Supu Special Thread: Jifunze jinsi ya kupika aina mbalimbali za supu ya nyama na mboga mboga

Supu Special Thread: Jifunze jinsi ya kupika aina mbalimbali za supu ya nyama na mboga mboga

Ubongo unaliwa bwana. Siku moja home wifi yangu alipika hio kitu na nlikuwa sipo. Nliporudi nkakuta vitu mezani, na huo ubongo umekaa kama mayai yalikaangwa (crumble ) nikajua ni mayai, lohhh kula mwanangu haviliki. Kuuliza ndo naambiwa ubongo wa ng'ombe. Uroho uliniisha
[emoji23] [emoji23] [emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jinsi ya kupika supu ya pweza

supu+ya+pweza.jpg


Mahitaji

  • 1 Samaki pweza mkate na msafishe vizuri
  • 50 gram kitunguu swaumu
  • 100 gram kitunguu maji chop chop
  • 100 gram kariti kata vipande vidogo
  • 1 pilipili ya kijani fresh
  • 1 kijiko kidogo cha chai unga wa korienda au girigilani
  • Chumvi
  • 5 gram pilipili manga
  • 100 ml mafuta ya kupikia
  • 50 ml juisi ya Limao
  • 150 gram nyanya ya kopo
  • 1.5 lita ya Maji

Jinsi ya kupika

  1. Weka mafuta katika sufuria kisha kaanga kitunguu maji na kitunguu swaumu.
  2. Baada ya hapo weka pweza kaanga kwa dakika 10 kisha weka viungo vyote vilivyobakia kaanga kidogo.
  3. Weka maji chemsha katika moto wa wastani kwa dakika 15 na baada ya hapo itakua imeiva na tayari kwa kuliwa.
Sijawahi kunywa supu yake
Lkn pweza nampenda na pilipili na ndimu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom