Swali Butu: Mambo haya 4 Magufuli anayafanya tofauti na Marais 3 waliomtangulia! Nani anabisha?

Kushindwa kumuondoa makonda wakati wa makontena na kumuondoa CAG ilikuwa ni kipimo kwamba tuna Rais fisadi.
Uko sahihi Mkuu ukisha ona mtu hamtakiCAG muadilifu hataki tujue kinachoendelea bungeni ujue kuna shida.
 
Hivi mnasomaga wapi wenzetu? ukisikia "deni la taifa" unadhania ni nini?
Ila issue ya deni sio ya kuidharau sana. Najua ni dhana tofauti na kujitegemea lakini zinaweza kuhusianishwa. Maana hela tunazokopa tukishindwa kuzilipa kwa sababu moja ama nyingine kunakuwa na athari kwenye kujitegemea. Kumbuka wanaotukopesha wanatupa masharti (hasa kwa mikopo isiyo ya kibiashara). Kw asasa makusanyo yetu ya kodi bado hayawezi kukidhi recurrent expenditure (tunapanga kukusanya kodi sh 20, wakati matumizi yetu ya kawaida ni sh 22), achilia mbali matumizi katika miradi ya maendeleo.

Mojawapo ya mambo ambayo Mkapa anajivunia kufanya katika utawala wake ni kupunguza deni la taifa (kwa kulipa na mengine kuomba kusamehewa). In a way ni kama alikuwa anawalaumu Nyerere na Mwinyi kwa kumuachia madeni makubwa na nchi isiyokopesheka. Baada ya kupunguza madeni tukaanza "kukopesheka" tena. Kwa hivyo deni la taifa likiwa kubwa sana tutashindwa kukopesheka, na kama kodi tunayokusanya bado haitoshi tutalazimika kurudi kuwa ombaomba.....na kushindwa "kujitegemea" maana watakaokuwa wanatusaidia wataamua pakubwa kuhusu sera zetu.

All in all, napenda attitude ya Magufuli kuhusu potential ambayo nchi yetu inayo...tunapaswa kuwa donor country kama tukijipanga vizuri! Hapa nampa 100%
 
Wacha mimi nichague kukaa kimya tu hapa nikimsema huyu mzee mleta mada ni kujitafutia laana.

Taifa kama halina umoja na upendo hayo unayomsifu nayo yanasaidia nini

Kwenye historia ya nchi hii kuna mwaka watu walishawahi kususia uchaguzi wa serikali za mitaa? Hili wewe unalitazama kwa midhani ipi? Ni jambo dogo sana hili kwako?

Hakuna mtu mbinafsi kama Magufuli ni swala la muda haya mnayomsifia yanayo yatawatokea puani

Leo Watanzania wanaambiwa wakapige kura waumini wa wakatoliki, kesho Kkkt watawaambia waumini wao wasipige kura vivyo hivyo kwa Waislamu

Leo Tanzania hii mbunge anaenda kwao anazuiwa kwamba hana kibali na akitaka kwenda ni mpaka aombe kibali

Huoni kabisa hatari iliyo mbele yetu badala yake Stiglers gorge wewe ndio umeona kitu cha maana?

Mtu kuropoka hovyo wewe ndio unaita uwazi kama ile wakati anaingia madarakani sukari ilikuwa 2000 serikali yake ikateremsha mpaka 5000

Kama kweli huyu Magufuli ni muadilifu Prof Assad (CAG) ni kati ya watu waliopaswa kuundiwa zengwe na yeye mwenyewe na Ndugai?

Haya endeleeni na mapambio yenu mkishtuka jahazi lishazama
 
Sijui kwa nini watu kama Mzee Mwanakijiji huwa hawataki kuelewa jambo rahisi tu linalorudiwarudiwa mara kwa mara - lakini hawataki kabisa kulielewa.

Hayo mambo uliyoorodhesha hapo juu, kweli kuna anayeyapinga kwa dhamira safi?

Kinachomwondolea sifa Rais Magufuli ni jambo moja kuu. "Kutoheshimu HAKI za wengine, 'full stop.'"

Haya unayosema anayafanya, yanahitaji 'HAKI' za watu zikanyagwe ndipo yafanywe? Hayawezi kufanyika bila ya kuumiza wengine?
Inahitaji kufarakanisha jamii katika taifa ili taifa 'lijitegemee'?

Siku moja kaa chini uandike makala ndefu kuhusu hilo, nitaisoma yote kwa makini.
 
Boss Mzee Mwanakijiji Kati ya Mambo hayo manne, nakubaliana na wewe Mambo mawili tu:
1. Dhana ya kujitegemea.
4. Ujenzi mpya wa Taifa.
Haya hata na Mimi nampongeza sana Mh. Rais.

Lakini haya mawili yaliyobaki, Hakuna kitu:
2. Amekataa kuheshimu Sura, hii si kweli. Mwenye macho aambiwi tazama, angalia baadhi ya Wasaidizi wake anavyowakingia vifua, angalia baadhi ya skendo anavyofungia vioo, hafukui makaburi.
3. Amekuwa Muwazi kupita maelezo, ili nalo Mzee umetuingiza Chaka, Mfano Mdogo tu Ununuzi wa Ndege, kwanini CAG kazibwa mdomo???!!!

Ungeweka hili,UDHUBUTU, kwa kweli mnyonge mnyongeni, HAKI yake mpeni. Kwa hili la UDHUBUTU Mh. Rais anastahili TUZO.

Kwa kazi ya Mh. Rais haikutakiwa kabisa nguvu kubwa kumsifia na kutangaza mazuri yake. Always Kizuri kinajiuza, na kibaya kinajitembeza.

Ushauri wangu: Viongozi wengi waandaliwe, wapikwe wapikike. Taasisi imara ziimarishwe, kuliko kuimarisha Watu au Mtu.

Hakuna Kiongozi mzuri duniani. Ukishakuwa Kiongozi ujue kabisa utakuwa Kiongozi mzuri na Kiongozi mmbaya. Hata ufanye mazuri mengi, lazima atatokea au watatokea Mtu atasema wewe ni Kiongozi mmbaya.

Na. M. M. Mwanakijiji

Yote tisa, kumi tuseme ukweli. Kuna mambo ambayo mtu anaweza kuamua kuyachukia dhidi ya Rais Magufuli. Mtu anaweza kuamka na kuapa kwa jina la miungu na mababu zake ya kwanini hataki kulisikia jina la Rais Magufuli. Tena mtu anaweza akaamka hata usiku wa manane kama mtu aliyepatwa na jinamizi akiwa na hofu ya Magufuli. Siwezi kuwasemea wale ambao wakisikia jina la Rais Magufuli wanaweza kujihisi pumzi zinawaisha na kujisikia unyonge. Umpende au umchukie Rais Magufuli bado anaonekana kugawa hisia za watu mbalimbali tena kwa ukali sana; ama unamkubali au unamkataa; hakuna upande wa katikati.

Na wapo pia ambao wanaposikia jina la Magufuli kwao wanajisikia matumaini, faraja, na wengine wanakuwa kama yule mwanamuziki aliyeimba wimbo wa “Magufuli Raha Tu”. Hawa wanaposikia jina la Rais Magufuli ni kama wanapata Amani ya huko mbeleni, wanajua nchi iko salama na kuwa wao na watoto wao wanashuhudia mambo ambayo labda hayakudhaniwa kuwa yanaweza kutokea katika nchi hii hii ya Waafrika tena miongoni mwa zile nchi zilizokubali jina la “Maskini Zaidi” duniani. Kwa hawa ukitaja jina la Magufuli hata ukiwaamsha usingizini wengine wanaweza kuhisi ni kama unawakatisha zile ndoto tamu tamu zinazoweza kumfanya mtu ajikute anatafuna mto akidhania ni keki!

Vyovyote vile ilivyo kuna mambo manne ambayo naweza kuyasema kwa ufupi tu ambayo Rais Magufuli anayafanya tofauti sana na viongozi wengine. Bila ya shaka kuna mengine anayafanya ambayo yanafanana na watangulizi wake na kubwa katika hayo ni ile hali ya kutukuza chama chake na kukifanyia kila namna ya msaada na mbinu ya kutaka kiendelee kubakia madarakani kwa miongo mingi ijayo. Sidhani kama kuna kiongozi atakayekuja kutoka CCM ambaye atafikiria au kujaribu kufanya kinyume cha hilo. Hata hivyo, binafsi ningependa kudokeza yale mambo ya kiutendaji (executive) ambayo Rais Magufuli anayanya – kwa maoni yangu – kwa namna tofauti na viongozi watatu waliomtangulia.

1. Dhana ya Kujitegemea Ameipa Magurudumu
Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere wakati anaikaripia serikali ya Rais Mkapa kufuatia ile sera ya “ubinafsishaji wa mashirika ya umma” na ile hali ya kujaribu kuendekeza sana “wawekezaji wa nje” aliwahi kusema hivi (naapa nimenyambulisha kidogo) “Mnaweza kuamua kuachana na siasa ya ujamaa, lakini hamuwezi kuachana na sera ya kujitegemea”.

View attachment 1266057
Rais na viongozi wengine wakiangalia modeli ya bwawa la kufulia umeme la Nyerere, Rufiji.
​

Nadharia hii ya “Kujitegemea” ni miongoni mwa dhana ambazo bila kueleweka zinaweza kumfanya mtu awe duni mbele ya wengine. Mtu ambaye ni “tegemezi” au Nyerere aliita “ombaomba” kwa kiasi fulani anajidunisha mbele yaw engine. Kwa muda mrefu nchi zetu hizi za Kiafrika zilifika mahali za kuomba hadi misaada ya kujenga vyoo! Na bado hata leo kuna watu ambao wanasubiria serikali iwafanyie vitu ambavyo hata vilivyopo ndani ya uwezo wao. Kurudi kwenye “kujitegemea” ni kurudi kwenye kuuheshimu na kuulinda utu wetu kama binadamu. Hivi ni kweli, tunahitaji msaada wa kigeni kupanda bustani ya maua shuleni, au kwenye ofisi? Je, ni kweli tunahitaji msaada kutoka SIDA, USAID, EU, JICA, DANIDA, NORAD ili kuweza kufanyia ukarabati shule zetu kongwe, kujenga shule mpya, kutengeneza madawati kwa ajili ya shule za watoto wetu, au kujenga viwanja vya kuchezea watoto na maktaba? Magufuli anaposema “tunaweza” anataka kutuambia kuwa “tumechelewa kujitegemea!”

Magufuli tangu kuingia kwake madarakani ameamua kulishikilia hili kama kwa mapembe. Analazimisha Taifa liwe na fikra za kujitegemea. Na hapa ni katika kutumia raslimali zake, uwezo wake, watu wake na mipango yake katika kujiletea maendeleo. Hakuna jambo linalotishia uhuru na utu wetu kama taifa kama kutegemea watu wa nje kwa mafanikio yetu. Jambo hili la kulazimisha taifa kujitegemea linaweza kuwa ni mafanikio makubwa zaidi ya Rais Magufuli kuliko mambo mengine.

Binafsi sitoshangaa kwa mwaka unaokuja Magufuli akiagiza wizara na idara zote kuandaa bajeti zao za 2020/2021 bila kuweka ndani au kusubiria misaada ya kigeni. Sitoshangaa kabisa akaamua kutukatisha kunyonya (weaning) kutoka kwa mashangazi zetu wa Ulaya na kulazimisha taifa kupanga bajeti yake kwa kutumia mapato na vyanzo vyake vya ndani. Misaada ya kigeni ikawa siyo tena ya moja kwa moja kwenye bajeti (Non-direct budgetary support). Akiamua kufanya jambo hili nawahakikishia dunia nzima itashtuka na hawatoamini na siyo hivyo tu wapo wenzetu humu humu (wapingaji) ambao watatuambia kwanini hatuwezi kujitegemea kwenye bajeti!

2. Amekataa Kuheshimu Sura
Kwa muda mrefu watu walikuwa wakishika madaraka walikuwa wanajiona wamefika. Watu walipoapishwa kushika ofisi yeyote walijisikia wako salama na wengine walifanya sherehe na kujisahau wakidhania sasa hatimaye na wao wamekuwa kwa waliokuwemo. Magufuli amewafanya sasa hivi watu kutokuwa salama kwenye vyeo vyao. Mtu anaweza kudhania hili ni jambo baya; lakini kiutawala hakuna jambo muhimu kama watu kurudi na kutambua dhana ya “cheo ni dhamana”. Hakuna aliye salama kwenye kiti chake na kuwa wakati huko nyuma watu walitegemea “Rais kuwalinda” sasa hivi hakuna anayeweza kuishi na kujihisi kuwa analindwa. Unaweza hata kuwaonea watu huruma.

Lakini kinyume na hisia ya wengi Rais Magufuli haoni aibu au kufikiria mara mbili kumuondoa hata mchezaji nyota kwenye mechi! Kulikuwepo na baadhi ya “wachezaji nyota” na wakajikuta wanaondolewa na mechi inaendelea kupigwa na watu wakashinda vile vile. Jambo hili limewafanya baadhi ya watu wanaojidhania au wanaojifikiria kuwa ni wachezaji nyota kujiangalia mara mbilimbili kweli kweli. Sasa hivi, hakuna kujali sura, tunajali utendaji wa kazi. Niliandika mada moja mwanzoni mwa utawala wa Magufuli na labda watu hawakuelewa uzito wake; nilisema “Tengua Tengua Inayokuja”. Sasa hivi ukipewa kiti cha utawala sheherekea huku unatokwa machozi. Wale wale watakaokuletea maua ya pongezi ndio watakaomletea mwingine maua ya pongezi.

Matokeo ya hili ni kuwa tunaona watendaji wengi – hasa mawaziri – wakiwa wanyenyekezu, wenye kujituma na kila mmoja akijitahidi kujionesha yuko kazini. Hata yule mwana mpendwa baada ya kupigwa mkwara wa juzi, tunamuona naye sasa hivi anakalia kitu kwa kukinyemelea! Wanaofikiria Magufuli anaiheshimu sana sura yake, watakuja kushangaa sana siku si nyingi.

3. Amekuwa Muwazi Mno hadi Kupitiliza
Kwa muda mrefu tulikuwa hatujui mambo yanayoendelea ndani ya serikali yetu. Mambo mengi tulikuwa tunayasikia kwenye majungu tu na vijiwe. Mambo mengine tulikuwa hata hatuyajui kabisa lakini sasa hivi ni kama tumefunguliwa mlango na madirisha tuchungulie kinachoendelea ndani. Rais Magufuli kwa ile tabia yake ya kutokuwa mzuri sana wa maneno, na kukataa kuyapamba maneno yake anaweza kuonekana wakati mwingine kama “fyatu” fulani hivi. Lakini kwa wanaomjua na sisi ambao tumemfuatilia kwa muda mrefu tunajua ni kuwa hana tabia ya kuficha ficha. Hata ile kauli yake maarufu ya “Msema kweli mpenzi wa Mungu” kimsingi inatuambia tu kuwa haoni sababu ya kwanini Watanzania wafichwefichwe. Kile anachoamini ni ukweli atakisema hadharani na wazi kabisa na wakati mwingine kutoificha aibu ndani ya serikali yake mwenyewe. Na watu wakaona – wakamsema na hata kumnyoshea kidole yeye mwenyewe. Rais wetu kwa kiasi kikubwa hana siri sana! Kuna mambo ya siri lakini ukiangalia sana mambo mengi ambayo watu wangependa kuwa ya siri hayana usiri wa maana kivile zaidi ya kufichiana tu siri zisizo na maana.

Uwazi huu umewasaidia wananchi kuona nini kilikuwa kinafanyika na nini kinafanyika sasa hivi. Bahati mbaya inaweza kusemwa ni kuwa uwazi huu ungenoga zaidi kama vyombo vya habari visingekuwa vinajisikia vinabanwa au kuulizwa ulizwa vinapojaribu na vyenyewe kufichua mambo. Hili sitolishangaa litatokea pia kwani “msema kweli ni mpenzi wa Mungu”. Siyo majungu, siyo umbeya, siyo porojo bali ukweli tu. Kwa vile Rais ameamua kuwa muwazi kwa wananchi ni lazima awaache na wananchi wawe wawazi kwa serikali yao; kwa maana halisi ya quid pro quo (nipe nikupe). Hakuna haja ya kufichana.

4. Ameamua Kufanya Ujenzi Mpya wa Taifa
Mojawapo ya mambo ambayo labda ni kubwa zaidi (linaloendana na lile la kwanza) ni uamuzi wake wa kufanya ujenzi mpya wa taifa (national reconstruction). Magufuli ni kama amedakia alipoachia Nyerere. Ukiangalia sasa hivi ni kana kwamba miaka ya Mzee Mwinyi, Mkapa na Kikwete haipo. Ni kama Magufuli ameamua kuifuta na kuichukua nchi mwaka 1985. Akiichukua nchi mwaka 1985 anaikuta nchi ambayo imetoka kwenye janga la wahujumu uchumi (ufisadi), viongozi ambao wameshaonja ubepari na sasa kila mtu anataka kula kwa raha zake, na kuwa analikuta taifa ambalo wananchi wake wanatafuta maisha bora. Magufuli anaingia na kuamua kuendeleza mambo yale ya msingi ya kujenga misingi.

View attachment 1266052
Ujenzi wa Tanki la Maji huko Singida
​

Katika hili ameamua kufanya masuala ya ardhi na makazi, miundombinu (infrastructures), elimu, maji, umeme na nishati, kilimo, madini na afya. Katika mambo haya Rais Magufuli anajaribu kupalilia nchi na kupanda mbegu ili wengine waje kuvuna. Na anachofanya – na labda wakati mwingine wengi hawasikii – ni kuwa katika nchi nzima, na kwa wakati ule ule (simultaneously) miradi mbalimbali inatekelezwa.

Anachokifanya ni kuhakikisha kuwa hakuna sehemu kubwa ya nchi ambayo inaweza kujihisi inapitwa. Ukiwasikiliza watu wenye kukosoa kinachofanyika “Chato” unaweza ukadhania Magufuli amegoma kufanya jambo lolote sehemu nyingine ya nchi. Hili linaweza kuwa ni udhaifu wa taasisi zenyewe kujieleza lakini kwa tunaofuatilia tunajua jinsi gani matanki ya maji, njia za umeme, hospitali, vituo vya afya, barabara, vinavyoendelea kujengwa au vilivyokwisha jengwa ndani ya miaka hii minne kulinganisha na miaka mingine yote.

Mwisho
Mambo haya manne Magufuli anayafanya kwa namna ya tofauti sana. Lakini tofauti hiyo naweza kuielezea inatokana na mambo makubwa mawili ambayo hayakuwepo huko nyuma. Moja ni kuwa amekataa kufuata kilichoandikwa vitabuni. Kwamba, namna ya kufanya mambo ni a, b, na c kama watu walivyosoma shuleni. Badala yake anawalazimisha watendaji walio chini yake kufikiria nje ya sanduku na kujaribu vitu tofauti. Matokeo yake baadhi ya mambo ambayo yangekuwa yanachukua muda zaidi au raslimali zaidi yanaweza kufanyika kwa ubora na uharaka kuliko huko nyuma. Chukulia mfano wa mambo mawili tu kati ya mengi – suala la Masoko ya Madini na Vituo vya Mabasi – mambo haya hayakutangaliwa na vikao virefu vya sera na mipango; ni mambo ambayo yaliamriwa na watu wakapewa kazi kwenda kuyatekeleza.

Jambo la pili ni kuwa Rais Magufuli hana hofu ya kukosea au kuonekana amekosea. Kwa wanaomjua Magufuli hili wala si jambo jipya. Toka zamani Magufuli amekuwa ni mtu wa kufikiria kitu na kukitenda labda wakati mwingine kwa gharama kwa serikali au hata hadhi yake; lakini hofu ya matokeo ya kisheria (legal ramification) haijamzuia Magufuli kufanya kitu anachoamini ni sahihi. Hofu ya kuogopa kushtakiwa, au kugombana na wakubwa haikumzuia. Tuliona hili wakati wa suala la Makanikia na jinsi gani baadhi ya watu waliona kama Magufuli amegusa wakubwa na hatokuwa salama tena. Lakini Magufuli alisimamia kile hadi dakika ya mwisho. Hata hili suala la ujenzi wa Bwawa la Nyerere; kwa wengine liliwatia hofu kuwa wakubwa watetezi wa “mazingira” wangemkwamisha; lakini kama huwaombi dola zao watakukwamisha kwa lipi?

Miye nasubiria watakapoanza kutengeneza zile “cable cars” kuruka Ngorongoro na kutengeneza viewing platforms kama zilizoko kwenye vivutio vingi kwenye nchi za wenzetu (nenda pale Grand Canyon utaona). Sitoshangaa kuna watu watapiga kelele kweli. Wakati wenzetu wana barabara za lami zikikatisha Yosemite Parks na Parks nyingine huko majuu sisi kwetu tunaambiwa hata zinatishia wanyama na kuvuka kwa wanya kana kwamba hakuna namna ya kushughulikia hilo. Hili la pili ndio linaweza au limeweza kumtengeneza Magufuli maadui wengi wan je. Hana heshima kwao na kitendo chake cha kutokwenda kwao “kujionesha onesha au kujitambulisha” kunawakwaza wengi kweli kweli. Rais wa Afrika asiyependa kushikana mikono huko New York, Geneza, Paris na London ni mtu wa tofauti sana.

Mambo haya 4 bila ya shaka Magufuli anafanya tofauti sana na wengine watatu waliomtangulia. Inawezekana yapo mengine mengi ambayo anayafanya tofauti na wenzake. Na hapa nazungumzia yale chanya. Mtu mwingine anaweza kubisha. Nani anabisha?

Niandikie:
[email protected]
 
Mzee MM anazeeka vibaya, though sijawahi kukutana nae USO kwa USO lakini tulishawahi kuwa kwenye harakati za Ukombozi pamoja, anajua maana tulikua na Max pia na kwamba anaujua ukweli jinsi gani alikua akitumika, aliamua kuhamia CCM yeye na Slaa.

Hongera Sana Maxence Melo kwa kukataa kuwa mtumwa! Unakumbuka mwaka ule tuliongea kwa kifupi juu ya mambo Haya na jinsi walivyokusumbua....

Mwanakijiji, salams.

Umefanya uchambuzi mzuri na vizuri.

Hata hivyo nina swali moja tu kwako. Nitalipa utangulizi kusudi uweze kulielewa.

Mie ni mseminari katoliki mstaafu. Seminarini, wakati tunasoma moral philosophy, tulifundishwa kuwa kuna siasa za aina nne:

- mosi ni siasa zinazochanganya mbinu halali na malengo halali.

- pili ni siasa zinazochanganya mbinu halali na malengo haramu.

- tatu ni siasa zinazochanganya mbinu haramu na malengo halali.

- na nne ni siasa zinazochanganya mbinu haramu na malengo haramu.

Siasa za kundi la kwanza tuliambiwa ni adilifu. Makundi matatu yaliyobaki tuliambiwa ni siasa haramu.

Kwa kuangalia matendo na malengo ya JPM katika mipaka ya mambo haya manne uliyoyataja unaona yeye anafanya siasa zilizo katika kundi gani?

Zingatio: Wakoloni walitekeleza miradi mingi na mikubwa kama vile ujenzi wa reli ya kati lakini bado tuliwakataa kwa sababu moja: mradi huu ulikuwa ni mbinu halali kwa ajili ya kufanikisha lengo haramu la kuendeleza ukoloni--yaani kuendelea kututendea kama watumwa ndani ya nchi yetu wenyewe

nani haqkufanya hayo? mbona mnakuwa watu wa ajabu! Msiwe kama Mwakyembe jamani!
Ushabiki au hasira zikizidi zinazuia mtu asione uhalisia wa mambo, au anaona lakini anajikuta anakataa ukweli bila kujijua.
Let's prioritize reasoning over emotions, emotions may cloud your judgement.
Hate, Joy, sentiments, grief, and love are the products of emotions.

If your hate or love for Magufuli is too much then you are bound to judge his performance compelled by emotions.
Either you won't see positive or negative side of him depending on the receiving end you are in..

Njaa pia inaweza kukufanya umchukie Magufuli au umepende kiasi cha kukufanya usikubali mazuri yake au mabaya yake kutegemeana na wewe upo upande gani kati ya wanaofaidika nae au wanao umizwa na utendaji wake kwa kuzuiwa maslahi yao binafsi.

Kuna sisi neutrals tunaona yote vizuri sana, mazuri na mabaya ya Magufuli, tena ni watu wenye amani ktk nafsi zetu.
 
1. Kuipa magurudumu dhana ya kujitegemea.

Magufuli ni mtu mwenye utovu wa elimu ya kisiasa. Ni Mkemia aliyejikuta kwenye siasa. Hajui akitaka kujitegemea aanzie wapi.

Yupo incoherent.

Mfano mdogo. Aliona kuingilia biashara ya korosho kwa nguvu ya jeshi ndiyo kitu kizuri. Akaonywa hilo si jambo jema na litaangusha mapato, hakusikia, matokeo yake, ripoti ya Benki Kuu ya Tanzania ya Oktoba 2019 inasema mapato ya exports za mazao ya kilimo kwa mwaka ulioishia Agosti 2019 yameanguka kwa asilimia 55, ukiyalinganisha na ya mwaka uliopita. Sababu kubwa kabisa ya kuanguka huku ni serikali ilivyoingilia kwa mabavu biashara ya korosho, zao la kwanza kwa kutupatia fedha za kigeni.

Kwa kila shilingi 1000 tuliyopata mwaka wa kabla ya huu uliopita, kwa mwaka uliopita tumepata shilingi 450, hasara ya shilingi 550, zaidi ya nusu nzima!

Mtu aliye incoherent, ambaye anakwenda kwa kuhamanika kwa munkari bila mkakati, hawezi kutupa hoja ya kujitegemea.

2. Magufuli hajakataa kuheshimu sura. Anatengeneza image ya uongo kwamba yeye haheshimu sura. Magufuli angekuwa haheshimu sura kweli, Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda, angekwishaondolewa siku nyingi sana. Makonda ana scandals nyingi sana. Scandal iliyomvua nguo kabisa Magufuli ni pale Makonda alipotaka kuingiza samani kwa ujanjaujanja, Magufuli akamsema kama anamuogopa vile, wakati kawaida yake anatumbua watu kabla hotuba haijaisha. Hili limetuonesha kwamba Magufuli ni bully tu, anawa bully watu fulani, akifika kwa watu wake kina Makonda anachekacheka, hata wavamie redio na bunduki au waingize vitu bila kulipa kodi. Kabakia kutukana viongozi wenziwe na wake zao tu.

3. Uwazi
Uwazi ni kitu kizuri. Lakini there is such a thing as "too much information". Rais anatakiwa kuwa muwazi, lakini anatakiwa kuwa na kifua cha kuweka maneno.Magufuli hana kifua cha kuweka maneno, anaropoka sana, huu si uwazi. Kuna tofauti ya mtu kuwa muwazi na mtu kuwa mropokaji. Magufuli si muwazi, ni mropokaji. Usichanganye hayo mawili.

4. Ameamua kufanya ujenzi mpya wa taifa

Kuna habari moja, sijui kama ni ya kweli au kutungwa, lakini ina funzo zuri, hivyo kwa msingi huo, naiona inafaa kurudiwa, hata kama ni ya kutungwa, kwa sababu ina mafunzo mema.

Wanasema kulikuwa na Waziri mmoja wa Fedha wa Nigeria. Alienda Uswizi kwenye mabenki makubwa ya dunia. Akaaulizia, hapa benki kubwa kabisa inayoficha hela za vigogo wa Nigeria iko wapi? Akatajiwa. Akaenda ile benki, akasema mimi waziri wa fedha wa Nigeria, naomba kuongea na mkurugenzi wenu.

Akapewa appointment na Mkurugenzi, akaenda kuongea naye.

Akamwambia Mkurugenzi, nimekuja hapa nina shida, Africa tunaibiwa sana fedha. Nataka unipe list ya wateja wako wa kutoka Nigeria, na hela walizoweka katika benki yako, tuwahakiki na biashara zao kama hela hizi ni halali, wanalipa kodi etc.

Yule Mkurugenizi Swiss banker akamwambia wewe jamaa una kichaa ama nini? Sisi tuna sheria za kulinda wateja wetu hapa. Waziri akamwambia mimi sijajja kufanya mchezo hapa, nina barua kutoka serikali ya Nigeria. Mswizi akamwambia hata ingekuwa serikali ya Uswizi au Marekani, hatujali, tuna sheria zinatulinda. Waziri akasema sawa, tutafuta deals zote za serikali ya Nigeria na benki yako, mtakosa hela nyingi sana. Yule Mkurugenzi akasema wala sijali. Waziri akatoa bastola, akamuwekea Mkurugenzi kichwani, akasema nipe majina haya, usiponipa nakufyatulia risasi ufe. Banker Mkurugenzi Mswizi akasema Waziri wewe niue tu, majina sikupi.

Waziri akasema, vizuri sana. Nimeitafuta benki yenye usiri kama hii kwa muda mrefu sana sijaipata. Haya hapa mamilioni yangu nataka mniwekee, maana kwa usiri huu umehatarisha mpaka maisha yako, nikiweka hela zangu hapa, hakuna atakayejua.

What is the point of this story? Mara nyingine watu wanaojifanya wakali sana kupinga rushwa, kujenga taifa etc, wanaweka show tu. Wao hao hao ndio wapigaji wakubwa na wala rushwa wakubwa.

Magufuli hawezi kuwa ameamua kujenga taifa, kwa sababu analigawa taifa kisiasa, ameharibu umoja wa kitaifa kuliko rais yeyote aliyempita, anasema wazi kwamba atapendelea watu wa CCM. Sasa hapo anajenga taifa au anajenga watu wa chama chake?
Comment bora sana siku ya leo, huyo Mwanakijiji hawezi kukuelewa kwasababu haishi Tz, angekua uku kitaa angeona jinsi tulivyogawanyika asingekua anaimba mapambio hapa, yeye anawasikiliza kina Pengo na Sheikh wa Bakwata ndio anaona mtazamo wetu waTz
 
Tatizo wako soo caught up na miundo mbinu..kila wakitengeneza barabara hii,wanaona watengeneze na nyingine..wanasahau kuweka mambo kwenye balance,maeneno mengine pia kama Elimu yanahitaji matengenezo pia,..kila kitu kifanyike moderately.....

Mfumo wetu wa Elimu ukifumuliwa elimu itakayotolewa ikiwa inaendana na mazingira..(relevant education), then tatizo la ajira litapungua sana tuu...hawa wahitimu wa sasa hivi tunaweza tusijue la kufanya kuhusu wao,lakini tuna nafasi kubwa tu ya kurekebisha hili tatizo kwa wahitimu wanaokuja.......

Lugha pia imekua identified kama ni barrier kwenye Elimu yetu,lakini nothing is done,mie sijali kama tutatumia kiswahili kote kuanzia vidudu mpaka chuo au kutumia kingereza kuanzia vidudu mpka chuo...lazima tuchague lugha moja kama tunataka wasomi na sio wahitimu waliokariri theories...
[/QUOTE Wanangu nilisha watoa kwenye kundI la wahitimu Mkenya na Mganda wakija hapa watapambana nao vibaya hadi kieleweke.
 
Comment bora sana siku ya leo, huyo Mwanakijiji hawezi kukuelewa kwasababu haishi Tz, angekua uku kitaa angeona jinsi tulivyogawanyika asingekua anaimba mapambio hapa, yeye anawasikiliza kina Pengo na Sheikh wa Bakwata ndio anaona mtazamo wetu waTz
Asante mkuu.

Huyo kaamua tu kuwa mpiga zumari wa mfalme. Anachosema si sababu yakukaa US.

Hata mimi nakaa US lakini nikifuatilia mambo naona kinachoendelea Tanzania si kizuri.
 
Magufuli ni muwazi kupitiliza? What is this? kuwaambia kwamba huwa anasoma meseji za mawaziri wake wa kike wakichambana ndo uwazi huo? Aruhusu basi CAG apite kidogo tu huko kwenye madini, ATCL, ujenzi wa Chato Airport, Ununuzi wa korosho etc.
 
Hakuna nchi isiyo na deni la taifa; Marekani sasa hivi deni lake la taifa ni trilioni 22 (dola) hivi. Haina maana ni mwisho wa dunia na haina maana uchumi ni mbaya. Ukopaji wa serikali kuu kwa ajili ya kufanya shughuli mbalimbali ni jambo la kawaida katika nchi yeyote. Sasa suala la "inalipwaje" ndio swali zuri na unatakiwa kuangalia mipango ya BoT au Wizara ya FEdha wanasema nini kuhusu servicing the national debt.

Fedha za ndani zina deni? Kama kuna ukopaji huambiwi unachoambiwa miradi ni fedha za ndani, hiyo bank kuu inaweza kukuambia ulipaji wa deni? Kwakuwa ww umeweza kuja na pambio la hayo maendeleo, sio vibaya ukija na kibwagizo cha jinsi ya kulipa deni.
 
Siyo kumsifia; ni kuonesha anafanya vitu fulani tofauti na waliomtangulia na matokeo yake ni chanya kwa taifa. Wapo wengi wanamkosoa na wengi wanafanya kazi nzuri; si lazima wote tujipange mstari wa kukosoa ili kusema "ni wakosoaji".

Mbona hakuna jambo linalofanywa kwa mabavu, au kashfa? Huo ukali una matatizo gani? Unataka watu wabembelezwe na kupewa peremende; kwamba watu wasikaripiwe au kugombezwa? Kwani hawa watoto wadogo wa kuchekelewa chekelewa. Tumechekeleana sana na kuimbiana "kumbaya".. hizi ni zama nyingine sana. Siombei Tanzania irudi kwa watu wenye kuchekeleana tena!
g
Well kwakua ume-side na vitu ambavyo kwako ni chanya kwa mtazamo wako baso ngoja nikuonyeshe jambo dogo sana ambalo ni hasi kwenye jambo moja ulilolionesha kuwa ni zuri kwa mtazamo wako.
9

MMK sipingani na mradi wa bwawa la umeme. Lkn napingana sana na utekelezaji ambao haukuzingatia viwango na ushauri wa kitaalamu haswa kwenye swala la utunzaji mazingira na vyanzo vya maji.

Pili sioni mantiki ya kurisk such expensive huge project kwenye eneo ambalo nimiudt close to the mouth of an ocean. Hii inamaana oceanic catastrophe may wash it away. Kwasabb kwa physical nature ya eneo la mradi bahari ina tapikia humo kwenye mto rufiji. Ilitakiwa implementation ifanyike kwenye eneo tofaut and it could have been so wise ungepelekwa hata usawa wa small ruaha river. Rufiji ikabaki kupokea maji na ystumike kwa ajili ya kazi za kilimo na ikatengenezewa recreation site baada ya bwawa.
Well ngoja kwanza ninyonyeshe ntarudi
 
Mwanakijiji subiri kidogo usiondoke,wapiga vinubi,na wapiga zumari na watukufu wasifiaji wa awamu hii wanakuja kukuburudisha na vinubi vyao uandae kabisa style ya kucheza zumali linapopigwa
 
Waziri akasema, vizuri sana. Nimeitafuta benki yenye usiri kama hii kwa muda mrefu sana sijaipata. Haya hapa mamilioni yangu nataka mniwekee, maana kwa usiri huu umehatarisha mpaka maisha yako, nikiweka hela zangu hapa, hakuna atakayejua.

What is the point of this story? Mara nyingine watu wanaojifanya wakali sana kupinga rushwa, kujenga taifa etc, wanaweka show tu. Wao hao hao ndio wapigaji wakubwa na wala rushwa wakubwa.
Kwa huyu, dalili zipo wazi kabisa.
Huwezi kwenda kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa kijijini...ukawa huna ushamba wa aina fulani!
 
What is the point of this story? Mara nyingine watu wanaojifanya wakali sana kupinga rushwa, kujenga taifa etc, wanaweka show tu. Wao hao hao ndio wapigaji wakubwa na wala rushwa wakubwa.

Venezeula walikuwa na Chavez ambaye alijisifu kuwa mzalendo namba moja. He tanked the economy kwa siasa za nationalism na one man show. Akawaachia Maduro and the rest is history.

Hapa tunaye Rais Magufuli anayejisifu kwa uzalendo na one man show. Gimmicks za kugawa pesa barabarani kuonekana anajali hazina tofauti na Chavez. Investing in white elephants kama Chavez na pia atatuachia Maduro (Makonda) and the rest will be history.

Muhimu watu waelewe hii miradi ya SGR (Dar mpaka Mwanza), Stiegler's Gorge and ATCL will bankrupt the country na kusababisha matatizo makubwa kwenye uchumi. Wasomi wachache watakimbia na kutabaki na brain drain kubwa.

Kwa sasa "mabeberu" wanafikiria ni jinsi gani watakuja kufanya debt swap and restructuring wakati sisi tunashabikia mtu anayetupeleka shimoni. Historia itaona si wote tulishabikia.
 
JPM ndo rais wa kwanza Tanzania kukiri kwa kinywa chake na kusema "Tanzania ni nchi tajiri....watanzania tunaweza, tembeenj vifua mbele"...
Predecessors wake wote including Nyerere walikuwa wanakesha kutufanya tujisikie wanyonge kutuambia sisi ni masikini, featherweight na lazima tusujudu...
 
  • Thanks
Reactions: Ole
Back
Top Bottom