let the caged bird sings
JF-Expert Member
- Sep 19, 2020
- 3,699
- 8,857
- Thread starter
-
- #381
Na ilo ni moja ya sifa ya kuwafanya wawe more civilized kuliko Race nyingine.Hawana exposure na mambo yaliyo nje ya mipaka ya nchi yao!!
Sent from my Infinix X690B using JamiiForums mobile app
Acha upuuzi.Unaandika as if ni mtu mwenye ubongo wa nzi.Unauliza swali la kipumbavu ili kukwepa hoja makini.
#Be a great thinker.
Nashindwa kujua shida kwao ni Mungu ama shida ni contradiction!!😂Nimeuliza kwanini hitimisho liwe hakuna Mungu kwenye hiyo hitimisho?
Wanajichanganya.Nashindwa kujua shida kwao ni Mungu ama shida ni contradiction!!😂
Mungu ambaye dhana ya kuwepo kwake ina contradiction isiyoweza kutatulika hayupo, ni story tu.Nashindwa kujua shida kwao ni Mungu ama shida ni contradiction!![emoji23]
Dhana ya kuwepo kwake au dhana ya yeye kuumba huu ulimwengu? Hebu weka sawa hapo.Mungu ambaye dhana ya kuwepo kwake ina contradiction isiyoweza kutatulika hayupo, ni story tu.
Ukiruhusu contradiction, utaruhusu chochote.
Utaruhusu ulimwengu ambao hauna logic.
Na ulimwengu tunaouona una logic.
Dhana ya kuwepo kwake.Dhana ya kuwepo kwake au dhana ya yeye kuumba huu ulimwengu? Hebu weka sawa hapo.
Mbona unajichanganya? unazungumzia dhana ya uwepo wa Mungu au Mungu kuumba huu ulimwengu?Dhana ya kuwepo kwake.
Hata kabla hajaumba ulimwengu.
Unaambiwa Mungu hatakiwi kuumba ulimwengu unaoruhusu mabaya, kimantiki. Kabla ulimwengu haujaumbwa.
Halafu anaumba ulimwengu unaoruhusu mabaya.
Hii ni contradiction inayoonesha huyo Mungu katungwa tu, hayupo.
Dhana ya uwepo wa Mungu, mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote haiwezi kutenganishwa na uwepo wa ulimwengu.Mbona unajichanganya? unazungumzia dhana ya uwepo wa Mungu au Mungu kuumba huu ulimwengu?
Maana hivyo ni vitu viwili naona unavichanganya.
Hatutenganishi uwepo wa ulimwengu na Mungu hapa bali tunazungumzia contradiction kwenye suala la dhana ya Mungu kuumba huu ulimwengu, na contradiction inaishia kutuonesha tu kwamba hilo jambo si sahihi kwa maana ni suala ambalo haliwezekani.Dhana ya uwepo wa Mungu, mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote haiwezi kutenganishwa na uwepo wa ulimwengu.
Kutenganisha uwepo wa ulimwengu na uwepo wa Mungu huyo ni kusema Mungu huyo hana uwezo wote, ulimwengu umeweza kutokea bila yeye kujua au kutaka.
Jambo ambalo lina contradict sifa yake ya uwezo wote.
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.
Kwa sababu kuna ulimwengu, unaoruhusu mabaya, unaoonesha hayupo.
Angekuwepo, ulimwengu huu usingekuwepo.
Kuwa na mtazamo kwamba Mungu yupo, ikiwa hayupo, hakumfanyi awepo.Hatutenganishi uwepo wa ulimwengu na Mungu hapa bali tunazungumzia contradiction kwenye suala la dhana ya Mungu kuumba huu ulimwengu, na contradiction inaishia kutuonesha tu kwamba hilo jambo si sahihi kwa maana ni suala ambalo haliwezekani.
Sasa hoja ya kwamba huyo Mungu hayupo ndio maana kuna hiyo contradiction huo ni mtazamo wako na mwengine anaweza kuwa na mtazamo tofauti kuhusiana na hiyo contradiction.
Nimekwambia kwamba wewe kusema kuwa Mungu hayupo kwa sababu ya hiyo contradiction huo ni mtazamo wako binafsi na si uthibitisho ndio maana nikasema mtu mwengine pia anaweza akawa na mtazamo tofauti.Kuwa na mtazamo kwamba Mungu yupo, ikiwa hayupo, hakumfanyi awepo.
Vilevile, kuwa na mtazamo kwamba Mungu hayupo, wakati yupo, hakumfanyi asiwepo.
Hivyo, mtazamo si kitu muhimu. Kwa sababu hautuambii chochote definitively.
Kitu kinachotuambia kwa uhakika si mtazamo, ni uthibitisho.
Unaweza kuthibitisha kwamba Mungu yupo?
Unaweza kutueleza imekuwaje Mungu anayesemwa kuwa ni mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, kaumba ulimwengu ambao mabaya yanaweza kutokea, wakati alikuwa na uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?
Kwanza kabisa, kusema Mungu hayupo kwa sababu ya contradiction iliyopo katika hoja ya kuwepo kwake, si mtazamo wangu binafsi.Nimekwambia kwamba wewe kusema kuwa Mungu hayupo kwa sababu ya hiyo contradiction huo ni mtazamo wako binafsi na si uthibitisho ndio maana nikasema mtu mwengine pia anaweza akawa na mtazamo tofauti.
Contradiction inaishia tu kutuonesha ya kwamba hilo jambo(Mungu kuumba huu ulimwengu) haliwezekani na hivyo si sahihi, ila ukija kutuambia kwamba hiyo contradiction inatokana na kwamba huyo Mungu kuwa hayupo hapo ndipo inapokuwa ni mtazamo wako tu na mwengine anawezakuwa na mtazamo tofauti kuhusiana na sababu ya hiyo contradiction.
Mungu ambaye dhana ya kuwepo kwake ina contradiction isiyoweza kutatulika hayupo, ni story tu.
Ukiruhusu contradiction, utaruhusu chochote.
Utaruhusu ulimwengu ambao hauna logic.
Na ulimwengu tunaouona una logic.
Haijalishi ni akina nani wana huo mtazamo point ni kwamba hawana uthibitisho hivyo ni mtazamo tu binafsi tofauti na uthibitisho.Kwanza kabisa, kusema Mungu hayupo kwa sababu ya contradiction iliyopo katika hoja ya kuwepo kwake, si mtazamo wangu binafsi.
Ni jambo lililosemwa na kuandikwa na wanafalsafa mamia ya miaka kabla sijazaliwa.
Ni wewe tu hujasoma.
Na hilo ni tatizo kubwa.
Hujasoma the basic texts on the matter.
Ungesoma, usingesema haya ni mawazo yangu binafsi.
Hicho unachokiita contradictions kinaelezeka endapo ukiwa na upande, wewe huna upande.
Sasa utasema hivi baadae utasema vile.
Mtu anaesema Mungu hayupo huyo huyo anauliza why Mungu alifanya hivi na vile.
Binafsi uwa sina pumzi ya kujadiliana na watu wa Karba yako.
Jaribu kuwa na upande mmoja ili hizo unazoziita contradictions zitatulike.
Uthibitisho gani wa kuonesha Mungu hayupo unaweza kuukubali kwamba unatosheleza na si mtazamo binafsi?Haijalishi ni akina nani wana huo mtazamo point ni kwamba hawana uthibitisho hivyo ni mtazamo tu binafsi tofauti na uthibitisho.
Huo unabaki tu kuwa ni mtazamo kama uliikuta na kuamua kuufuata basi pia tambua kuwa wengine wana mitazamo tofauti na huo.
Kwanza tuwekane sawa, hoja yangu inaanzia kwenye kupinga madai ya kwamba hiyo contradiction(Mungu kuumba huu ulimwengu) ndio inahitimisha au ndio uthibitisho kuwa hakuna Mungu.Uthibitisho gani wa kuonesha Mungu hayupo unaweza kuukubali kwamba unatosheleza na si mtazamo binafsi?
Na mtu akikwambia habari ya kuwepo Mungu si kweli, kwanza haijathibitishwa, utawathibitishiaje Mungu yupo kweli na si hadithi za watu tu?
And the worst part about them ni kwamba,Wajapani hawana DINI...