Hicho unachokiita contradictions kinaelezeka endapo ukiwa na upande, wewe huna upande.
Sasa utasema hivi baadae utasema vile.
Mtu anaesema Mungu hayupo huyo huyo anauliza why Mungu alifanya hivi na vile.
Binafsi uwa sina pumzi ya kujadiliana na watu wa Karba yako.
Jaribu kuwa na upande mmoja ili hizo unazoziita contradictions zitatulike.
Wewe huelewi immanent critique ni nini.
Immanent critique, ni njia ya kuonesha mapungufu ya hoja, si kwa kuipinga moja kwa moja, bali kwa kuanza kama unakubaliana nayo, halafu kuonesha mapungufu ya hoja. Kuonesha contradictions za hiyo hoja.
Mathalan, wewe una miaka 30 leo.
Unaniambia mama yako mzazi ni binti mchanga ana miezi 6 leo.
Mimi najua hili jambo haliwezekani.
Lakini, nataka kukuonesha hilo polepole.
Nasema, nianze kama nakubaliana nawe, tuseme huyo binti mchanga wa miezi sita ni mama yako mzazi.
Halafu nakuuliza, ikiwa huyo binti wa miezi sita ni mama yako mzazi kweli, na yeye amezaliwa mwaka 2021, na wewe una miaka 30, kwa hiyo umezaliwa mwaka 1992, huyo mama yako mzazi alikuzaaje mwaka 1992 wakati alikuwa hqjazaliwa mpaka mwaka 2021?
Nakuonesha, kwa contradiction, kwamba huyo mama yako mzazi aliyezaliwa mwaka 2021 wakati wewe umezaliwa mwaka 1992 hayupo, ni wazo lako tu. Mama yako ni mwingine.
Sasa, tatizo lako, mimi nikianza kufanya hii immanent critique kwa kusema "tuseme huyo binti ni mama yako mzazi" nakuchanganya.
Kwa sababu una tatizo kwenye kufikiri kidhahania na kimantiki.
Huwezi kufuatilia mantiki ya immanent critique.
Ukiona mtu anafanya immanent critique, unafikiri hana upande.