Suluhisho la vita ya Mashariki ya kati ni kwa Wapalestina kutulia au kuhama kabisa pale Gaza

Suluhisho la vita ya Mashariki ya kati ni kwa Wapalestina kutulia au kuhama kabisa pale Gaza

Suluhu kuwe na nchi mbililakini siyo kila siku taifa teule linachukua aridhi ya watu alafu achiwe abadani hiyo haiwezekani.
Hakuna nchi 2, ndo kwanza twataka waondoa hao magaidi, kwa sasa ni kuhakikisha twaharibu majengo yote
 
Aliwakuta wapo, Sasa watulie mwenye mji karudi.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Sio sahivi naongelea hao kina Joshua na wayahudi walikuta Canaan ina watu tayari na ilikua na makabila zaidi ya 13!! Sema waliwaua hao wote ndio wakaweka nchi. Kwahiyo si kweli kwamba mwanzoni nchi ilikua yao!! Ila WALIIPORA kwa WENYEJI
 
Hilo eneo la Gaza hapo mashariki ya kati ni dogo sana, kavu mnoo, halina rasilimali zozote muhimu za kiuchumi ukiachilia hizi blah blah za kiimani ambazo zinatumika na pande zote kinafiki tu na kimchongo ili kujitengenezea uhalali wa kumiliki hayo maeneo kwa sababu ya umuhimu wa kihistoria.

Sasa kwanini watu wakae kwa wagombana?
Kwani dunia haina sehemu zingine za kuishi?
Kuna raha gani kuishi katika hali hiyo?
kwa nini nyinyi munakomaa na kuishi ngorongoro wakati pia ni eneo kavu na halina uzalishaji?

Munavyopenda kuzungumzia ya wenzenu wakati yenu ndiyo ya aina ile ile lakini laiti mungepewa nafasi basi mungefanya hivyo hivyo.
 
Ahsante mkuu.

Wayahudi wapo wa aina tatu , wayahudi wa kutoka Ulaya yaani Diaspora Jews (ambao ndo wenye matatizo na wapalestina hadi kesho) na hawa ni wale wa Ashkenaze na jamii zao zilitokea Ulaya ya mashariki na Ulaya ya kati kama nilivyoeleza hapio juu na nchi walizotoka ni pamoja na Poland.

Wayahudi wa aina ya pili ni wale wa kihispania (mji wa Majorca) na kireno (kitongoji cha Belmonte) ambao wao wametapakaa katika maeneo ya Ulaya Magharibi katika nchi za Uholanzi (wamejaa Amsterdam), Italy , Hispania yenyewe, Ureno, Uingereza, Ujerumani (mji wa Hamburg wamejaa pale) na pia wapo Canada na Marekani.

Pia mfano mwingine wa hawa wayahudi wapo pale Uingereza katika vitongoji kama Stamford Hill na Golders Green na wana shule zao kabisa ambaoz ni watoto wao tu husoma humo.

Haya makundi mawili yana uhusiano mkubwa na yalianza kukutana ili kuzoeana ili kuimarisha jadi na tamaduni zao kutokana na kwamba waote watokea barani Ulaya.

Kundi la tatu na la mwisho ni wayahudi weusi ambao watokea mashariki y akati na Afrika Kaskazini na waitwa Mizrahimu hawa wameanzia kutoka Ethiopia hadi Morocco wapo kule. Pia kwenye kundi hili wamo wayahudi wa kutoka Irak, Libya, Algeria, Yemen, Iran, Uturuki na Tunisia.

Kama nilivyosema hapo juu ni hawa wayahudi wa kutoka barani Uklaya (Diaspora Jews) walipoanza kujaa katika eneo ambalo lilikuwa likitawaliwa na Uingereza baada ya kumpokonya Ottoman kutoka kwa mfalme Suleiman.

Mwaka 1916 Mwingereza akaingia mkataba wa siri "Triple Entente" na Mfaransa ili achukue sehemu kusini ya Himaya ya Ottoman ambayo ilijumuisha sehemu ya kusini ya Israeli ya leo yenye mji wa Beersheba na Ashdod na vitongoji kama Ashkelon. Sehemu zingine ambazo zilikuja kuwa chini ya Uingereza ni Palestina, Jordan na kusini mwa Iraq.

Tukirudi nyuma kuna suali kwamba je katika hiisehemu hawakuwepo wayahudi?

Jibu ni kwamba wayahudi walikuwepo kabla ya kuanzishwa kwa taifa la Israeli mwaka 1948 waloitwa wayashuvi na walikuwa ni idadi ndogo sana ambayo haikuwatisha wapalestina. Hawa ni wahamiaji wa kiyahudi walotokea Himaya ya Urusi katika mji wa Kharkiv wa nchi ya Ukraine ya leo ambao walihamia mahala hapo mwaka 1882 na kuanzisha makazi na mashamba na mji wao ukaitwa Rishon Lezion.

Maana ya neno Rishon Lezion ni "First to Zion" hivyo hapo utaelewa mtiririko wa mwanzo wa kuhamia mahala hapo kwa wayahudi hawa.

Ni mwishoni mwa karne ya 19 ndipo mchakato wa kuanzisha taifa la Isreali ulianza ndo yaitwa "Rise of Zionism" ambapo hawa (Diaspora Jews) wengi walianza kufikiria kujimilikisha ardhi ambayo mwanzoni walikuwa wakiikodi. Sababu kubwa ya kuanzisha taifa la Israeli ni kwamba hadi kufikia mwaka 1948 wayahudi hawa walikuwa tayari wamefikia idadi ya zaidi ya 600,000.

Ndo waingereza kwa hila wakakimbia kesi huku wakiacha mgogoro ulokuwepo baina ya wapalestina na hawa wayahudi wahamiaji na mwaka 1948 taifa la Israeli likatangazwa rasmi. Jerusalem ni mji wa wapalestina na ambao israeli kwanza waliteka Jerusalem ya magharibi baada ya vita vya mwaka 1948 na waarabu na baadae baada ya vita ya 1967 wakateka sehemu ya Jerusalem ya mashariki ukiwemo mji wa kale na kuchukua mazima hadi leo.

Suluhisho la msingi hapa ni kurudi mipaka ya mwaka 1948 ambapo wapalestina na jerusalem yao watakuwa taifa kamili na Israeli na Tel Aviv watakuwa na taifa lao.

Bila hivyo hapo ni matumizi ya sababu zingine lakini nyuma ya pazia ni mipango ya Israeli kuendelea kumega zaidi ardhi ya wapalestina kwa kutumia nguvu. Mipango la Israeli kwa sasa ni ukanda wa magharibi.

Kuhusu Wayahudi kupewa Uganda kama ndo makazi yao lilikua ni wazo la katibu wa makoloni bwana Chamberlain ambae alitaka sehemu ya ilokua koloni la Uingereza la Afrika Mashariki (British East Afrika) wapewe wayahudi (kundi la wazayuni ) hao walokimbia Urusi na ilikuwa ni mwaka 1903 na alitaka wapewe mita za mraba 5,000 ambalo ni eneo zilipo Kenya na Uganda leo.

Iliposhindikana hiyo (walikataa) ndo wakapewa pale Palestina ilokuwa chini ya uangalizi wa Uingereza.
Asante sana mkuu Richard.

Uchangiaji wa mada wa aina hii umekuwa wa nadra sana siku hizi humu JF.

Umenipa funzo ambalo nilikuwa sijawahi kulipata.

Sasa kama kuna mtu mwingine, mwenye mtizamo au usahihi wa taarifa zaidi ya huu ulioutoa hapa wewe; hapo sisi wanafunzi katika eneo hili tungefaidika na mjadala wa aina hiyo.

Lakini pia, pamoja na somo hili ulilotoa hapa, nadhani bado kuna sehemu ya historia ambayo pengine inawaweka wayahudi katika eneo hilo, ambayo ni ya mbali zaidi ya hapo ulipoishia wewe. Hii jerusalem, kwa mfano, kuwa mji wa wapalestina, tokea lini? Enzi za akina Pilato wanaosemwa kwenye vitabu vya kidini? Wayahudi walikuwepo hapo enzi zile; halafu baadae, kwa njia moja au nyingine wakasambaratishwa na kuacha eneo hilo kuwa chini ya waPalestina?

Nirudie tena niliyokwisha yaandika humu mara kadhaa. Suluhisho la kudumu katika eneo hilo hautapatikana kwa kutegemea matumizi ya maangamizi ya silaha, na kukandamiza binaadam wengine.
 
Ubishi, ukaidi na ujeuri wa Wapalestina kutaka kupambana na Israel itapelekea maafa na mateso zaidi kwa watu wasiokuwa na hatia. Ama kwa kupenda au kutokupenda, suluhisho rahisi na lenye kuleta amani mashariki ya kati ni wapalestina kuwa watulivu ili waendelee kukaa pale kwa amani au kuhama kabisa maeneo yale ili kuepusha shari zaidi.

Hizi choko choko za vikundi vya Hamas nk. ni kujilisha upepo na kuongeza mateso, hazina msaada wowote endelevu kwa wapalestina. Wapalestina wakae wakijua, hakuna nchi ya kiarabu itajiingiza kichwa kichwa kuwapigania pale, sio Iran, Lebanon, Syria, Egypt, Jordan au Saudi Arabia ambayo ina muda, nguvu, rasimali au dhamira ya dhati ya kwenda moja kwa moja kuwapigania wapalestina, kila taifa linapambana na hali yake tu.

Hilo eneo la Gaza hapo mashariki ya kati ni dogo sana, kavu mnoo, halina rasilimali zozote muhimu za kiuchumi ukiachilia hizi blah blah za kiimani ambazo zinatumika na pande zote kinafiki tu na kimchongo ili kujitengenezea uhalali wa kumiliki hayo maeneo kwa sababu ya umuhimu wa kihistoria.

Sasa kwanini watu wakae kwa wagombana?
Kwani dunia haina sehemu zingine za kuishi?
Kuna raha gani kuishi katika hali hiyo?

Unaweza kusema au kuwaza kuwa kwanini waisraeli wao wasihamishwe pale? Jibu ni moja tu, Israel kwa sehemu kubwa ndio inapamiliki pale kwa sasa (iwe kwa haki au mabavu), Israel haina muda wa kuchokoza wapalestina ili iendelee kukaa pale bali ina dhamira, muda na nguvu za kutaka kuwakandamiza zaidi na kuwatuliza vilivyo ikiwa wapalestina watataka kuendelea kubakia pale.

Kama kuna wafia dini huku duniani wanaoona ni lazima kuendelea kupigana vita pale mashariki ya kati basi waende wao pale kwa vivuli vya dini yao kupigana na sio kutumia wapalestina kama chambo.

Note:
Taifa la Palestina lina mchanganyiko wa watu wenye imani tofauti tofauti wakiwemo waislamu (97%) na wakristo (3%), wakati taifa la Israel nalo lina waumini wa kiyahudi (81%), waislamu (14%), dini za asili (3%) na wakristo (2%). Lakini kote huko kwa hayo mataifa na hao waumini ukichunguza utagundua miongoni mwao kuna wapagani na wahuni kibao, hivyo tusilazimishe hii vita kuwa ni vita ya kidini wakati ni siasa na tamaa tu.

TUMECHOKA NA VITA
HATUTAKI VITA
Wahame waende wapi?
Hao waisrael walikataliwa huko Ulaya ndio maana wakarudi hapo sasa unataka wapalestina wahame waende wapi?
Kama tu kwenye vita hii hakuna nchi inayopokea zikiwemo nchi kama Egypt, unataka wahame waende wapi?
Solution ni nchi za magharibi kusema ukweli kuwa Israel anamnyanyasa Mpalestina, warudi kwenye mipaka iliyowekwa na umoja wa mataifa ambayo Israel kaikiuka na kuchukua hadi maeneo ya Wapalestina.
 
Solution ni nchi za magharibi kusema ukweli kuwa Israel anamnyanyasa Mpalestina, warudi kwenye mipaka iliyowekwa na umoja wa mataifa ambayo Israel kaikiuka na kuchukua hadi maeneo ya Wapalestina.
That's it.

Na ikishafanyika hivyo, yeyote atakayeleta chokochoko, huyo ndiye adui wa watu hawa, wote waIsrael na WaPalestina.

Siyo Marekani na maguvu yote ya silaha, wala Iran na wengineo, kwa sababu yoyote ile.
 
Kama Imani ni ujinga, basi subiri yatimie aliyoyataniri Nabii Amos 9:15 kwamba Israel atawarudisha Kutoka alikowatawanya, na wakirudi hakuna atakayewatoa. Wewe kama unaona ni ujinga, subiri uone huo ujinga.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Naona unazidi kujipambanua kuwa mjinga zaidi ya nilivyo kuona huko mwanzo wa mada.
Aliwakuta wapo, Sasa watulie mwenye mji karudi.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Mtazunguka na maelezo mengine lakini kisa Cha ugomvi wa Wapalestina na Waisraeli kinaelezwa hapa: Biblia kitabu Cha Kutoka 25:22-23 Watoto wawili wanapigana tumboni, hayo ni mataifa mawili, watafarakana, mmoja atakuwa hodari, mmoja atamtumikia mwingine. Ugomvi huo haitaisha, ni WA toka miaka 1600 BC.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Huu sasa ni upumbavu.
 
Mwanamgambo mmoja wa Israel amenasa tunduni
Hamas have captured an Israeli special forces officer after the IDF attempted an incursion into Gaza.

Possibly a Sayeret Matkal member
 
Ubishi, ukaidi na ujeuri wa Wapalestina kutaka kupambana na Israel itapelekea maafa na mateso zaidi kwa watu wasiokuwa na hatia. Ama kwa kupenda au kutokupenda, suluhisho rahisi na lenye kuleta amani mashariki ya kati ni wapalestina kuwa watulivu ili waendelee kukaa pale kwa amani au kuhama kabisa maeneo yale ili kuepusha shari zaidi.

Hizi choko choko za vikundi vya Hamas nk. ni kujilisha upepo na kuongeza mateso, hazina msaada wowote endelevu kwa wapalestina. Wapalestina wakae wakijua, hakuna nchi ya kiarabu itajiingiza kichwa kichwa kuwapigania pale, sio Iran, Lebanon, Syria, Egypt, Jordan au Saudi Arabia ambayo ina muda, nguvu, rasimali au dhamira ya dhati ya kwenda moja kwa moja kuwapigania wapalestina, kila taifa linapambana na hali yake tu.

Hilo eneo la Gaza hapo mashariki ya kati ni dogo sana, kavu mnoo, halina rasilimali zozote muhimu za kiuchumi ukiachilia hizi blah blah za kiimani ambazo zinatumika na pande zote kinafiki tu na kimchongo ili kujitengenezea uhalali wa kumiliki hayo maeneo kwa sababu ya umuhimu wa kihistoria.

Sasa kwanini watu wakae kwa wagombana?
Kwani dunia haina sehemu zingine za kuishi?
Kuna raha gani kuishi katika hali hiyo?

Unaweza kusema au kuwaza kuwa kwanini waisraeli wao wasihamishwe pale? Jibu ni moja tu, Israel kwa sehemu kubwa ndio inapamiliki pale kwa sasa (iwe kwa haki au mabavu), Israel haina muda wa kuchokoza wapalestina ili iendelee kukaa pale bali ina dhamira, muda na nguvu za kutaka kuwakandamiza zaidi na kuwatuliza vilivyo ikiwa wapalestina watataka kuendelea kubakia pale.

Kama kuna wafia dini huku duniani wanaoona ni lazima kuendelea kupigana vita pale mashariki ya kati basi waende wao pale kwa vivuli vya dini yao kupigana na sio kutumia wapalestina kama chambo.

Note:
Taifa la Palestina lina mchanganyiko wa watu wenye imani tofauti tofauti wakiwemo waislamu (97%) na wakristo (3%), wakati taifa la Israel nalo lina waumini wa kiyahudi (81%), waislamu (14%), dini za asili (3%) na wakristo (2%). Lakini kote huko kwa hayo mataifa na hao waumini ukichunguza utagundua miongoni mwao kuna wapagani na wahuni kibao, hivyo tusilazimishe hii vita kuwa ni vita ya kidini wakati ni siasa na tamaa tu.

TUMECHOKA NA VITA
HATUTAKI VITA
Pumbavu
 
Binafsi jambo lolote la haki likiishahusisha umwagaji damu basi mimi huliona kama limekosa uhalali kuwepo.

Palestina wanakufa kwa kupigania haki,ambayo kimsingi sio muhimu kuliko maisha yao na vizazi vyao,kifupi wanatumika bila kujua.
Pole sana
 
Mwanamgambo mmoja wa Israel amenasa tunduni
Hamas have captured an Israeli special forces officer after the IDF attempted an incursion into Gaza.

Possibly a Sayeret Matkal member
Benjamin Netanyahu mwenyewe amewahi kuwa team leader wa hiyo company.
 
Watumishi wa ibrahimu na lutu walikuwa wanagombania malisho mungu akaingilia kati akaamua ugomvi wao. Kila mmoja akaoneshwa upande wa kuelekea akalishe mifugo yake huko na ugomvi ukaisha. Wakati mwingine inabidi uondoke tu uumpishe mbabe kuepusha maafa. Elekea upande mwingine kuna usalama huko
Mwenyezi Mungu hawakatazi kuwafanyia hisani na uadilifu wale ambao hawakupigana nanyi kwa ajili ya dini, wala hawakuwafukuza katika nchi zenu. Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wafanyao uadilifu. Isipokuwa Mwenyezi Mungu anawakataza kuwafanya marafiki wale wanaopigana nanyi katika dini, na wakawafukuza katika nchi zenu na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu, na wawafanyao marafiki, basi hao ndio madhalimu" (60: 8 - 9)
 
Back
Top Bottom