Sumbawanga: Madereva Bajaj waandamana kisa CHADEMA kushindwa kuwalipa baada ya kukodishwa kumpokea Freeman Mbowe

Wewe uliwahi kuona bodaboda/Bajaj anaweka mafuta Kwa hela yake kwenda kumpokea mwanasiasa Kwa kukodiwa akitegemea kulipwa baada ya kurudi?
Wamefeli sana.. Kutunga huu upupu.
 
Story wao, script wao, directors wao, location yao( angalia kushoto hapo kuna bendera yao).
 
Mbona MAGUFULI alwadhurumu VYETI FAKE Mafao yao mlikaa kimya ?
 
Wajinga mnazidi kuongezeka
 
1. Kama walienda ofisi za chadema kwa nini mleta mada asingeleta picha/ video wakiwa huko ofisini na badala yake ameleta wakiwa Wanafurahi kupiga kelele za kijiweni kwao. Tafsiri ni kwamba huu ni uzushi uliopangwa hapo kijiweni maana ingekuwa na uhalisia wangedaiana ofisini.

2. Siyo lazima kwenda sumbawanga kujua ukweli vielelezo ulivyovileta vimetosha kuthibitisha uongo wa kitoto na kama ninyi Ndio mnaotegemewa kutengeneza propaganda basi mrudi shule.

3. Mwonekano wa mtu ktk tukio nao waweza kuwa ni kiashiria cha tukio, haiwezekani kwamba kweli wewe uwe unadai kudhurumiwa tena kwa mwendesha bodaboda au bajaji kiasi cha sh 10,000 halafu adai haki yake akiwa anacheka na kuimba mapambio, wewe uliona wapi uhalisia huo kama si maigizo.
 
Na mimi nawachukia wajinga kama nyie. Ambao mkiambiwa jambo mnakubali bila kufanya uchunguzi.
Unajua Hawa wanaoambiwa ujinga Kisha wanaamini ndio wajinga zaidi kuliko walio Tunga ujinga huo.
Yaani jitu like humu JF na linajiita great thinker halafu linadanganywa na kuamini kama zuzu?? Upuuzi mtupu
 
Kumbe jamaa wanakodisha wahudhuriaji wa mikutano!!!

Hahaaa, sishangai, maana Dar Kuna watu wanakodishwa kulia misibani.

Ukiangalia mikutano ya chadema, watu wamevaa jezi za Simba, Yanga, hawana uhusiano na chadema
Shabiki wa Simba au Yanga hawezi kuwa shabiki wa Chadema?
Amandla...
 
Acheni utoto? Sasa kwanini waende ofisi ya CCM kama wanadai Chadema?

Katibu wa Chadema keshasema wataenda mahakamani kufungua shitaka kuwafanyia Fujo kwenye eneo la biashara maana sio ofisi za chama pale!!
 
Wanafiki ni waongo. Imeandikwa, Yakobo 3:14 "Lakini mkiwa na wivu wenye uchungu na ugomvi mioyoni mwenu msijisifu wala msiseme uongo juu ya kweli."
 
Poleni sana Bajaj Sumbawanga. Daini haki yenu kwa hawa wadhulumishi wa CHADEMA. Hata wakiwalipa msisahau kuwaadhibu kwenye sanduku la kura kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa hadi uchaguzi mkuu 2025. Hiki chama kilichojaa dhuluma lazima kipotee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…