Supplier wangu Muhindi aliekuwa na deni la Bilioni 80 kalimaliza, Nimekaa na kutafakari hawa watu wapo serious na biashara, bado tuna safari ndefu

Wahindi ni Moja ya jamii ambayo ni waaminifu sana linapokuja suala la pesa na biashara, ni watu ambao Wana heshimu sana deni na wakikopa pesa wanajitahidi kadri wawezavyo waishi kulingana na mkataba unavyosema.

Wakikopa pesa wanaipeleka yote kwenye biashara kusudiwa, na ndio maana kwenye marejesho hawasumbui hata kidogo.

Tofauti kabisa na waswahili ambao wanakopa pesa lakini hawako tayari kuheshimu mkataba wa mkopo... mbongo anakopa 10m halafu kwenye biashara husika aliyoiombea mkopo anaweka 4m pekee tu, pesa nyingine yote iliyobaki anaitapanya kwenye petty issues ambazo hazimuingizii Hela.

....haya ukifika wakati wa kuleta marejesho anaanza kuteseka, Kwa sababu return anayoipata kwenye biashara ni ndogo sana kuwiana na kiasi cha rejesho analopaswa kuleta, na hiyo inatokana na kuwekeza kiasi kidogo sana Cha pesa kwenye biashara.

....atajitahidi kuleta marejesho miezi ya awali, halafu baada ya hapo ataanza excuses mara ohoo biashara ngumu, nivumilie sijui Nini, baadae ataacha kabisa hata kupokea Simu za maafisa mikopo mwisho WA siku mnafikishana mahakamani Kwa kesi ya madai.

Ngozi nyeusi/waswahili ni watu WA ovyo sana linapokuja suala la uaminifu kwenye pesa na ndio maana Mimi Huwa naamini siku zote biashara yoyote ambayo unategemea uaminifu kama msingi mkuu WA kustawi Kwake, basi hiyo biashara sio ya kufanya na wabongo waswahili.
 
Muibukie kwake na wadau Kama wa3, lazima akulipe kwa wenge😂🤣
Mpuuzi yule pale kwake nilipokuwa napafahamu Mimi alishahama, alishindwa Kodi... Na huko alipo hamia sipajui.

Hata deni nimeamua kuachana nalo tu baada ya kumuona ni mjinga.

Imagine mtu mmekuwa marafiki tangu mkiwa form two halafu leo hii urafiki wenu unakuja kuvunjwa na 36,000/=?
 
Eqe jobless pro max acha ubishi, namjua dogo 1 ni same age na Mimi.

his business makes 18m per month, siku tume kutana tukawa tuna jadili deals & challenges.

Nili jifunza vingi Sana, as a competitor na rafiki
Duh ujue wengine badogo tunakunywa supu ya miatano mkuu uliniambia watu. Wanamake bilions🤣mimi na kagenge langu siku niktengeneza profit 50k ni sherehe
 
🤣🤣🤣 hebu kwanza ncheke mana wanachofanyiwa hao pesa x na wakopaji
Watazifunga tu hizo app zao kama TALA.

Moja ya biashara ambayo mtu hatakiwi kufanya hapa Tanzania ni hii biashara ya kukopesha pesa...!

Wabongo suala la uaminifu walishafeli.

Biashara yoyote Ile ambayo inahusisha nidhamu na uaminifu kama msingi mkuu WA kustawi kwake, hiyo biashara sio ya kufanya na wabongo.
 
K
Kwanini umkopeshe rafiki yako wa kitambo elf 36? Mtu mpaka anakopa 36k ni majalala, ungemwambia huna au umpe tu . 36k ni kitu cha kuanza kumsumbua rafiki yako ambae hana kitu
 
Iko hivi; kama aliamninwa na Benki na hatimaye kupewa mkopo wa kiasi hicho, maana yake ni kwamba investment zake zilikuwa na uwezo wa kufanya biashara ya kiasi hicho na pia kupata faida.. Kwa hiyo mimi nakushauri usishangae mtu huyu kurudisha mkopo wa billion 80 bali unatakiwa ushangae namna alivyoweza ku-invest hadi kufikia kuwa na CAPITAL hiyo iliyompelekea akaweza kuaminiwa na Benki hadi akakopeshwa Billion 80
Ni muhimu ukajua hilo kwa sababu inaweza kukusaidia hata wewe ukawa investor mkubwa au mtu mwingine aliye karibu na wewe
Nakushauri urudi tena kwa rafiki yako wa Benki ili akakusaidie kupata details zaidi kuhusiana na mtu huyu
 
Ukitaka kupata taarifa zetu vzur waulize kampuni za sm zinazokopesha zitakuambia watanganyika ni mbwa kabisa,deni la elfu 5 mtu anatupa laini

Kumbe hata mbunge wetu atatoboa anadaiwa bil 1 ila deni limemsumbua sana
 
Deni la B80! kalifuta ? Age 30yrs ? Kama n real : Inavutia.

Kuondoa ukakasi
Nadhani Ungeshusha details zaidi Hilo deni lina mda gani na anapush biashara gani

Ukishindwa huu Uzi ni chai pro maximum
#73
 
K

Kwanini umkopeshe rafiki yako wa kitambo elf 36? Mtu mpaka anakopa 36k ni majalala, ungemwambia huna au umpe tu . 36k ni kitu cha kuanza kumsumbua rafiki yako ambae hana kitu
Boss jamaa alinikopesha 100,000/= Kwa makubaliano baada ya wiki mbili atanirudishia pesa yangu...ila ilimchukua mwezi mzima kunirejeshea, ambapo na penyewe alinirushia kwenye simu 65,000/=(nikatoa buku ya makato) akaniambia nyingine iliyobaki atanipa kesho yake.

Hiyo kesho yake ndio zikaanza kalenda nyingi mpaka akafikia hatua ya kutopokea simu.

Lakini Pamoja na njaa zangu, kuhusu deni nilisha samehe muda sana ila yeye ndio Bado anajishtukia, yes alikuwa ni mwanangu mno na tulikuwa na mipango mingi na yeye ikiwemo kwenda nje ya nchi...!! Huwa naskitika sana kila nikimkumbuka.
 
Anazingua angekwambia tu nimekwama mbona hela ndogo tu, mngeweza kufanya makubwa zaidi
 
Ushahawai kusikia tajiri wa kihindi anatunza bendi ?

Ushawai kuona harusi ya wahindi hapa Tanzania wamemlipa Mc ama Dj milioni 5 kama jinsi weusi tunavyomlipa Mc garab ?
ukifanya nao kazi maofisini, ikifika mchana anafungua kibegi chake anatoa msosi aliobeba kutoka home...hawana ujinga wetu wa kila siku kwenda kula vibandani na kwenye vihoteli uchwara...they live simple cheap life lakini wanawekeza sana na wana ukwasi wa hela!
 
Wewe ni mpumbavu fulani hivi, badala ya kuichukulia kama game changer/catalyst ya kukufanya uzinduke kwenye mawazo mgando, wewe unajifanya kichwa ngumu. Hakika wewe ndio mfano hai wa ngozi nyeusi
Jinga kabisa ili jamaa.sio kila kitu kanuni kanuni tuuuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…