hivyo hapo ni matumizi ya sababu zingine lakini nyuma ya pazia ni mipango ya Israeli kuendelea kumega zaidi ardhi ya wapalestina kwa kutumia nguvu. Mipango la Israeli kwa sasa ni ukanda wa magharibi.

Kuhusu Wayahudi kupewa Uganda kama ndo makazi yao lilikua ni wazo la katibu wa makoloni bwana Chamberlain ambae alitaka sehemu ya ilokua koloni la Uingereza la Afrika Mashariki (British East Afrika) wapewe wayahudi (kundi la wazayuni ) hao walokimbia Urusi na ilikuwa ni mwaka 1903 na alitaka wapewe mita za mraba 5,000 ambalo ni eneo zilipo Kenya na Uganda leo.

Iliposhindikana hiyo (walikataa) ndo wakapewa pale Palestina ilokuwa chini ya uangalizi wa Uingereza.
 
Ila Allah kweli kama yupo angeshawakomboa wapalestina zamani. Anavyoabudiwa kwa nidhamu, mashindano na kutajwatajwa kila wakati kwa ajili ya wapalestina yani angeshaifutilia mbali taifa teule Israel.
Unamweka Allah kwenye ligi na Mungu wa Israel? aiseee.......
 
Inavyoonekana binadamu hatuwezi kuacha kupigana, hatuna common enemy mwenye akili za kiwango chetu ama kutuzidi wa kutuunganisha ili kupigana naye.

Siku tukiwa na tishio la kiumbe chenye akili kikawasili katika sayari yetu mambo mengi yatabadilika na huenda tukaacha kulipuana wenyewe kwa wenyewe nguvu zote zikaelekezwa kwengine.
 
ilokua koloni la Uingereza la Afrika Mashariki (British East Afrika) wapewe wayahudi (kundi la wazayuni ) hao walokimbia Urusi na ilikuwa ni mwaka 1903 na alitaka wapewe mita za mraba 5,000
Mkuu ina maana leo hii Kenya na Uganda wangekua wanatandikwa ili wapishe wayahudi? Duh nadhani hata ziwa Victoria wangekua wamepora!!?

Jokes aside, a very insightful comment with objective recommendations. Indeed vintage JF vibes!
 
Mkuu naona common enemy akiwa Artificial Intelligence na Robotics!! Imagine siku maroboti yakawa na accumulated algorithms za kufanya maamuzi at free will!! Maybe then wanadamu tuta unite
 
Reactions: Tsh
🤣🤣🤣
Acha upagani wewe, njoo tukubatize! what about christians? ambao asili ya dini yao inatoka huko, na Bwana yesu mwenyewe ametokea huko? Kwa taarifa yako JEWS ni waumini wa judeism na moja ya tatizo lao ni kutaka ISRAEL iwe jewish state!
 
Mkuu naona common enemy akiwa Artificial Intelligence na Robotics!! Imagine siku maroboti yakawa na accumulated algorithms za kufanya maamuzi at free will!! Maybe then wanadamu tuta unite
Kuna movie ya zamani kidogo niliitazama ya anold inaitwa terminator. Ai ilisumbua sana.
 
Vita ile ni michongo ya koo na falme... Imekuwa hivyo kwa na miaka karne na karne Nawashangaa waofuata upepo mara Israel mara Palestine bila hata kujua chanzo cha vita ni nini?!
Alafu kama kweli hizo dini zao pendwa ni kwa ajili ya MUNGU, upendo, amani, msamaha inakuwaje waumini wa dini wanachukua upande wa kuwaumiza wengine??
 
Walikuta wanaishi Palestinians...... wakawapora makazi yao.
Kwako unawezaje kupora? Biblia kitabu Cha Mwanzo 15:18 Mungu aliwapa Waisraeli. Quran 5 :21 Allah aliwapa Waisraeli nchi hiyo. Warumi walitawanya Waisraeli mwaka 135 AD na akawarudisha 1948. Mtu aliyerudi kwake anakuwaje mvamizi? Wapalestina wakae kwa kutulia vinginevyo kipondo kitaendelea.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kuna watu wa ajabu sana,unakuta mtu hata history hasomi na current situation hana uelewa but yupo front kutoa recommendations kutokana na hisia zake za kiimani.
Watu ni wajinga sana.
Kama Imani ni ujinga, basi subiri yatimie aliyoyataniri Nabii Amos 9:15 kwamba Israel atawarudisha Kutoka alikowatawanya, na wakirudi hakuna atakayewatoa. Wewe kama unaona ni ujinga, subiri uone huo ujinga.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mtazunguka na maelezo mengine lakini kisa Cha ugomvi wa Wapalestina na Waisraeli kinaelezwa hapa: Biblia kitabu Cha Kutoka 25:22-23 Watoto wawili wanapigana tumboni, hayo ni mataifa mawili, watafarakana, mmoja atakuwa hodari, mmoja atamtumikia mwingine. Ugomvi huo haitaisha, ni WA toka miaka 1600 BC.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Binafsi jambo lolote la haki likiishahusisha umwagaji damu basi mimi huliona kama limekosa uhalali kuwepo.


Palestina wanakufa kwa kupigania haki,ambayo kimsingi sio muhimu kuliko maisha yao na vizazi vyao,kifupi wanatumika bila kujua.
 
Kwa hizi wiki mbili ni wazi kuwa ''ubishi'' na mashambulizi ya kuvizia yatawaathiri sana Wapalestina.

Kweli wana haki na eneo, lakini vifo na mauaji haya yanawapa faida gani?

Ni kweli Israel anafanya unyama kwa mwamvuli wa kujilinda na kulipiza kisasi.

Kwa mtazamo tu Palestina huwa anaachwa mwenyewe apambane na Israel, sio ulimwengu wa Kiarabu unaoishia kutoa nyaraka wala sio Urusi na China wanaoishia kwenye kutoa mapendekezo tena wakiwa UN - pale New York.

Kama kweli dunia ingesimama pamoja na Palestina kama ambavyo tunasimama nao kwenye slogan na hashtag za ''I stand with Palestine'' basi leo hali ya Gaza isingekuwa ya kusikitisha kwa kiwango hiki.
 
Utashanga hadi Pro-putin wanaoshabikia uvamizi wa Urusi huko Ukraine wanapinga hili!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…