Sura ya Mungu kupitia Wajapani

Sura ya Mungu kupitia Wajapani

Ukitaja kitu chochote,ukisema kwa mfano Akili,akili hatuioni lakini tunasema ipo.Tukisema Kira.nga.u,hana akili,ni kuwa akili ipo,lakini ni yeye Kira.nga.u ndio hana akili,lakini ipo akili.
Na ni vile vile ,Kira.nga.u akisema hakuna Mungu,ni kuwa Kira.nga.u,hamjui Mungu,lakini Mungu Yupo.Kira.nga.u kutomjua Mungu,hakufanyi Mungu kutokuwepo.
Na ndio hivyo hivyo,na ndivyo ilivyo,kwa kutokuwa na akili Kira.nga.u,hakufanyi kuwa akili haipo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mara nyingi kuangalia mazingira tu kunapotosha.

Mathalani.

Mtu anaweza kukaa kibarazani kwake, akaangalia ardhi, akajua dunia ni bapa.

Kumbe dunia ni tufe.

Mtu anaweza kuangalia angani, jua linachomoza , linazama, akafikiri jua linaizunguka dunia.

Kumbe dunia ndiyo inalizunguka jua.

Kama vitu vilivyo complex vinahitaji akili kubwa zaidi kuviumba viwepo, hoja hii inathibitisha haiwezekani awepo Mungu muumba vyote. Kwa sababu na yeye atakuwa complex na atahitaji muumba wake, na muumba wake atahitaji muumba wake, ad infinitum, ad nauseam.

Kwa hivyo, hoja yako ya kwanza nimekuonesha hatari ya kutafuta majibu ya maswali makubwa kwa njia nyepesi nyepesi tu. Unaweza kupotoka kirahisi. Inatubidi tujifunze sana, ukweli mara nyingine uko counterintuitive. Unaona dunia bapa, wakati ni tufe. Unaona jua linazunguka dunia, kumbe dunia ndiyo inqzunguka jua.

Scale yetu kwenye universe haitupi uwezo wa kuona na kujua mengi, inabidi tuchunguze kwa kina kabla ya kujiridhisha.

Hoja yako ya pili, also in a counterintuitive way, inatuthibitishia Mungu muumba vyote hawezi kuwapo.
Kukaa kibarazani nakuangalia ardhi nakujua kuwa dunia ni bapa kumbe ni tufe kunaondoa vipi uwepo wa dunia kuwako licha ya uwepo wake unakuwa nitofauti na vile unavyoonekana? Ni sawa nakusema kabla ya kuja kwa mitume/manabii kuna watu walikuwa wa kiabudu masanamu kama Miungu yao ila ziliposhuka hoja juu yao kuhusu Mungu imani yao yakuabudu ilibadilika kutoka kuabudu Masanamu mpaka kumuabudu Mungu mmoja asiyehitaji kutengenezwa na yoyote ili kuhitaji uweko kwake. Hivyo imani juu Mungu ilibadilika bila ya kuondosha uweko wa Mungu.

Tukiendelea mfano kuweko kwa Google kunategemea Internet, na kuweko kwa Internet kunategemea computer au simu, na ili computer na simu ziwepo kunategemea umeme/binadamu kuzitengeneza, mlongo huu unaweza kuendelea, ila hatuwezi kuwa na infinity regress of dependent thing, we require a place where it all stop and make sense which is the independent, self-sufficient, necessary being ambaye ni Mungu.
 
Kutokumjua Mungu,hakusaidii,kufanya Mungu asiwepo.Kwasababu huko kutajwa,na wanaosema Mungu,hayupo,ni baada ya kujua yupo,ndio wakasema hayupo.
Na hao,wanaosema Mungu hayupo,wanamtaja Mungu,ndio wakasema hayupo,ni uthibitisho tosha,wenye kujitosheleza,kuwa wamejua yupo Mungu,ndipo wakasema hayupo.

Kama kutaja Mungu hayupo maana yake yupo, basi vilevile kutaja Mungu yupo maana yake hayupo. Nonsense.

Thibitisha Mungu yupo.
 
Kwanini hitimisho liwe hakuna Mungu? Au ni kwa sababu haonekani kwa maana hakuna uthibitisho?
Kwasababu ya contradiction

Ni kama ambavyo aliyekuambia kuna invisible tea pot inayo orbit katikati ya jua isiyopimika kwa kipimo chochote

Ukamkatalia kuwa tea pot ya namna hiyi haipo kutokana na contradiction inayoonesha haiwezekani kisichoonekana wala kupimika kwa kipimo chochote halafu kitu hicho kimeweza kujulikana kiki orbit jua

Unafikiri swali lake la kusema kwanini hitimisho liwe hakuna invisible tea pot litakuwa na mantiki yeyote?
 
Nimeuliza kwanini hitimisho liwe hakuna Mungu kwenye hiyo contradiction?
 
Toa mfano wa wengi,waliobadili mawazo kwa kilichokuwepo,wakasema hakipo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Greeks ancient gods were banned

Hakuna anaye worship hiyo miungu

Vitu vingi viliaminiwa kimakosa na baadaye ukweli ulipojulikana imani hiyo ikatoweka

Wapo walioamini radi ni hasira ya mungu aitwaye Zeus lakini saizi kila mtu anajua kuwa ni msuguano wa mawingu unaosababisha radi na sio Zeus tena, hiyo dhana ndio ilipofikia ukomo hapo

Wapo watu walioamini jambo la uwongo kwa kuangalia personal experience asubuhi wanapoona jua linachomoza mashariki na kuonekana likizama magharibi wakajua pale ni jua linatembea

Wote hao wahakuwa disproved na hakuna mwenye imani hiyo (japo kuna wajinga wachache hawakosekani)

Kwa hiyo kitu fulani kudaiwa kuwa kipo au imani juu ya jambo fulani haina msaada wowote wa kufanya jambo hilo liwe kama ambavyo linachukuliwa na jamii hiyo inayokubaliana na jambo hilo
 
Nimeuliza kwanini hitimisho liwe hakuna Mungu kwenye hiyo hitimisho?
Nimekujibu ni kwasababu ya contradiction inayoonesha jambo hilo halipo

Invisible tea pot ambayo ni undetectable na kipimo chochote ukiambiwa chupa hiyo ya chai inazunguka jua huko anga za juu

Kauli hiyo itakuwa na contradiction au haina?
 
.
Screenshot_20220412-035224.jpg
 
Nimekujibu ni kwasababu ya contradiction inayoonesha jambo hilo halipo

Invisible tea pot ambayo ni undetectable na kipimo chochote ukiambiwa chupa hiyo ya chai inazunguka jua huko anga za juu

Kauli hiyo itakuwa na contradiction au haina?
Jambo lipi halipo? Ni kwamba contradiction inaonesha kuwa huyo Mungu hajaumba huu ulimwengu kama inavyodaiwa au hana hizo sifa za upendo wote na ujuzi wote kama inavyosemwa?
 
Jambo lipi halipo? Ni kwamba contradiction inaonesha kuwa huyo Mungu hajaumba huu ulimwengu kama inavyodaiwa au hana hizo sifa za upendo wote na ujuzi wote kama inavyosemwa?
Ukisema Mungu hana sifa hizo utarudi pale pale kuwa yule ambaye amesemwa ana sifa hizo hayupo

Kwa tafsiri hiyo hata beyonce ambaye hana uwezo wote na ujuzi wote na upendo wote atafit kwenye hiyo position

Hata ng'ombe anayeabudiwa na dini za kihindu ata fit as long as zile sifa za ukuu zitakuwa excluded
 
And the worst part about them ni kwamba,Wajapani hawana DINI...
Shinto, Buddhism, and Confucianism hizi ni baadhi ya dini za wajapan , naamini Mungu yupo Ila uwepo wa madhehebu unamwasilisha Mungu isivyo , Madhehebu ni uongo mtupu na hakuna mtu atahukumiwa Kwa kutofata taratibu za madhehebu ambayo yapo kuneemesha watu wanaojiita wachungaji
 
Ukisema Mungu hana sifa hizo utarudi pale pale kuwa yule ambaye amesemwa ana sifa hizo hayupo

Kwa tafsiri hiyo hata beyonce ambaye hana uwezo wote na ujuzi wote na upendo wote atafit kwenye hiyo position

Hata ng'ombe anayeabudiwa na dini za kihindu ata fit as long as zile sifa za ukuu zitakuwa excluded
Hapana, yani mimi nikisema kwamba Scars ni mtoto wa kiume pekee kwenye familia yao ila pia Scars ni mama wa watoto wawili, hapo nitakuwa nimetoa maelezo yenye contradiction kumuhusu Scars na hivyo hizo sifa nilizoeleza kumhusu yeye(kwamba ni mwanaume na ni mama mwenye watoto) haziwezi zote kuwa za kweli ila haifanyi kuwa Scars ambaye ndio mkusudiwa hayupo.
 
Kwanza tengua huo mfano wako ambao umeuweka kwa ridiculous
 
Back
Top Bottom