Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
MashaAllah uzi mtamu...supu ya pwezaaaaaa, naaaam! Naam!
Unapenda supu ya pweza eehh???
wauliza karafuu pemba yakheeee?
Ulimi wa ng'ombe!!! Unasafishwaje kwanza...tupe ujuzi mkuu ili hata ukiwa haukutengezwa vizuri tujue
Hii kitu mimi huwa ndo inanishinda kabisa, awe amekaangwa, amechemshwa, amechomwa, kaungwa n.k mimi huwa ananishinda.
Nimejaribu mara nyingi ila wapiii!!!!
Mi ulimi wa ng'ombe sijawahi kula nahisi km disgusting. Hata ubongo, korongo, kichwa vyote hivo havipandi abadan
Jinsi ya kupika supu ya karoti
Mahitaji![]()
- 2 kubwa carroti (ioshe vizuri kisha ikwangue kwangue. Usiimenye maganda)
- 1 kiazi kikubwa, (osha vizuri na katakata vipande vipande ikiwa na maganda yake
- 1 jani la celery, (kata kata na majani yake)
- 120 ml maziwa
- 1 kitunguu kikubwa, katakta vipande
- 5 gram kitunguu swaumu cha kusagwa
- 3 gram saffron (zafarani)
- Chumvi
- 5 gram pili pili manga
Jinsi ya kupika
- Chemsha carrots na viazi ulaya kwa dakika 4.
- Chukua maziwa ya uvugu vugu yaliyopo kwenye bakuli kisha weka saffron (zafarani).
- Weka kijiko kimoja cha mafuta katika sufuria yako yapate moto kisha weka kitunguu maji, kitunguu swaumu, chop celery na chumvi kisha kaanga mpaka iive kwa dakika 2.
- Chukua mchanganyiko wote na uumimine katika blender pamoja na carrots na viazi ulivyokwisha chemsha kisha saga.
- Baada ya kusaga vizuri kabisa rudisha katika sufuria na acha ichemke tena kwa dakika 2.
- Mimina maziwa yale uliyochanganya na saffron kisha punguza moto ichemke kwa dakika 3.
- Baada ya hapo supu yako itakuwa imeiva na tayari kwa kuliwa.
NB: Hakikisha unakoroga vizuri maziwa na mchanganyiko wako wa supu vichangayike vizuri kabisa wakati supu yako ikiwa bado jikoni.
Duhh!!! Hivi kumbe kuna watu wanakula ubongo? Makubwa!!!
Nimeona kumbe kila mtu ana kitu asichokipenda..
Mimi hapo kwenye pweza aisee nimejitahidi kuwapenda ila nimeshindwa!!! Nimekula kila mahali, nimejaribu waliochemshwa, waliokangwa n.k n.k vyote havipandi...yaani siku nikila pweza kesho yake siendi kazini naumwa tumbo balaa mpaka nachomwa sindano!!
Siku hizi hata nikipita tu pale ferry nikiwaona napatwa kichefuchefu kabisa yani!
Hee!! Pole. Au unanunua magengeni labda ndio tumbo likakuuma??
Ubongo unaliwa bwana. Siku moja home wifi yangu alipika hio kitu na nlikuwa sipo. Nliporudi nkakuta vitu mezani, na huo ubongo umekaa kama mayai yalikaangwa (crumble ) nikajua ni mayai, lohhh kula mwanangu haviliki. Kuuliza ndo naambiwa ubongo wa ng'ombe. Uroho uliniisha
This must be yummy.
Ubongo unaliwa bwana. Siku moja home wifi yangu alipika hio kitu na nlikuwa sipo. Nliporudi nkakuta vitu mezani, na huo ubongo umekaa kama mayai yalikaangwa (crumble ) nikajua ni mayai, lohhh kula mwanangu haviliki. Kuuliza ndo naambiwa ubongo wa ng'ombe. Uroho uliniisha
hata kwa hoteli nilishajaribu...actually sea foods zimenikataa! Nilijaribu twice Southern Sun lakini wapi!
Ubongo unaliwa bwana. Siku moja home wifi yangu alipika hio kitu na nlikuwa sipo. Nliporudi nkakuta vitu mezani, na huo ubongo umekaa kama mayai yalikaangwa (crumble ) nikajua ni mayai, lohhh kula mwanangu haviliki. Kuuliza ndo naambiwa ubongo wa ng'ombe. Uroho uliniisha
Hahahahahaha lol! Mie ningeambiwa ni ubongo wa ng'ombe nisingegusa Kha! kuna vingine vinahitaji moyo kuvitia kinywani hiki ni kimojawapo.
Umenichekesha bibi weye siku nimealikwa mahali nkaona ndizi mbichi bibi nkaanza kula naona ipo inagandaganda heee kumbe makopa nliacha nkaenda kutema ila nliumwa tumbo siku hiyo sitasahau