Michael Amon
JF-Expert Member
- Dec 22, 2008
- 8,768
- 3,622
Jinsi ya kupika supu ya ulimi wa ng'ombe/nyama ya ng'ombe/mkia wa ng'ombe/makongoro/nyama ya mbuzi/samaki/kuku/utumbo
Mahitaji
Jinsi ya kupika
NB: Unaweza kuipika pamoja nyanya ili kuongeza ladha zaidi kama ukipenda.
Mahitaji
- Ulimi wa ng'ombe/nyama ya ng'ombe/mkia wa ng'ombe/makongoro/nyama ya mbuzi/samaki
- Soy sauce
- Ndimu au limao
- Kitunguu saumu
- kitunguu maji
- Tangawizi
- Chumvi
- Pilipili
- Karoti
Jinsi ya kupika
- Bandika sufuria jikoni, weka nyama ya ulimi wa ng'ombe/nyama ya ng'ombe/mkia wa ng'ombe/makongoro/nyama ya mbuzi/samaki, kamulia ndimu, weka vitunguu saumu na karoti.
- Kata karoti na kitunguu maji vipande vidogo kisha viweke kwenye sufuria yako.
- Weka maji ya kutosha kisha funika sufuria na mfuniko.
- Ikikaribia kuiva weka soy sauce, hii inasaidia kuongeza ladha kwenye supu.
- Onja kama nyama imeiva, kama tayari weka pilipili. Vilevile unaweza kuongeza pililipi ukishaipua supu toka jikoni.
NB: Unaweza kuipika pamoja nyanya ili kuongeza ladha zaidi kama ukipenda.
Jinsi ya kupika supu ya pweza
![]()
Mahitaji
- 1 Samaki pweza mkate na msafishe vizuri
- 50 gram kitunguu swaumu
- 100 gram kitunguu maji chop chop
- 100 gram kariti kata vipande vidogo
- 1 pilipili ya kijani fresh
- 1 kijiko kidogo cha chai unga wa korienda au girigilani
- Chumvi
- 5 gram pilipili manga
- 100 ml mafuta ya kupikia
- 50 ml juisi ya Limao
- 150 gram nyanya ya kopo
- 1.5 lita ya Maji
Jinsi ya kupika
- Weka mafuta katika sufuria kisha kaanga kitunguu maji na kitunguu swaumu.
- Baada ya hapo weka pweza kaanga kwa dakika 10 kisha weka viungo vyote vilivyobakia kaanga kidogo.
- Weka maji chemsha katika moto wa wastani kwa dakika 15 na baada ya hapo itakua imeiva na tayari kwa kuliwa.
Jinsi ya kupika supu ya maboga
![]()
Mahitaji
- 240 gram maboga yaliyomenywa yakachemshwa pamoja na kitunguu maji kimoja na kusagwa katika blenda
- 60 gram Karanga ya kusaga (peanut butter) laini kabisa
- 1 kijiko kikubwa cha chakula siagi
- 1 Kiazi kitamu
- Chumvi
- 5 gram pili pili manga
Jinsi ya kupika
- Safisha na katakata viazi vitamu kisha vichemshe na vikishachemka toa viazi vyako ktk sufuria kisha viweke kwenye blender na uvisage pia.
- Chukua siagi na uiweke ktk kiakaango chako kilichokwisha pata moto na ukaange ule mchanganyiko uliosagwa wa maboga, mchanganyiko wa viazi vitamu pamoja na peanut butter.
- Kisha ongezea maji kufanya mchanganyiko wako uwe laini na uweke chumvi na pili pili manga kupata ladha safi.
- Koroga mpaka iwe laini na imechanganyika vizuri hakikisha unachemsha kwa dakika 10 tu inakua tayari kwa kuliwa.