Surveyormunkondya sasa nipo jamiiforum kwa ajili ya elimu juu ya masuala ya ardhi

Surveyormunkondya sasa nipo jamiiforum kwa ajili ya elimu juu ya masuala ya ardhi

Joined
Feb 8, 2019
Posts
94
Reaction score
124
Ahsante sana ndugu zangu kwa kuniomba nijiunge jamiiforum ili pia niweze kuendelea kutoa elimu juu ya masuala mbali mbali ya ardhi.

Na sasa nimejiunga rasmi na jukwaa hili kwa ajili ya kuendelea kuwaelimisha watanzania wenzangu ili kuepukana na matatizo mbali mbali ya ardhi kama;

-kununua eneo lisilo sahihi
-kujenga eneo lisilo sahihi
-kupata hati miliki isio sahihi
-kubomolewa nyumba
-kutopewa fidia stahiki
-kudhurumiwa ardhi na masuala mengi zaidi

Kwa wale wote watakao taka kujiunga na baadhi ya magroup yangu ya whatsapp unaweza kuniandikia namba yako hapo chini..
Ahsante sana
Surveyormunkondya(mpima ardhi)
0765532858
Screenshot_20190408-140658_Facebook.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunashukuru kwa ujio wako humu, Swali: mimi nina eneo langu lenye ekari kama 5 hivi, je naweza kuligawa viwanja kwa kutumia GPRS bila ya kuwashirikisha watu ardhi? eneo lipo kijijini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mimi natakaka kujua umbali wa kutoka kwenye nyaya za umeme wa masafa mpaka kwenye nyumba huwa ni mita ngapi?
 
Karibu ndg nadhani ni vizuri tukaelimishana humu mambo ya magroup ya whatsapp wengine hatuwezi mie nitauliza humu na nijibiwe humu JF

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunashukuru kwa ujio wako humu, Swali: mimi nina eneo langu lenye ekari kama 5 hivi, je naweza kuligawa viwanja kwa kutumia GPRS bila ya kuwashirikisha watu ardhi? eneo lipo kijijini.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio unaweza kuligawa lakini usipo washirikisha watu wa ardhi kama manispaa au wizara ya ardhi basi eneo lako halitatambulika katika database ya taasisi za serikali....

Lakini pia ni vema ningejua dhamira ya wewe kugawa viwanja katika eneo lako..?
Kwa sababu kugawa viwanja katika shamba ndo upimaji....

Na upimaji lazima uidhinishwe na kupitishwa na taasisi za serikali kama manispa na wizara ya ardhi...
Hivyo basi lengo lako la kutaka kugawa eneo lako la ekari 5 bila kushirikisha taasisi za ardhi utakuwa sio upimaji.....

Ahsante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nitatambuaje kwamba kiwanja flani ni "dhaifu"?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kabla hujanunua kiwanja au kufanya uendelezaji wowote hakikisha uhalali wa eneo husika katika mamlaka husika kama halmashauri au wizara ya ardhi kupitia wewe mwenyewe au surveyor(mpima ardhi),ambapo data au vipimo vya awali ambavyo huchukuliwa kwa handed gps(kifaa ya upimaji) na kupelekwa wizarani kuangalia matumizi sahihi ya eneo husika kama ni eneo la makazi, barabara,shule,hospitali au eneo la wazi yote hayo atayajua kupitia wizara ya ardhi au manispaa..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunashukuru kwa ujio wako humu, Swali: mimi nina eneo langu lenye ekari kama 5 hivi, je naweza kuligawa viwanja kwa kutumia GPRS bila ya kuwashirikisha watu ardhi? eneo lipo kijijini.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio unaweza kuligawa lakini usipo washirikisha watu wa ardhi kama manispaa au wizara ya ardhi basi eneo lako halitatambulika katika database ya taasisi za serikali....
Lakini pia ni vema ningejua dhamira ya wewe kugawa viwanja katika eneo lako..?
Kwa sababu kugawa viwanja katika shamba ndo upimaji....
Na upimaji lazima uidhinishwe na kupitishwa na taasisi za serikali kama manispa na wizara ya ardhi...
Hivyo basi lengo lako la kutaka kugawa eneo lako la ekari 5 bila kushirikisha taasisi za ardhi utakuwa sio upimaji.....

Ahsante

Sent using Jamii Forums mobile app
Haiwezekani kugawa kiwanja kwa GPRS acheni kupotoshana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haiwezekani kugawa kiwanja kwa GPRS acheni kupotoshana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Boss nimeassume anamaanisha GPS receiver na sio GPRS(general packet radio service) kwa sababu GPRS ni kuhusu mambo mtandao wa simu 2G au 3G na havihusiani na ardhi..
Hivyo nimemjibu nikiamini anamaanisha GPR receiver kwa sababu ndo kifaa hutuka kwenye mambo ya upimaji wa ardhi...
Ahsante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
So uchaguzi wa Serikali za Mitaa u karibu[emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
Bado si rafiki!
Kuna maeneo kiwanja kinauzwa kuanzia 150,000.
Being inapaswa kuendana na gharama za kiwanja eneo husika, ikiwa kama lengo ni kuhasisha watu wengi wapime.
Ikumbukwe, watu wengi (hasa vijijini) wana maeneo ambayo yakipimwa yanatoa viwanja vingi.
Kwa mfano, eneo likitoa viwanja 4, mmiliki atapaswa kulipia 600,000/-. Siamini kama wengi 'watajipendekeza'.
 
Leo waziri wa ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi Mh.lukuvi alikuwa na kikao cha pamoja na makampuni ya upimaji. Kwa pamoja wamekubaliana kuwa gharama za urasimishaji zitakuwa si zaidi ya laki na nusu(150000) kutoka laki mbili na nusu(250000) hapo awali....
View attachment 1074324

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hilii serikali inahitaji pongezi maana ukitazama mji kama dsm ni ni ishara tosha ya kushindwa kupanga huu mji ambao kijiographia ulipaswa uwe mji mmoja mzuri sanaaa yaan kama ungepangwa ....ukitazama mji kama nairobi umepangwa vizuri atleast hope dodoma kwa hili litazibitiwa
 
Wala tatizo haliko kwa wapimaji .labda kwa wasio jua iko hiv, mpimaji kazi yake ni kusurvey eneo.kazi ya kurasimisha ili upate hati iko kwa serikali kuanzia kwa ofisi za ardhi katka halmashauri.hao watatakiwa kupitisha michoro na process zingine .hapa ndiyo shiida huanza .hapa kimsingi ndiyo kwenye gharama zaidi.watakupiga hela na watakuzungusha vile vile.hapo mimi nawaonaga hao maofisa ardhi wana nguvu sana ya kukwamisha mchakato kuliko waziri wa ardhi mwenyewe

Mfano sis hapa Dar maeneo ya Pugu kajiungeni tulijikusanya watu zaidi ya 100 tukaanza mchakato wa upimaji toka 2013 tulilipia gharama zote.Tulimalizana vizuri na mpima na ofisa wa ardhi alikuja kuhakiki maeneo yetu yakawa poa pia nyaraka zote mhimu zilikuwa zimeambatanishwa kwenye fomu zetu kama utaratibu unavyotaka. Tunasikia mafaili yetu yamekwamishwa na na ofisa mmoja anaitwa Mbembera hapo manispaa ya Ilala ofisi ya ardhi mpaka leo.ukifuatilia utaambiwa nenda kwa huyu mara kwa yule mpaka sasa tumechoka hatuelewi tufanyeje.

Sasa hivi viwanja zaidi ya 100 ,halimashauri imekosa mapato yale ya urasimishaji.maana si.kuna zile.gharana za umiriki.zinazolipwa kwa .halmasahuri kulingana na ukubwa wa kiwanja chako hatujapewa kadirio ili tukalipie.Lakini pia serikali imekosa mapato kutoka kodi ya viwanja kuanzia 2013.

So hili la waziri kushusha bei ya upimaji silioni kama linaweza harakisha chochote.labda watazame upya mfumo mzima wa mchakato wa urasimishaji ardhi.kuna watu kwenye hizi halmashauri wananufaika sana na huu mfumo kuliko wananchi wenyewe
 
Back
Top Bottom