Sumaye: Kinana anapiga dili za meno ya Tembo

Wanachofanya ni kuprun tu maana tembo wamekuwa wengi mpaka mashambani wanakuja wengi
 
Wakuu kuuliza si Ujinga hivi hizo ni Pembe au Meno ya Ndovu?
Pili hua yanafanyia kazi gani au ni Malighafi ya kutengenezea bidhaa gani?
Wewe unauliza vitu vidovidogo nenda kajisomee utajua kama ni pembe au meno. pia utajua kwanini ni dili katika baadhi ya mataifa.
 
Ni hivi? Halafu leo anasifiwa kwa kufanya makubwa!
 
Kwa nchi inayojali uadilifu,tuhuma tu zinatosha kumuengeu mtu in any post,lakini sio kwenye nchi yangu Tanzania.Very sad.Nashangaa hata baada ya tuhuma kwamba Kinana anashiriki kwenye biashara haramu ya pembe za ndovu,bado ameendelea kukumbatiwa CCM.Inaudhi to say the least.
 
Kweli tumsikilize Sumaye . Sumaye Frederick Tiruway??? Mh
 
Kweli tumsikilize Sumaye . Sumaye Frederick Tiruway??? Mh
Sawa tunaweza tusimsikilize Sumaye,ingawa nazo ni tuhuma.Na hata hivyoo, kwa nini tusimsikilize Sumaye na tumdharau,kwa kuwa alihama chama chetu?Funny reasoning.Lakini labda tujiulize,kwani tuhuma kwamba Kinana anashiriki kwenye biashara haramu ya pembe za ndovu ni za leo,mbona hazikufuatiliwa?Na Sumaye mbona sio wa kwanza kuzitoa?Kwa nini hatuzifuatiliwi, ili kujiridhisha kwamba si za kweli?Kwa kuwa ni mwenzetu na tunaogopa kukiabisha chama?Also funny reasoning.Mimi naomba, with all due respect kwa chama changu,ifike mahali tujue kwamba mawazo haya hayakijengi chama na badala yake yanakibomoa.Kunapokuwa na tuhuma lazima zifuatiliwe,bila kujali zinamhusu nani na nani kazitoa,vinginevyo tuteendelea kufuga wezi,majambazi na wahuni kwenye chama,na hivyo kuendelea kukifanya chama kiendelee kudharaulika.I for one desire a respectable party.
 
Jungu Kuu! Haya ndo maelezo ya tunavyomfahamu.
 
Hili haliwaingii akina Kikwete na Samia.
 
Nimeona watanzania wengi sana hawana imani kabisa na mzee Kinana hasa likija suala la usafirishaji wa nyara za serikali kama vile meno ya tembo.

Naomba kujua ni kipi kinafanya kundi hili kubwa la watu kukosa imani na huyu mzee? Mimi sidhani kama kwa umri wake anaweza mikiki mikiki ya kufukuzana na tembo mbugani.
 
kwani anaenda kukamata tembo na kuwang'oa meno yeye au anatuma watu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…