Swali chechefu: Sijawahi kumsikia Kadinali Rugambwa akitema cheche hata kiduchu tu. Kwani kuna shida?

Swali chechefu: Sijawahi kumsikia Kadinali Rugambwa akitema cheche hata kiduchu tu. Kwani kuna shida?

Kwa Mufti wa wenzetu kule, akina Takbiir!, unaweza kung'amua ni kwanini yupo kimya; ila kwa huyu wa kwetu, Mhashamu sana, Mkuu sana, kulikoni hasemi chochote? Mimi kwa kweli huwa naonaga picha zake tu, halafu natamani sana aseme neno, lakini simsikii kabisa kabisa akisema neno - akitema cheche!

Na sio maneno mengi wala, kiongozi mwenye ukubwa kama yeye, ni maneno kidoogo tu, baaaasi! Unaunguza mtandao mzima wa mapori tengefu, cheche!

Kumbe mimi nisingekuwa Padri mzuri, japo nilitabiriwa kuwa padri, maana napenda sana kuongea, na sio maneno matupu tu, bali, ni cheche! Najua mnajua naongea kitu gani haswa: cheche! Hata Padri Kitima alivyoshambuliwa, nilitegemea kuziona cheche!

Nikiyasema haya, linanijia jina la Laurent Mwonsengwo Pasinya, huyu alikuwa ni Padri huko Congo DRC ambaye alikuja kuwa Kadinali. Enzi za maisha yake, huyu mkuu sana, alikuwa anawatemea sana cheche na moto, viongozi wa Congo DRC waliotaka kubagaza haki za raia na demokrasia. Alimpa shuruba sana Mobutu Seko Kuku Ngwendu wa Zebanga, na pia alimtemea sana cheche Joseph Kabila alipotaka kuupora uchaguzi wa 2011 huko Congo.

Wakati utawala wa Mobutu Seko ukikaribia ukingoni, ni Mwonsengwo Pasinya aliyeaminiwa na wacongo kushika nyadhifa kubwa kwenye serikali ya mpito kama: President of the Sovereign National Conference mwaka 1991, president of the High Council of the Republic mwaka 1992, na speaker of a Transitional Parliament mwaka 1994.

Najiuliza swali: Ikiwa Kadinali wetu hatemi cheche, je, ataweza kuvivaa viatu vya Mwonsengwo Pasinya? Au, ya Pasinya tumuachie Pasinya?

Cheche zipo wapi cheche?
MC
Kwanini unataka awe vile unavyotaka wewe ?
 
Back
Top Bottom