Unaweza kuthibitisha huyo Mungu yupo, ukiondoka kwenye maelezo matupu ya siyo na uthibitisho?
Maana kama ni kupiga hadithi tu, hata mimi naweza kukuambia kwamba kuna pembetatu ambayo hapo hapo ni duara.
Naweza kukuambia mimi ndiye Mungu, wewe huwezi kujua tu.
Je, hilo linanifanya niwe Mungu?
Pembetatu duara itakuwepo?
Mimi kusema hivyo hakufanyi pembetatu hiyo iwepo.
Au naweza kusema kuna mtu anaitwa Shokolokabangoshee ni balozi wa dunia nzima.
Wakati mtu huyo hayupo.
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote aliyeumba ulimwengu huu unaoruhusu mabaya hayupo, hoja ya kuwepo kwake inqjipinga yenyewe.
Na zaidi ya huyo, hujaweza kuthibitisha uwepo wa Mungu mwingine yeyote.