Sumaye: Kinana anapiga dili za meno ya Tembo

Sumaye: Kinana anapiga dili za meno ya Tembo

Lowassa na Sumaye hawana jipya la kutueleza watanzania.kama ni suala la ufisadi walikuwepo kwenye serikali hii hii ya ccm kwa kipindi chote cha Kula maisha na raha zao.leo hii wamekosa nafasi ya kuwania urais ndio wanayaona haya? Hatudanganyiki
 
Sumaye we sumaye why sasa umekosa ya kusema,ulipokuwa waziri mkuu si ndo ungemkabili?kwa sasa ni sawa na majungu tu pole

Siyo majungu, Sumaye siyo mgombea na Kinana siyo mgombea pia. Kumbuka ccm kama chama kingine ina codes of conduct zake ambazo haziruhusu taarifa zake za ndani kutoka nje. Hivyo ukitoka unapata fursa ya kusema.
Kumbuka pia kuwa mh. Kinana kama katibu mkuu wa chama tawala, ndo mwajiri mkuu wa government executives.
 
miaka 10 ya uongozi wa Kikwete na biashara haramu imeongezeka sana. Wafanya biashara hizi ndiyo vigogo wakuu wa CCM.
 
Huna sera wewe.

Kivipi Lizaboni? Kuwa tembo hawajauwawa au muuaji hajajulikana bado?
Note: hata kama wewe ni kada ifike sehemu nafsi ikusute kuhusu vifo vya tembo, waonee huruma tembo
 
Sasa huyu sumaye kama kapagawa mwanzo aliona utani bt sasahv ashajua ukawa kushinda uchaguzi ni shida so anomba yatoked ata machafuko na yy angemshughulikia alivokua waziri mkuu kam c unafiki ni nini nasura yke tu na macho unajua ni mtu wa aina gani

Machafuko yatokee ya nini wewe acha mbinu za kishamba na kizamani.watanzania wako vizuri siku hizi usifikiri ni vichwa maji kama wewe
 
Sumaye we sumaye why sasa umekosa ya kusema,ulipokuwa waziri mkuu si ndo ungemkabili?kwa sasa ni sawa na majungu tu pole

Mbona Lowassa alipokuwa CCM hamkumuita fisadi? Mfumo unawalinda mafisadi sasa hivi yupo nje ya mfumo huo, KINANA muuaji tembo wetu
 
Jana kwa mara nyingine waziri Mkuu mstafu Ndg. F. Sumaye alimlipua katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi A. Kinana na kusema katibu mkuu huyo kwa muda mrefu amekuwa akijihusisha na uuzaji wa meno ya tembo (pembe za ndovu)... "Soma gazeti hapa chini"

Ilimbukwe kuwa mwaka jana kituo cha utangazaji cha Aljazeera kilitoa data kuhusu tembo wa Tanzania kuuwawa na kuonyesha kwamba mwaka 2007 kulikuwa na jumla ya tembo 146,879 na mpaka mwaka jana 2014 tembo hao wameuwawa kwa asilimia 64% na kubaki tembo 56,000 tu...

Mytake: Hili suala la Kinana tulifikiri ni uzushi ila ukiona waziri mkuu aliyekaa madarakani kwa miaka 10 kaliweka wazi mbele ya wananchi ni wazi hakuna ubishi tena katika hilo....

Kwa taarifa yako mwenyewe unasema Waziri Mkuu huyo amesoma kwenye gazeti inamaana hajui.
 
Lowasa mbona kashindwa kujibu ufisadi wote aloufanya etiii mzee usibishane nao kaaa kimya.... mmh akae kimya ama hana la kujibu makuu nyie mnashabikia msilolijua

Wooote upi wewe kasuku?
 
mbona hakusema wakat yupo serkaln? tunataka mtu asiyebadilika badilika km Dr Slaa nyeusi iwe nyeus sasa leo list ya mafisad imeondolewa kwenye web ya chadema unategemea nn

Slaa kabadilishwa na Mushumbusi, kapewa taff na usalama wa taifa, kakutana na Mwakyembe masaa matatu kabla ya kupanda kwenye mimbari ya Serena hotel
 
Kwanini hakumshitaki wakati alikua waziri mkuu? Huyu ni ziro kweli kweli
 
1. Nawashangaa wanaowachoma moto Vibaka na kumuacha Lowassa akitanua mitaani-Freeman Aikaeli Mbowe;
2. Anayemuunga mkono Lowassa akapimwe akili haraka-Mch. Peter Msigwa
3. Nina ushahidi wa kutosha kuhusiana na Wizi na Ufisadi wa Lowassa na Rostam-John Mnyika.
4. CCM wamempatia Fisadi Lowassa fomu ya kugombea urais. Ni hatari sana-Tundu Lissu.
5. Nimesema kama UKAWA tutamsimamisha fisadi, mna haki ya kututosa-Halima mdee
6. I thought safari ya Matumaini was poorly organized, imekuwa safari ya matumizi
7.Taarifa kwa Umma: Serikali iache kumlinda Lowassa, ni mmoja wa mizizi ya ufisadi wa Richmond. Akamatwe, ahojiwe na achukuliwe hatua za kisheria- Yeriko Nyerere
8. Wakati Mwakyembe na Magufuli wakiwajibika kulitumikia taifa , kuna Mapaka shume yanatembea Makanisani na Misikitini yakisaka urais-Yeriko Nyerere
8. Ni heshima kwa Mungu kumzomea na kumtukana mtu FISADI kama Lowassa-Godbless Lema
9. Pamoja na haki ya kila mtu kugombea urais, kwa hawa walioomba kutoka CCM, I don't see talent, kwangu mimi wote ni average brain-Peter Msigwa' s tweet 09/06/2015
10. Mtu anayetaka nafasi urais, lazima awe tayari kujipima, kujitafakari, kujiridhisha kuwa anatosha, yeye mwenyewe kwanza, afanye hayo, ajipime , ajitafakari na ajiridhishe kuwa anatosha:
¡ kiafya
¡¡ kiakili
¡¡¡ kimaadili
¡v kidhamira
Lazima ujipime hayo kama unapungukiwa na mojawapo kati ya hayo, hufai, lakini la pili uwe tayari Umma kukupima katika hayo niliyoyataja, uwe tayari Umma ukupime kiafya, kiakili, kimaadili na kidhamira, siyo unajipima tu mwenyewe na unasema , mimi sawasawa, A a a a, na Umma nao ukupime- Fredrick Tluwaye Sumaye
11. CCM mkimpitisha Lowassa nahama Chama-Sumaye


12. Njaa hadi kwenye nyumba za ibada, Wachungaji wa makanisa mbalimbali ya Kikristo wakiandamana muda huu kwenda nyumbani kwa Edward Lowassa kumshinikiza achukue fomu ya kugombea urais. I hope Mapadre hawamo humo. Mungu atuepushe.
Yaani Kanchi ketu haka kanaendeshwa kwa ujanja ujanja na wiziwizi tu. Mtu akiwa na hela zake basi anafanya jambo lolote tu-Julius Mtatiro
13. Lowassa ni dhaifu-MBOWE
14. #KATAALOWASSAKWENDAIKULUJIZIII !-Yeriko Nyerere
 
Huwa sielewi maadili ya watu wa chama na serikali ni ya sayari gani.Nadhani ukishatuhumiwa kwa lolote,ina maana wale unaowaongoza wamesha-loose confidence na wewe.Kama wamesha-loose confidence na wewe you can't exercise any authority over them, which means you have got to quit.Tuhuma hizi kwamba Kinana ni baron wa pembe za ndovu,kwa niaba yake binafsi na kwa niaba ya CCM ni za muda mrefu sana.Na inasemekana yeye ndiye co-ordinator wa biashara hiyo haramu kwa niaba ya CCM.Halafu eti wanamnyoshea Lowassa vidole.I just can't understand.Jamaa hawa wameoza kabisa.No they have got to go.
Jana kwa mara nyingine waziri Mkuu mstafu Ndg. F. Sumaye alimlipua katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi A. Kinana na kusema katibu mkuu huyo kwa muda mrefu amekuwa akijihusisha na uuzaji wa meno ya tembo (pembe za ndovu)... "Soma gazeti hapa chini"

Ilimbukwe kuwa mwaka jana kituo cha utangazaji cha Aljazeera kilitoa data kuhusu tembo wa Tanzania kuuwawa na kuonyesha kwamba mwaka 2007 kulikuwa na jumla ya tembo 146,879 na mpaka mwaka jana 2014 tembo hao wameuwawa kwa asilimia 64% na kubaki tembo 56,000 tu...

Mytake: Hili suala la Kinana tulifikiri ni uzushi ila ukiona waziri mkuu aliyekaa madarakani kwa miaka 10 kaliweka wazi mbele ya wananchi ni wazi hakuna ubishi tena katika hilo....
 
Back
Top Bottom