The Assassin
JF-Expert Member
- Oct 30, 2018
- 4,942
- 20,077
Hizi ni skills ambazo ni lazima mwanaume uwe nazo.
1. Mwanaume lazima ujue kupika. Kupika sio kazi ya wanawake wala sio gender role hii. Haya ni maarifa anayotakiwa kua nayo kila mtu.
Kuna watu waliamua kuoa tu kwa sababu wanataka mtu wa kuja kuwapikia. Maana yake kama wangekua wanajua kupika wasingeoa ama wangekua na maamuzi mengine.
2. Mwanaume lazima ujue kurekebisha vitu vidogo vidogo nyumbani. Mwanaume sio kila kitu unaita fundi, nyoka ikiingia ndani unakimbia nyumba ama unaita jirani.
Mwanaume lazima ujue ku fix vitu vidogo vidogo nyumbani inapotokea shida, sio sinki la maji la jikoni halipitishi maji unasubiri uite fundi, huu ni ujinga.
3. Mwanaume kama una gari ujue kupiga jeki na kubadilisha tairi, sio kila kitu upeleke kwa fundi. Hii inakusaidia siku moja uko mwenyewe na unapata pacha eneo ama wakati wa usiku usishindwe kuendelea na mishe zako kisa fundi hayupo.
4. Mwanaume ujue kuunganisha vifaa vya elektroniki nyumbani, mfano spika na tv, hdmi ama vga cables sio kila kitu umuite fundi.
5. Mwanaume ujue kumbadilisha mtoto nepi na kumuogesha, sio kila kitu unamuachia mama yake.
6. Mwanaume ujue kufua, sio kila kitu kinafuliwa kwenye mashine na kikatakata. Mfano boxers nk hizi unafua kwa mkono, hii haijalishi una mke ama huna. Ujue kufua.
7. Mwanaume usikose vitu basic kwenye tool boz yako kama bisibisi, spana za kufungulia ama kufunga vitu kama vitanda, viti ama meza nk. Sio kila kitu fundi.
8. Mwanaume usikose silaha yoyote ndani ya nyumba. Siraha kama panga, sime, upinde, Bastola nk ila uwe na silaha. Hii haijalishi unaishi Dar ama mkoani.
9. Ogezea za kwako.