*Leo nitawaeleza namna ardhi inavyopatikana tanzania*
Kuna njia mkuu 5 za halali za namna watu wanavyo pata ardhi tanzania ambazo ni;
i)kutwa
ii)urithi
iii)kugawiwa na serikali
iv)kununua
V)upangishaji au kukodi
Upatikanaji wa Ardhi Tanzania
Upatikanaji wa ardhi Tanzania huwezeshwa kwa kupitia njia
kadhaa ambazo ni halali na zinazokubalika kisheria katika jamii.
Kwa ujumla mtu au taasisi anaweza kumiliki ardhi kwa ama kugawiwa, kurithishwa, kupewa, kutwaa au kununua. Sheria za Tanzania zinataja njia kadhaa ambazo mtu anaweza kupata
Ardhi nchini;
a. Kutwaa
Njia hii hutumika pale ambapo mtu huingia katika eneo
kama vile pori na kusafisha kisha kuliweka katika matumizi.
Njia hii ni kongwe sana hapa nchini. Pori linalosafishwa
linaweza kuwa ardhi ya kijiji, hifadhi au ya jumla. Ni ngumu
kutumia njia hii nyakati hizi, lakini bado inatumika katika
maeneo mengi ya Tanzania. Pale ambapo utatakiwa kufuata
taratibu kama vile kusajili utatakiwa kutii amri hiyo. Kama
utatakiwa kuhama eneo hilo basi mamlaka husika itatakiwa kulipa fidia ya maendelezo uliyoyafanya katika ardhi hiyo.
Hali kadhalika, mtu anaweza kutwaa ardhi kwa kuachwa
akae kwenye ardhi au nyumba ya mtu fulani kwa kipindi
kirefu kisichopungua miaka kumi na mbili (12) kama vile
yuko kwenye ardhi yake na kuweza kufanya kila atakavyo
bila kukumbushwa, kukemewa, kulipishwa kodi au bila
ya bughudha ya aina yeyote ya umiliki huhesabiwa kuwa
anamiliki ardhi ile kihalali. Hata hivyo, njia hii ya utwaaji
haiwezi kutumika dhidi ya ardhi inayomilikiwa na taasisi
ya serikali.
b.Urithi
Wewe kama mwanamke unaweza kupata ardhi kwa njia ya urithi. Mwanamke anaweza kurithi ardhi kutoka kwa mume
au wazazi wake kama kutakuwepo na wosia na mwanamke ametajwa katika wasio basi atakuwa na haki ya kurithi.
Kama hakutakuwa na wosia basi katika mgawanyo wa
mirathi mwanamke anayo haki ya kurithi ardhi pia. Jinsia
au tamaduni na mila haviwezi kuwa kigezo cha kumnyima
mwanamke haki hiyo ya kurithi ardhi. Mgao wowote
utakaomnyima haki hiyo kwa misingi ya jinsia au mila ni
batili na unaweza kuwafikisha wahusika mahakamani. Si tu mwanamke hata mwanaume pia.
Baada ya njia ya "urithi" kama njia moja wapo ya kupata ardhi tanzania kama nilivyo waeleza katika makala iliyopita sasa njia nyingine ni hizi hapa;
c. Kugawiwa na Serikali
Mtu anaweza kupata ardhi kwa kugawiwa na Serikali. Anaweza kuomba ardhi katika ardhi ya jumla au ya kijiji. Kamishina akiridhika kwamba umetimiza masharti atakugawia ardhi hiyo. Katika ardhi ya kijiji, serikali ya kijiji ndiyo yenye mamlaka ya kugawa ardhi. Mtu
akipeleka maombi ya ardhi serikali ya kijiji itayajadili na
kuyapeleka Mkutano Mkuu wa Kijiji kuyapitisha. Kama
maombi ni chini ya hekta 21 basi Halmashauri ya Kijiji
itamgawia ardhi hiyo.
d. Kununua
Hii pia ni njia mojawapo ambayo mtu unaweza
kuitumia kupata ardhi.Wakati mmiliki anapotaka kuuza
ardhi yake iwe ya kijiji, hifadhi au jumla, sheria inatoa ruhusa
ya kununua kama unaweza. Ugumu kwa wanawake walio
wengi kupata ardhi kwa njia hii ni uwezo wao mdogo wa
kiuchumi kuweza kumudu bei ya soko.lakini ni njia ambayo wengi hupata ardhi tanzania.
e. Upangishaji au kukodi
Upangishaji ni njia mojawapo ya kupata ardhi. Tofauti na njia nyingine za upatikanaji wa ardhi, upangishaji unakupatia haki pungufu na yule anayekupangisha.
Wanawake pia wanaweza kupata ardhi kwa kupangisha pia.
Hivyo basi watu wengi tanzania wana ardhi ya kutwa,ardhi ya kurithi,ardhi ya kugawiwa na serikali,ardhi ya kununua pamoja na ardhi ya kupangishiwa au kukodi.
*somo lijalo...
HAKI MILIKI
*itaendelea......*
By
Surveyor Munkondya (mpima ardhi)
Simu;0673540985
Whatsapp;0765532858