Haki Miliki
Kuna aina za umiliki ardhi kama unavyotambuliwa na sheria za nchi uko wa aina mbili:-
(i) Haki miliki ya kiserikali (granted right of occupancy), na
(ii) Haki miliki ya kimila(customary right of occupancy).
Aina hizi za kumiliki ardhi sio ngeni kwani ndizo zilikuwa
zinatumika hata katika Sheria ya Ardhi ya zamani ambayo ilifutwa na kutungwa sheria za ardhi za mwaka 1999, isipokuwa
mabadiliko mawili makubwa yamejitokeza katika sheria hizi
mpya nayo ni:-
a. Katika sheria ya zamani hakimiliki ya kisheria ilihusisha kupewa hati inayotolewa na Kamishna wa Ardhi, wakati
hakimiliki ya kimila haikuhitaji hati. Hivi sasa utaratibu ushafanyika kuwezesha hata hakimiliki ya kimila kuwa na
hati inayotolewa na kijiji.
b. Katika sheria ya zamani, hakimiliki ya kimila ilidhaniwa tu (dhana ya umiliki) kuwa na hadhi sawa na hakimiliki ya
kisheria lakini kiutekelezaji hilo halikuwezekana kwani
hakimiliki ya kimila ilichukuliwa kama haki ya matumizi tu ya ardhi na haikubeba uzito kama ilivyo kwa hakimiliki ya
kiserikali. Kwa hiyo, ilipotokea mgogoro kati ya wamiliki wawili, mmoja akiwa na hatimiliki ya kiserikali na mwingine akiwa na hakimiliki ya kimila, basi hakimiliki ya kimila ilionekana kuwa haina nguvu na hivyo kutotambuliwa. Kwa hivi sasa haki miliki ya kimila ina hadhi sawa sawa na hakimiliki kiserikali. Hata hivyo itachukua muda mrefu
kwa watu kuzoea jambo hili.
Nani Anaweza Kumiliki Ardhi?
Mtu yeyote ambaye ni;
a. Mtanzania, mwanamme au mwanamke.
b. Kikundi cha watu ambao ni raia wa Tanzania walio katika
umoja wa kisheria au la, au ni wabia au washirika,wanaweza
kumiliki ardhi.
Ifahamike kwamba mtu ambaye sio raia wa Tanzania, au kikundi
cha watu au mtu ambaye ana shirika lenye hisa, ambao wengi
wa wanahisa wake sio Watanzania hawana haki ya moja kwa moja ya kumiliki ardhi nchini na kupewa hakimiliki ya ardhi isipokuwa tu kama watapewa ardhi hiyo kama wawekezaji wa mujibu wa Sheria ya Uwekezaji ya mwaka 1997.
Utaratibu wa Maombi ya Hati ya Hakimiliki ya Kiserikali
Itaendelea.....
By surveyorMunkondya(mpima ardhi)
Simu;0765532858
Whatsapp;0673540985