Surveyormunkondya sasa nipo jamiiforum kwa ajili ya elimu juu ya masuala ya ardhi

Surveyormunkondya sasa nipo jamiiforum kwa ajili ya elimu juu ya masuala ya ardhi

Point, sheria ya NOTARY PUBLIC AND COMMISSION ER FOR AOTH, imetoa mamlaka hayo Kwa WAKILI, ikisomwa pamoja na sheria ya mawakili inazuia mawakili ndiyo wanaoruhusiw kudraft documents za mauziano ni mawakili tu,
pia lukuvi alishasema kununua ardhi kwa wenyekiti ni sawa na kununua bomu muda wote linaweza kulipuka sababu moja wapo mihuri ya wenyekiti haina kibali cha kutumika kwenye mauziano ya ardhi hivyo ni sawa haujanunua kitu, hilo hilo eneo akitokea mwingine amenunua kwa mkataba wakili ujue bomu limeshalipuka
 
ADVOCATE ACT imetoa mamlaka hayo kwa mawakili kudraft contract pia imetoa adhabu kwa mtu yoyote ambaye sio wakili akidraft contact ni kosa lenye adhabu ya faini ya shilingi milioni moja pamoja kifungo cha mwaka mmoja kama sijakosea au anakumbuna navyo vyote kwa pamoja.

"mwenyekiti wa serikali ya mitaa" kisheria anaitwa "unqualified person" sheria haiwaruhusu kudraft mikataba hawana huo ujuzi, kama lukuvi alivyosema ukienda kinyume ujue umenunua bomu ni sawa na kushirikiana kununua ya mali ya uwizi
Point, sheria ya NOTARY PUBLIC AND COMMISSION ER FOR AOTH, imetoa mamlaka hayo Kwa WAKILI, ikisomwa pamoja na sheria ya mawakili inazuia mawakili ndiyo wanaoruhusiw kudraft documents za mauziano ni mawakili tu,
 
HATUA ILI UWEZE KUPIMIWA KIWANJA AU SHAMBA LAKO PAMOJA NA BEI ZAKE NA JINSI YA KUPATA HATI MILIKI.

(hatua ya 1)
Ukaguzi wa eneo husika ili kujua eneo lako limepangwa kwa ajili ya matumizi gani, Hapa atashirikishwa mpima ardhi kwa ajili ya kufanya utambuzi wa eneo husika kujua lipo kwa ajili ya matumizi gani, Hivyo ni lazima mpima ardhi (surveyor)afike site kwako na kifaa (Handheld GPS), Achukue vipimo kuzunguka eneo lako, Baada ya hapo akatafute taarifa za eneo lako wizarani au halmashauri ili aweze kupata ramani ya mpango mji wa eneo lako.

Bei hutegemea na mkoa kwa sababu ya thamani ya ardhi lakini mara nyingi huwa kati ya laki na nusu hadi laki mbili(inaweza kuwa pungufu au zaidi ya hapo tokana na makubaliano kati ya mpima ardhi na mteja) na hiyo bei sio ya upimaji bali ni ya presurvey tu au kwa hiyo hatu ya kwanza.

MATOKEO YA HATUA YA KWANZA
Matokeo ya Hatua hii yanaweza kufanya eneo likapimwa au lisipimwe

■ sifa za eneo ambalo halipimiki

i) Eneo linaweza kukosa sifa za kupimika mara tu hakutakuwa na mchoro wa mpango mji ambao huonesha matumizi sahihi ya eneo husika( kama mtaa au eneo husika halija pangwa na halmshauri)

ii)pia eneo hukosa sifa za kupimwa kama eneo husika kuwa katika matumizi ya maeneo ya kijamii kama shule, makabuli, barabara, soko n.k

■ sifa za eneo ambalo linaweza kupimika

Eneo litapimwa mara tu linapokuwa katika matumizi sahihi ambayo mtu binafsi anaweza kumiliki mfano makazi, hotel, biashara n.k

hatua ya 2)
KIBALI CHA UPIMAJI.
kama tayari eneo lako lina sifa ya kupimika, basi taaratibu za upimaji huanza kwa kuomba kibali cha upimaji
Kibali cha upimaji huombwa na Mteja au mmiliki halali wa eneo husika inabidi aandae barua kwa ajili ya kuomba kupimiwa eneo lake, Barua hiyo itapita serikali ya mtaa na halmashauri husika.
( mara nyingi mpima ardhi humsaidia mteja mfano wa barua hiyo )

(hatua ya 3
Hatua hii huwa ni upimaji

Hapa ni suala la kitaaluma zaidi ambapo mtaalamu ataweka mipaka katika eneo lako kwa kutumia mawe (beacons), litaandaliwa file kwa ajili ya kwenda wizarani likiambatanishwa na ramani ya upimaji ambayo huchora na mpima ardhi. Baadaye utarudishiwa ramani iliyo hakikiwa toka wizarani kama ramani ya upimaji.
Hapa ndo kazi yenyewe ya mpima ardhi na vifaa vyake na mara nyingi mteja huwa hausiki cha chochote labda kuwepo tu site kama mmiliki wa ardhi

hatua ya 4
Mteja utakabiziwa ramani ya upimaji.
Baada ya upimaji na kuchora ramani ambayo imepelekwa wizarani na kukubaliwa na kurugenzi wa upimaji na ramani katika wizara ya ardhi na makazi,mteja hupewa ramani ambayo kimsingi ndo kazi nzima ya mpima ardhi inapo ishia na hiyo ramani ndo end-product ya upimaji.

ILIKUPATA HATI MILIKI
Baada ya kupewa ramani na mpima ardhi(surveyor) iliyokubalika wizarani basi mteja atatakiwa kupeleka kwa afisa ardhi wa halmashauri husika ili atengenezewe hati miliki na hatua hii mara nyingi mpima ardhi hausiki huwa ni mteja mwenyewe ila unaweza kumwomba akuelekeze hatua za kufuta ili upate hati miliki yako kama hujui hatua za kufata baada ya kupewa ramani yako

GHARAMA ZA UPIMAJI

Gharama za upimaji zinatokana na ukubwa wa kazi na mara nyingi iko hivi,kwa mteja mwenye viwanja vingi kuanzia 10 na kuendele na vipo kwenye block moja bei huwa ni kuanzia laki 2 na kuendelea.
Lakini kwa mwenye kiwanja kimoja au viwanja vingi ila vipo sehemu tofauti tofauti bei huwa ni laki 8,9,1m na kuendelea.lakini kama una eneo kubwa linaweza kutoa viwanja vingi mara nyingi unaweza kuongea na surveyor akagharamia shughuri zote za upimaji ila mkagawana viwanja mara nyingi njia hii hutumika na wenye maeneo makubwa sanaa(sio lazima ila hutumiwa na wenye maeneo makubwa)

NOTE(ZINGATIA)
WENGI HUJIULIZA

Kwa nini bei ya urasimishaji ni laki 2 hadi laki mbili nusu lakini upimaji wa kawaida ni kuanzia laki 8,9,1m na kuendelea..?

Iko hivi.
Kupima viwanja vingi vilivyofatana kwa bei ndogo kama laki mbili ni nafuu zaidi katika uendeshaji wa zoezi la upimaji kuliko kupima eneo moja ndo maana gharama yake iko juu zaidi kwasababu kama viwanja vipo 100 na vimefuatana basi gharama ya endeshaji upimaji utakuwa sawa na ule wa kiwanja kimoja hivyo ni bora kupima viwanja vingi kuliko kiwanja kimoja kwamujibu wa masurveyor au wapima ardhi.
Hivyo basi usiringanishe urasimishani wa makazi holela na upimaji wa maeneo yaliyopangwa tayari...

Note:
Bei hizo zote huweza kuwa chini zaidi au juu zaidi lakini hizo nilizo watajia ndo standard na wapima ardhi wengi hurange katika izo bei hivyo unaweza kujipanga kwa izo bei na kama ni kuongezeka huwa ni kidogo vile vile kama ni kupungua huwa ni kidogo hizo ndo kawaida kwa wapima wengi

Written By surveyormunkondya
Simu;0765532858
Whatsapp:0673540985
Email;munkondyathom@gmail.com
 
Huko nyuma wapimaji wamewaumiza sana wananchi waliotaka kupimiwa ardhi yao huku kukiwa na longolongo nyingi hadi kukatisha tamaa. Hata sasa bado wapo wapimaji wachache wanaoendekeza njaa kwa kuwataka wapimiwaji kulipia gharama kubwa. Ila kwa sasa wananchi wenyewe wakijipanga na kutaka kupimiwa maeneo yao kwa pamoja bei haitakiwi kuzidi 150,000/= kwa kila kiwanja.
 
Swali fupi: ukiwa na eneo lenye ukubwa wa ekari kumi na ukataka ulipime na uligawe ili kupata viwanja vyenye ukubwa wa square metres 1,200 kila kimoja ukitoa na nafasi ya barabara unaweza kubaki na viwanja vingapi vyenye ukubwa huo kwenye hizo ekari kumi?
 
Nina eka 4 dodoma sehemu mmoja ila havijaungana...

Utanipimia kwa sh ngapi? Na hati nitapata kwa sh ngapi
 
Huko nyuma wapimaji wamewaumiza sana wananchi waliotaka kupimiwa ardhi yao huku kukiwa na longolongo nyingi hadi kukatisha tamaa. Hata sasa bado wapo wapimaji wachache wanaoendekeza njaa kwa kuwataka wapimiwaji kulipia gharama kubwa. Ila kwa sasa wananchi wenyewe wakijipanga na kutaka kupimiwa maeneo yao kwa pamoja bei haitakiwi kuzidi 150,000/= kwa kila kiwanja.
Ndio mkuu sema hiyo bei ni kwa urasimishaji na shida kubwa ni kwamba bado wananchi wengi hawajui kutofautisha kati ya upimaji wa kawaida na urasimishaji..
Kwa sasa naandaa tofauti ya urasimishaji na upimaji wa kawaida ili wananchi waweze kuelewa
 
Ndio mkuu sema hiyo bei ni kwa urasimishaji na shida kubwa ni kwamba bado wananchi wengi hawajui kutofautisha kati ya upimaji wa kawaida na urasimishaji..
Kwa sasa naandaa tofauti ya urasimishaji na upimaji wa kawaida ili wananchi waweze kuelewa
Ahsante. Naomba jibu la post no. 3.
 
Mbona hawa wapimaji kwenye project ya urasimisaji hawatoi "ramani "...? Naona wanaishia kupanda mawe tu
 
Hili nalo ni shida ,ukisikia laki na nusu ukienda kutafuta Kibali bei siyo hiyo na usumbufu wa kutosha juu wana sababu hao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Laki na nusu in urasimishaji (upimaji wa viwanja vya watu wengi kwa wakati mmoja ) ila upimaji wa MTU mmoja no zaidi ya milioni mbili maana huyu MTU atabeba gharama zote za upimaji
 
Mbona wa wapimaji kwenye project ya urasimisaji hawatoi "ramani "...? Naona wanaishia kupanda mawe tu
Raman zinatolewa mkuu nenda ofisi ya upimaji na Raman ya harmashauri au manispaa uliyopo, wengi huwa tunafika mbali tunazigawa pia katika ofisi ya mtaa husika
 
Ina gharimu kiasi gani ku-renew hati ya kiwanja ya mwaka 1990!?.
 
Back
Top Bottom