Supu Special Thread: Jifunze jinsi ya kupika aina mbalimbali za supu ya nyama na mboga mboga

Ulimi wa ng'ombe!!! Unasafishwaje kwanza...tupe ujuzi mkuu ili hata ukiwa haukutengezwa vizuri tujue

rahisi sana una chemsha maji yakichemka unatumbukiza huo ulimi bunasubiri kama dk 5 unatoa afu unaukwangua ngozi ya juu kwa kisu hadi lile gozi jeupe ulione ukimaliza mwisho wa ulimi kwenye ncha unakata..
 
Hii kitu mimi huwa ndo inanishinda kabisa, awe amekaangwa, amechemshwa, amechomwa, kaungwa n.k mimi huwa ananishinda.
Nimejaribu mara nyingi ila wapiii!!!!

Ladha yake au muonekano?
 
Mi ulimi wa ng'ombe sijawahi kula nahisi km disgusting. Hata ubongo, korongo, kichwa vyote hivo havipandi abadan
 

This must be yummy.
 
Nimeona kumbe kila mtu ana kitu asichokipenda..

Mimi hapo kwenye pweza aisee nimejitahidi kuwapenda ila nimeshindwa!!! Nimekula kila mahali, nimejaribu waliochemshwa, waliokangwa n.k n.k vyote havipandi...yaani siku nikila pweza kesho yake siendi kazini naumwa tumbo balaa mpaka nachomwa sindano!!

Siku hizi hata nikipita tu pale ferry nikiwaona napatwa kichefuchefu kabisa yani!
 
Duhh!!! Hivi kumbe kuna watu wanakula ubongo? Makubwa!!!

Ubongo unaliwa bwana. Siku moja home wifi yangu alipika hio kitu na nlikuwa sipo. Nliporudi nkakuta vitu mezani, na huo ubongo umekaa kama mayai yalikaangwa (crumble ) nikajua ni mayai, lohhh kula mwanangu haviliki. Kuuliza ndo naambiwa ubongo wa ng'ombe. Uroho uliniisha
 

Hee!! Pole. Au unanunua magengeni labda ndio tumbo likakuuma??
 
Hee!! Pole. Au unanunua magengeni labda ndio tumbo likakuuma??

hata kwa hoteli nilishajaribu...actually sea foods zimenikataa! Nilijaribu twice Southern Sun lakini wapi!
 

Ha ha haaaa!!! Umenifanya nicheke sana aisee. Ama kweli sio kila chakula unachokiona kinachovutia machoni chafaa kuliwa.
 

Umenichekesha bibi weye siku nimealikwa mahali nkaona ndizi mbichi bibi nkaanza kula naona ipo inagandaganda heee kumbe makopa nliacha nkaenda kutema ila nliumwa tumbo siku hiyo sitasahau
 
Hahahahahaha lol! Mie ningeambiwa ni ubongo wa ng'ombe nisingegusa Kha! kuna vingine vinahitaji moyo kuvitia kinywani hiki ni kimojawapo.

 
Hahahahahaha lol! Mie ningeambiwa ni ubongo wa ng'ombe nisingegusa Kha! kuna vingine vinahitaji moyo kuvitia kinywani hiki ni kimojawapo.

We acha tu. Mi mavyakula ya ajabu ajabu siyawezi. Hadi leo hii sikuwahi kula miguu wala vichwa vya kuku, wala ki K.

Halafu utakuta mtu anaweka special order sokoni. Unajua kuwa hadi mapu.bu ya ng'ombe watu wanakula best?
 
Reactions: BAK
Umenichekesha bibi weye siku nimealikwa mahali nkaona ndizi mbichi bibi nkaanza kula naona ipo inagandaganda heee kumbe makopa nliacha nkaenda kutema ila nliumwa tumbo siku hiyo sitasahau

Ha ha haaaa. Inabidi makopa huyawezi?

Msambwija Jee?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…