Sumu Kali kupita zote Duniani iliyotumika kumshambulia jasusi Wa Urusi alieasi Akiwa Uingereza

Sumu Kali kupita zote Duniani iliyotumika kumshambulia jasusi Wa Urusi alieasi Akiwa Uingereza

Junior Clinton Mr.

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
1,075
Reaction score
1,423
Novichok: Mambo muhimu kuhusu sumu kali ya Urusi iliyotumiwa kumshambulia jasusi


Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May Jumatatu alisema jasusi wa zamani wa Urusi na binti yake walipewa sumu kali ambayo ni sehemu ya kundi la kemikali za sumu kwa jina Novichok.

Sergei Skripal na binti yake Yulia bado wamo katika hali mahututi hospitalini kufuatia jaribio hilo la kuwaua eneo la Salisbury mnamo 4 Machi.

Kemikali hiyo ilitambuliwa na wataalamu katika maabara ya ulinzi na sayansi Porton Down.

Tunafahamu nini kuhusu kundi hili la kemikali zenye sumu?

1) Ziliundwa katika Muungano wa Usovieti

Jina Novichok maana yake ni "mgeni" kwa lugha ya Kirusi.

Ni jina linalotumiwa kurejelea kemikali za sumu ambazo hushambulia mfumo wa neva mwilini.

Kemikali hizo ziliundwa na Muungano wa Usovieti miaka ya 1970 na 1980.

Theresa May: Urusi imehusika kumshambulia Sergei Skripal

Zilifahamika kama silaha za kemikali za kizazi cha nne na zilistawishwa chini ya mpango wa silaha za Muungano wa Usovieti uliofahamika kama "Foliant".

Mwaka 1999, maafisa wa ulinzi kutoka Marekani walisafiri hadi Uzbekistan kusaidia kuvunja na kusafisha moja ya eneo kubwa zaidi lililotumiwa kufanyia majaribio silaha za kemikali na Muungano wa Usovieti.

Kwa mujibu wa afisa mmoja wa ngazi za juu ambaye alitorokea Marekani, maafisa wa Usovieti walitumia kiwanda kilichokuwa eneo hilo kuunda na kufanyia majaribio sampuli za kemikali ya Novichok. Kemikali hii iliundwa mahsusi kutoweza kugunduliwa na wakaguzi wa silaha na sumu katika mataifa mengine.


2) Ni sumu yenye nguvu kuliko sumu nyingine

Moja ya kemikali hizi zinazofahamika kama Novichok - A-230 - inadaiwa kuwa na nguvu mara 5-8 zaidi ya sumu nyingine hatari kwa jina VX.

"Hii ni sumu hatari na changamano kushinda sumu aina ya sarin au VX na pia huwa vigumu zaidi kuitambua," anasema Prof Gary Stephens, mtaalamu wa kemikali katika Chuo Kikuu cha Reading.

Sumu ya VX ndiyo iliyotumiwa kumuua ndugu wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un mwaka jana, kwa mujibu wa Marekani.

Aina mbalimbali za kemikali hii ya A-230 zimekuwa zikitengenezwa, na aina moja inadaiwa kuidhinishwa na jeshi la Urusi itumike kama silaha ya kemikali.

3) Aina mbalimbali za Novichok

Ingawa baadhi ya aina za sumu hii ya Novichok huwa majimaji, kuna aina nyingine ambazo ni yabisi (gumu au isiyokuwa majimaji).

Ni kemikali ambayo pia inaweza kugeuzwa kuwa poda laini.

Baadhi ya sumu hizi pia hudaiwa kutumiwa kama "silaha za ngazi mbili". Hii ina maana kwamba sumu hii huhifadhiwa mara nyingi kama kemikali aina mbili ambazo zikiwa kando kando si hatari. Zinapochanganywa, huingiliana na kutengeneza sumu.

Hii huifanya rahisi sana kwa viungo vya kemikali hii kusafirishwa kwani huwa sumu tu zikichanganywa.

"Moja ya sababu ambayo hufanya sumu hizi kuandaliwa ni kwa sababu viungo vyenyewe havijapigwa marufuku," anasema Prof Stephens.

"Hii ina maana kwamba kemikali hizi ambazo huchanganywa huwa rahisi sana kusafirishwa bila kuwa hatari kwa anayezisafirisha."

4) Zinaweza kuathiri mtu haraka sana

Mtu anapopumua sumu ya Novichok, au hata ikigusa ngozi yake, basi huanza kumuathiri upesi.

Dalili zake zinaweza kuanza kujionesha katika kipindi cha muda mfupi hivi, sekunde 30 hadi dakika mbili.

Hata hivyo, sumu hii ikiwa kama poda huchukua muda zaidi kuanza kuathiri mtu.

Dalili kali zinaweza kuanza kujionesha saa 18 baada ya mtu kukumbana na sumu hiyo.

Sumu aina ya Novichok

Mara 5 hadi 8

hatari zaidi ya sumu ya VX

2 kemikali ambazo hazina sumu zinazoweza kuchanganywa na kuunda sumu hii

Sekunde 30 Muda ambao unatosha kwa dalili za sumu kuanza kujionesha

1970 Kipindi ambacho sumu hii iliundwa na Muungano wa Usovieti

Science Direct

EPA

5) Dalili zake ni sawa na za sumu nyingine za neva

Sumu aina ya Novichok huwa na madhara sawa na ya sumu nyingine zenye kushambuliwa mfumo wa neva.

Hii ina maana kwamba huwa zinafanya kazi kwa kuzuia ujumbe au mawasiliano kati ya mfumo wa neva na misuli, na pia kusambaratisha shughuli nyingi muhimu za mifumo mwilini.

Dalili zake ni pamoja na macho kuwa na rangi nyeupe, huku mboni za macho zikiminyika, mtukutiko wa maungo, na mtu kuonekana kupumbaa. Wakati mwingine, mtu hupoteza fahamu, kushindwa na kupumua na kufariki.

Sumu hizi kimsingi hufanya moyo kupunguza mapigo yake na kubana njia zinazotumiwa na mwili kupumua na mwishowe mtu kufariki kutokana na mtu kukosa hewa ya kutosha.

Baadhi ya aina za sumu hii ya Novichok zimeundwa mahsusi kuhakikisha dawa za kawaida za kupoza nguvu ya sumu haziwezi kufanikiwa.

Iwapo mtu amepewa sumu huu, anafaa kuvuliwa mavazi yake na ngozi yake kuoshwa vyema kwa maji na sabuni.

Macho yake yanafaa pia kuoshwa vyema kwa maji na apewe hewa ya oksijeni.
 
Vipi kuhusu poleniam210. Hii nayo ni kiboko. Kuna taarifa gharama ya kuisafirisha ni kubwa na ni hatari hata kwa msafirishaji
 
Vipi kuhusu poleniam210. Hii nayo ni kiboko. Kuna taarifa gharama ya kuisafirisha ni kubwa na ni hatari hata kwa msafirishaji
AHuyu jamaa aliuwawa kifo cha kimbwa sana, yaani alikuwa anatia huruma

lexander Litvinenko

_76572847_003348062-1.jpg
 
Waingereza wamefanya false flag operation. Kuna kitu wanataka baada ya hilo tukio, mda utasema
hapana mkuu kumbuka mke wa jamaa alifariki katika ajai ya gari iliokua na utata huko urusi, baadae mtoto wake akaja kufariki kwa njia hiohio huko urusi, sasa hivi hawa memberb wawili wa familia waliobaki nao wako mahututi baada ya shambulizi hilo..sidhan km ni false flag ukiangalia hio trend
 
hapana mkuu kumbuka mke wa jamaa alifariki katika ajai ya gari iliokua na utata huko urusi, baadae mtoto wake akaja kufariki kwa njia hiohio huko urusi, sasa hivi hawa memberb wawili wa familia waliobaki nao wako mahututi baada ya shambulizi hilo..sidhan km ni false flag ukiangalia hio trend
Sasa huoni kutokana na hiyo Historia kwamba ni rahisi kuwanyooshe kidole Urusi? Ndio mtu muafaka wa kumfanyia operation. Majasusi sio watu aisee.
 
Back
Top Bottom