Sumbawanga: Madereva Bajaj waandamana kisa CHADEMA kushindwa kuwalipa baada ya kukodishwa kumpokea Freeman Mbowe

Sumbawanga: Madereva Bajaj waandamana kisa CHADEMA kushindwa kuwalipa baada ya kukodishwa kumpokea Freeman Mbowe

Story wao, script wao, directors wao, location yao( angalia kushoto hapo kuna bendera yao).
 
Madereva Bajaj wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa wameandama hadi kwenye ofisi za Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA aitwaye Cedrick Malila almaarufu IKUWO WAKIDAI MALIPO YAO waliyoahidiwa wakati wamekodishwa kwenda kumpokea Mwenyekiti cha CHADEMA Freeman Mbowe huko Katumba.

Akizungumza mmoja wa madereva aliyejitambulisha kwa jina la Kelvin Nobert anaeleza kuwa walikodiwa na CHADEMA ili wampokee Mbowe kutoka eneo la Katumba hadi Nduwa kwa malipo shilingi 10,000 lakini pamoja na ukweli kwamba walizidisha muda wa kufanya kazi kutoka saa 4 hadi 10 bado CHADEMA haijawalipa hata shilingi moja

TAZAMA VIDEO HAPA CHINI
View attachment 2531555
Mbona MAGUFULI alwadhurumu VYETI FAKE Mafao yao mlikaa kimya ?
 
Chadema ni kampuni ya watu wachache sio chama cha siasa..nikampuni ya wachagga..kama ni chama cha democrasia kweli ..kwanini mbowe ni mwenyekiti zaidi ya miaka 30,tokea nikiwa mdogo mpaka leo namsikia mbowe tu.

Huku Arusha madiwani wengi wa chadema enzi hizo walikuwa wachagga tu yaani asilimi kama 90,tofauti na ccm madiwa ni mchanganyiko hawachagui kabila..hata viongozi wa chama huku katika ngazi mbalimbali wengi ni wachagga...

Sasa najiuliza mbona kuna makabila mengi mfano,waarusha,wamasai,wameru,warangi,wasomali,na mengine ambao wana uwezo mkubwa sana kwanini wasipewe hiyo fursa ya kugombea?
Wajinga mnazidi kuongezeka
20221207_064831.jpg
 
1. Habari imeandikwa wameenda Ofisini kwa MWENYEKITI. Sasa kama unaona hapo ofisini kwa MWENYEKITI WA CHADEMA ni Kijiweni sawa.
2.Hoja yako ya pili nenda Sumbawanga ukafanya confimation
3. Hongera sana mtaalamu wa kujua wadai na wadaiwa kwa kuangalia mionekano
1. Kama walienda ofisi za chadema kwa nini mleta mada asingeleta picha/ video wakiwa huko ofisini na badala yake ameleta wakiwa Wanafurahi kupiga kelele za kijiweni kwao. Tafsiri ni kwamba huu ni uzushi uliopangwa hapo kijiweni maana ingekuwa na uhalisia wangedaiana ofisini.

2. Siyo lazima kwenda sumbawanga kujua ukweli vielelezo ulivyovileta vimetosha kuthibitisha uongo wa kitoto na kama ninyi Ndio mnaotegemewa kutengeneza propaganda basi mrudi shule.

3. Mwonekano wa mtu ktk tukio nao waweza kuwa ni kiashiria cha tukio, haiwezekani kwamba kweli wewe uwe unadai kudhurumiwa tena kwa mwendesha bodaboda au bajaji kiasi cha sh 10,000 halafu adai haki yake akiwa anacheka na kuimba mapambio, wewe uliona wapi uhalisia huo kama si maigizo.
 
Na mimi nawachukia wajinga kama nyie. Ambao mkiambiwa jambo mnakubali bila kufanya uchunguzi.
Unajua Hawa wanaoambiwa ujinga Kisha wanaamini ndio wajinga zaidi kuliko walio Tunga ujinga huo.
Yaani jitu like humu JF na linajiita great thinker halafu linadanganywa na kuamini kama zuzu?? Upuuzi mtupu
 
Kumbe jamaa wanakodisha wahudhuriaji wa mikutano!!!

Hahaaa, sishangai, maana Dar Kuna watu wanakodishwa kulia misibani.

Ukiangalia mikutano ya chadema, watu wamevaa jezi za Simba, Yanga, hawana uhusiano na chadema
Shabiki wa Simba au Yanga hawezi kuwa shabiki wa Chadema?
Amandla...
 
1. Habari imeandikwa wameenda Ofisini kwa MWENYEKITI. Sasa kama unaona hapo ofisini kwa MWENYEKITI WA CHADEMA ni Kijiweni sawa.
2.Hoja yako ya pili nenda Sumbawanga ukafanya confimation
3. Hongera sana mtaalamu wa kujua wadai na wadaiwa kwa kuangalia mionekano
Acheni utoto? Sasa kwanini waende ofisi ya CCM kama wanadai Chadema?

Katibu wa Chadema keshasema wataenda mahakamani kufungua shitaka kuwafanyia Fujo kwenye eneo la biashara maana sio ofisi za chama pale!!
 
Wanafiki ni waongo. Imeandikwa, Yakobo 3:14 "Lakini mkiwa na wivu wenye uchungu na ugomvi mioyoni mwenu msijisifu wala msiseme uongo juu ya kweli."
 
Poleni sana Bajaj Sumbawanga. Daini haki yenu kwa hawa wadhulumishi wa CHADEMA. Hata wakiwalipa msisahau kuwaadhibu kwenye sanduku la kura kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa hadi uchaguzi mkuu 2025. Hiki chama kilichojaa dhuluma lazima kipotee.
 
Back
Top Bottom