Asante mkuu, 'Richard', kwa kuchukua muda wako kutoa somo kama unavyolielewa wewe, nami kwa mengi ninakubaliana nawe.
Haya ni matatizo yaliyosababishwa, na yanaendelea kuchochewa na haya mataifa ya nje kwa manufaa ya mataifa hayo.
Kwa maelezo yako, ambayo ni kweli, kwamba wayahudi walikuwa wametapakaa sehemu mbalimbali huko nchi za Ulaya, nisilojua vizuri ni kama hapakuwepo na myahudi yeyote hapo ilipo Israel leo hadi walipomegewa kipande na waingereza. Kama ni hivyo, kutakuwa na swali pia, kwa nini waingereza waliona sehemu hiyo ndilo eneo walilotakiwa kuwepo wayahudi. Kuna taarifa nyingine husemwa kwamba moja ya eneo lililofikiriwa kupewa wayahudi ni Uganda (sina hakika na hili).
Je, inawezekana kwamba eneo lile wayahudi waliwahi kuishi hapo na kwa sababu mbalimbali za matukio, wakajikuta baadae wamesambaa kwingine duniani. Habari za maandiko ya vitabuni, ya kidini, historia hiyo ni kweli? Tunajua uwepo wa miji kama Jerusalem na maeneo mengine, ambayo ni wazi yanaonyesha uwepo wa watu hao katika maeneo hayo nyakati hizo za zamani.
Binafsi naamini kwamba, si Hamas, Iran, au hata Israel yenyewe watakaodai na kuwezesha kuondoka kwa mmoja kati ya waPalestina na waIsrael. Hakuna tena kwenye dunia ya leo kulisambaratisha moja kwa moja taifa moja dhidi ya jingine. hawa wakubwa wa dunia leo wanahangaika na maslahi yao, lakini kama ilivyokuwa kwa Himaya nyinginezo zilizopita, hawa wa leo na wao siku zao zinahesabika tu.
Kwa hiyo, la msingi, ni kutafuta njia ya usuluhishi, ili kila taifa liishi katika mipaka yake, na kuheshimu mipaka ya wengine.
Iran hata awe na uwezo kiasi gani, hawezi tena kumwondoa Israel hapo alipo. Kujiapiza kulifuta taifa hilo, ni kujidanganya; kama watakavyojidanganya Israel, kwa kudhani wanaweza kuishi kwa amani kwa kuwakandamiza waPalestina. Haiwezekani.
Ahsante mkuu.
Wayahudi wapo wa aina tatu , wayahudi wa kutoka Ulaya yaani Diaspora Jews (ambao ndo wenye matatizo na wapalestina hadi kesho) na hawa ni wale wa Ashkenaze na jamii zao zilitokea Ulaya ya mashariki na Ulaya ya kati kama nilivyoeleza hapo juu na nchi walizotoka ni pamoja na Poland.
Wayahudi wa aina ya pili ni wale wa kihispania (mji wa Majorca) na kireno (kitongoji cha Belmonte) ambao wao wametapakaa katika maeneo ya Ulaya Magharibi katika nchi za Uholanzi (wamejaa Amsterdam), Italy , Hispania yenyewe, Ureno, Uingereza, Ujerumani (mji wa Hamburg wamejaa pale) na pia wapo Canada na Marekani.
Pia mfano mwingine wa hawa wayahudi wapo pale Uingereza katika vitongoji kama Stamford Hill na Golders Green na wana shule zao kabisa ambazo ni watoto wao tu husoma humo.
Haya makundi mawili yana uhusiano mkubwa na yalianza kukutana ili kuzoeana ili kuimarisha jadi na tamaduni zao kutokana na kwamba waote watokea barani Ulaya.
Kundi la tatu na la mwisho ni wayahudi weusi ambao watokea mashariki y akati na Afrika Kaskazini na waitwa Mizrahimu hawa wameanzia kutoka Ethiopia hadi Morocco wapo kule. Pia kwenye kundi hili wamo wayahudi wa kutoka Irak, Libya, Algeria, Yemen, Iran, Uturuki na Tunisia.
Kama nilivyosema hapo juu ni hawa wayahudi wa kutoka barani Uklaya (Diaspora Jews) walipoanza kujaa katika eneo ambalo lilikuwa likitawaliwa na Uingereza baada ya kumpokonya Ottoman kutoka kwa mfalme Suleiman ndipo zogo lilipoanza.
Mwaka 1916 Mwingereza akaingia mkataba wa siri "Triple Entente" na Mfaransa ili achukue sehemu kusini ya Himaya ya Ottoman ambayo ilijumuisha sehemu ya kusini ya Israeli ya leo yenye mji wa Beersheba na Ashdod na vitongoji kama Ashkelon. Sehemu zingine ambazo zilikuja kuwa chini ya Uingereza ni Palestina, Jordan na kusini mwa Iraq.
Tukirudi nyuma kuna suali kwamba je katika hii sehemu hawakuwepo wayahudi?
Jibu ni kwamba wayahudi walikuwepo kabla ya kuanzishwa kwa taifa la Israeli mwaka 1948 waloitwa wayashuvi na walikuwa ni idadi ndogo sana ambayo haikuwatisha wapalestina. Hawa ni wahamiaji wa kiyahudi walotokea Himaya ya Urusi katika mji wa Kharkiv wa nchi ya Ukraine ya leo ambao walihamia mahala hapo mwaka 1882 na kuanzisha makazi na mashamba na mji wao ukaitwa Rishon Lezion.
Maana ya neno Rishon Lezion ni "First to Zion" hivyo hapo utaelewa mtiririko wa mwanzo wa kuhamia mahala hapo kwa wayahudi hawa.
Ni mwishoni mwa karne ya 19 ndipo mchakato wa kuanzisha taifa la Israeli ulianza ndo yaitwa "Rise of Zionism" ambapo hawa (Diaspora Jews) wengi walianza kufikiria kujimilikisha ardhi ambayo mwanzoni walikuwa wakiikodi. Sababu kubwa ya kuanzisha taifa la Israeli ni kwamba hadi kufikia mwaka 1948 wayahudi hawa walikuwa tayari wamefikia idadi ya zaidi ya 600,000.
Ndo waingereza kwa hila wakakimbia kesi huku wakiacha mgogoro ulokuwepo baina ya wapalestina na hawa wayahudi wahamiaji na mwaka 1948 taifa la Israeli likatangazwa rasmi. Jerusalem ni mji wa wapalestina na ambao israeli kwanza waliteka Jerusalem ya magharibi baada ya vita vya mwaka 1948 na waarabu na baadae baada ya vita ya 1967 wakateka sehemu ya Jerusalem ya mashariki ukiwemo mji wa kale na kuchukua mazima hadi leo.
Suluhisho la msingi hapa ni kurudi mipaka ya mwaka 1948 ambapo wapalestina na jerusalem yao watakuwa taifa kamili na Israeli na Tel Aviv watakuwa na taifa lao.
Bila hivyo hapo ni matumizi ya sababu zingine lakini nyuma ya pazia ni mipango ya Israeli kuendelea kumega zaidi ardhi ya wapalestina kwa kutumia nguvu. Mipango la Israeli kwa sasa ni ukanda wa magharibi.
Kuhusu Wayahudi kupewa Uganda kama ndo makazi yao lilikua ni wazo la katibu wa makoloni bwana Chamberlain ambae alitaka sehemu ya ilokua koloni la Uingereza la Afrika Mashariki (British East Afrika) wapewe wayahudi (kundi la wazayuni ) hao walokimbia Urusi na ilikuwa ni mwaka 1903 na alitaka wapewe mita za mraba 5,000 ambalo ni eneo zilipo Kenya na Uganda leo.
Iliposhindikana hiyo (walikataa) ndo wakapewa pale Palestina ilokuwa chini ya uangalizi wa Uingereza.