Sumu Kali kupita zote Duniani iliyotumika kumshambulia jasusi Wa Urusi alieasi Akiwa Uingereza

Sumu Kali kupita zote Duniani iliyotumika kumshambulia jasusi Wa Urusi alieasi Akiwa Uingereza

Novichok: Mambo muhimu kuhusu sumu kali ya Urusi iliyotumiwa kumshambulia jasusi


Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May Jumatatu alisema jasusi wa zamani wa Urusi na binti yake walipewa sumu kali ambayo ni sehemu ya kundi la kemikali za sumu kwa jina Novichok.

Sergei Skripal na binti yake Yulia bado wamo katika hali mahututi hospitalini kufuatia jaribio hilo la kuwaua eneo la Salisbury mnamo 4 Machi.

Kemikali hiyo ilitambuliwa na wataalamu katika maabara ya ulinzi na sayansi Porton Down.

Tunafahamu nini kuhusu kundi hili la kemikali zenye sumu?

1) Ziliundwa katika Muungano wa Usovieti

Jina Novichok maana yake ni "mgeni" kwa lugha ya Kirusi.

Ni jina linalotumiwa kurejelea kemikali za sumu ambazo hushambulia mfumo wa neva mwilini.

Kemikali hizo ziliundwa na Muungano wa Usovieti miaka ya 1970 na 1980.

Theresa May: Urusi imehusika kumshambulia Sergei Skripal

Zilifahamika kama silaha za kemikali za kizazi cha nne na zilistawishwa chini ya mpango wa silaha za Muungano wa Usovieti uliofahamika kama "Foliant".

Mwaka 1999, maafisa wa ulinzi kutoka Marekani walisafiri hadi Uzbekistan kusaidia kuvunja na kusafisha moja ya eneo kubwa zaidi lililotumiwa kufanyia majaribio silaha za kemikali na Muungano wa Usovieti.

Kwa mujibu wa afisa mmoja wa ngazi za juu ambaye alitorokea Marekani, maafisa wa Usovieti walitumia kiwanda kilichokuwa eneo hilo kuunda na kufanyia majaribio sampuli za kemikali ya Novichok. Kemikali hii iliundwa mahsusi kutoweza kugunduliwa na wakaguzi wa silaha na sumu katika mataifa mengine.


2) Ni sumu yenye nguvu kuliko sumu nyingine

Moja ya kemikali hizi zinazofahamika kama Novichok - A-230 - inadaiwa kuwa na nguvu mara 5-8 zaidi ya sumu nyingine hatari kwa jina VX.

"Hii ni sumu hatari na changamano kushinda sumu aina ya sarin au VX na pia huwa vigumu zaidi kuitambua," anasema Prof Gary Stephens, mtaalamu wa kemikali katika Chuo Kikuu cha Reading.

Sumu ya VX ndiyo iliyotumiwa kumuua ndugu wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un mwaka jana, kwa mujibu wa Marekani.

Aina mbalimbali za kemikali hii ya A-230 zimekuwa zikitengenezwa, na aina moja inadaiwa kuidhinishwa na jeshi la Urusi itumike kama silaha ya kemikali.

3) Aina mbalimbali za Novichok

Ingawa baadhi ya aina za sumu hii ya Novichok huwa majimaji, kuna aina nyingine ambazo ni yabisi (gumu au isiyokuwa majimaji).

Ni kemikali ambayo pia inaweza kugeuzwa kuwa poda laini.

Baadhi ya sumu hizi pia hudaiwa kutumiwa kama "silaha za ngazi mbili". Hii ina maana kwamba sumu hii huhifadhiwa mara nyingi kama kemikali aina mbili ambazo zikiwa kando kando si hatari. Zinapochanganywa, huingiliana na kutengeneza sumu.

Hii huifanya rahisi sana kwa viungo vya kemikali hii kusafirishwa kwani huwa sumu tu zikichanganywa.

"Moja ya sababu ambayo hufanya sumu hizi kuandaliwa ni kwa sababu viungo vyenyewe havijapigwa marufuku," anasema Prof Stephens.

"Hii ina maana kwamba kemikali hizi ambazo huchanganywa huwa rahisi sana kusafirishwa bila kuwa hatari kwa anayezisafirisha."

4) Zinaweza kuathiri mtu haraka sana

Mtu anapopumua sumu ya Novichok, au hata ikigusa ngozi yake, basi huanza kumuathiri upesi.

Dalili zake zinaweza kuanza kujionesha katika kipindi cha muda mfupi hivi, sekunde 30 hadi dakika mbili.

Hata hivyo, sumu hii ikiwa kama poda huchukua muda zaidi kuanza kuathiri mtu.

Dalili kali zinaweza kuanza kujionesha saa 18 baada ya mtu kukumbana na sumu hiyo.

Sumu aina ya Novichok

Mara 5 hadi 8

hatari zaidi ya sumu ya VX

2 kemikali ambazo hazina sumu zinazoweza kuchanganywa na kuunda sumu hii

Sekunde 30 Muda ambao unatosha kwa dalili za sumu kuanza kujionesha

1970 Kipindi ambacho sumu hii iliundwa na Muungano wa Usovieti

Science Direct

EPA

5) Dalili zake ni sawa na za sumu nyingine za neva

Sumu aina ya Novichok huwa na madhara sawa na ya sumu nyingine zenye kushambuliwa mfumo wa neva.

Hii ina maana kwamba huwa zinafanya kazi kwa kuzuia ujumbe au mawasiliano kati ya mfumo wa neva na misuli, na pia kusambaratisha shughuli nyingi muhimu za mifumo mwilini.

Dalili zake ni pamoja na macho kuwa na rangi nyeupe, huku mboni za macho zikiminyika, mtukutiko wa maungo, na mtu kuonekana kupumbaa. Wakati mwingine, mtu hupoteza fahamu, kushindwa na kupumua na kufariki.

Sumu hizi kimsingi hufanya moyo kupunguza mapigo yake na kubana njia zinazotumiwa na mwili kupumua na mwishowe mtu kufariki kutokana na mtu kukosa hewa ya kutosha.

Baadhi ya aina za sumu hii ya Novichok zimeundwa mahsusi kuhakikisha dawa za kawaida za kupoza nguvu ya sumu haziwezi kufanikiwa.

Iwapo mtu amepewa sumu huu, anafaa kuvuliwa mavazi yake na ngozi yake kuoshwa vyema kwa maji na sabuni.

Macho yake yanafaa pia kuoshwa vyema kwa maji na apewe hewa ya oksijeni.
Sasa huyo jasusi aliwekewage hiyo sumu?
 
Asante mkuu.
Imebidi niende Google kuiangalia familia ya Sergei.
Kumbe Yulia ni binti mdogo tu wa miaka 33.
Sasa kama kosa katenda baba mtu, why waiteketeze familia nzima?
Kwanini wasishughulike na baba tu mpaka wanaamua kuua familia nzima?
Mama, mtoto na sasa baba na mtoto wanakufa.
Nashangaa!!!!!!
nadhani unajua kitu kinaitwa kisasi
kwa
mfano akiwachwa huyo mtoto na serikali ya uingereza iamue kumlisha maneno na kumjaza sumu ya chuki anaweza kuja kutumika kufanya kisasi kibaya mno hapo baadae.

pia hao jamaa wanaishi kwa principle moja tu, akuanzae mmalize.
 
AHuyu jamaa aliuwawa kifo cha kimbwa sana, yaani alikuwa anatia huruma

lexander Litvinenko

_76572847_003348062-1.jpg
POLONIUM210 NOMA KAMA MBEKYEMWA.
 
nadhani unajua kitu kinaitwa kisasi
kwa
mfano akiwachwa huyo mtoto na serikali ya uingereza iamue kumlisha maneno na kumjaza sumu ya chuki anaweza kuja kutumika kufanya kisasi kibaya mno hapo baadae.

pia hao jamaa wanaishi kwa principle moja tu, akuanzae mmalize.
OK hapo pa kisasi na kulishwa maneno nimewaelewa vyema.
Aisee
Ila huruma sana jamani.
Kosa la Dad linacost maisha ya familia.
Dah!!
Very sad sana
 
Alikiuka sheria ya "trust will get you killed" (anti trust)mpk mtu kapata nafasi ya kumuwekea hiyo sumu alimwamini kama jamaa wa krb....
 
Putin ni mtu mmoja hatari sana duniani ,ni dictator alie kubuhu na bdo ana unga mkono na kufadhili ma dictator kma kule Syria Nk
 
Amewekewa Vp hyo sumu wakati huyo jamaa alikuwa na ulinzi wa serikali ingekuwa bongo tungesema kajiwekea sumu kutafuta kik
Uki-google wanasema alitembelewa na bintiye kutoka kwako Russia so inawezekana alipitishiwa hiyo sumu kutoka kwa mwanae ambaye naye yupo ktk hali mbaya.
 
Waingereza wamefanya false flag operation. Kuna kitu wanataka baada ya hilo tukio, mda utasema

wamekazana kutafuta uhungwaji mkono...tuu..
kama wapo serious sana na waiondoe timu yao kwenye world cup.....
kama bi.theresa kasema hakuna mwana wa mfalme atakaeudhuria.....mashindano hayo...
 
Back
Top Bottom