Swali chechefu: Sijawahi kumsikia Kadinali Rugambwa akitema cheche hata kiduchu tu. Kwani kuna shida?

Swali chechefu: Sijawahi kumsikia Kadinali Rugambwa akitema cheche hata kiduchu tu. Kwani kuna shida?

Jitokeze kusema wewe mwanaume mzima unasubiri usemewe? Chefuuu
Jifunze kutofautisha kati ya kusema na kutema cheche, na hapo ndo ilipo tofauti kati yangu na wewe. Wewe unaimba sana maneno ya taarabu na kanga - maneno meengi yasiyo na impact. Mimi maneno yangu kidogo sana, lakini nikiyatoa, lazima kitatange kama wewe uibuke kutoka mafichoni, natema cheche!
 
Hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kuropoka bila ya kuangalia ; ukweli ni kwamba hayo mnayosema mtandaoni ni drama za kuleta hofu kwa mtawala ila hamna tatizo ..Yalikuwepo na yataendelea kuwepo ,kama kufa watu kila siku wanakufa .

Kila zama wanasiasa wa upinzani wanatumia mbinu ya kupinga utawala .. Magufuli walimzushia mengi na kumuita dikteta ,huyu wanamuit mtekaji baada ya hoja ya uzanzibar wake kupata majibu.

Hakuna hofu wala tatizo kama litakuwepo ataongea ...Sio kila mtu ni mjinga wa kufanyiwa manipulation na wanasiasa ...Umeme enzi zile ukikatika anatukanwa January Makamba ila leo Anatukanwa samia ,yule waziri wa mambo ya ndani kwa vile dini ile hasemwi hata watu wakitekw😂
Kuropoka sio kutema cheche, usipotoke mkuu, ni bora ukaniuliza kwanza maana ya kutema cheche, kulikoni kunisulubisha kwa kunilisha maneno.
 
Hivi ni yule Pole Pole aliekua mwenezi wakati wa JPM?
Ndiye yeye mzee wa V8. Ndiyo maana kwa sasa hakuka pa kushika. Huku Sukuma gang kule wahuni katikati Chauma. Ujinga ujinga kama huu unaweza sababisha wazee wa Ubwabwa wakashika madaraka kama ilivyokuwa kwa Jiwe kuwa Rais
 
Kwa Mufti wa wenzetu kule, akina Takbiir!, unaweza kung'amua ni kwanini yupo kimya; ila kwa huyu wa kwetu, Mhashamu sana, Mkuu sana, kulikoni hasemi chochote? Mimi kwa kweli huwa naonaga picha zake tu, halafu natamani sana aseme neno, lakini simsikii kabisa kabisa akisema neno - akitema cheche!

Na sio maneno mengi wala, kiongozi mwenye ukubwa kama yeye, ni maneno kidoogo tu, baaaasi! Unaunguza mtandao mzima wa mapori tengefu, cheche!

Kumbe mimi nisingekuwa Padri mzuri, japo nilitabiriwa kuwa padri, maana napenda sana kuongea, na sio maneno matupu tu, bali, ni cheche! Najua mnajua naongea kitu gani haswa: cheche! Hata Padri Kitima alivyoshambuliwa, nilitegemea kuziona cheche!

Nikiyasema haya, linanijia jina la Laurent Mwonsengwo Pasinya, huyu alikuwa ni Padri huko Congo DRC ambaye alikuja kuwa Kadinali. Enzi za maisha yake, huyu mkuu sana, alikuwa anawatemea sana cheche na moto, viongozi wa Congo DRC waliotaka kubagaza haki za raia na demokrasia. Alimpa shuruba sana Mobutu Seko Kuku Ngwendu wa Zebanga, na pia alimtemea sana cheche Joseph Kabila alipotaka kuupora uchaguzi wa 2011 huko Congo.

Wakati utawala wa Mobutu Seko ukikaribia ukingoni, ni Mwonsengwo Pasinya aliyeaminiwa na wacongo kushika nyadhifa kubwa kwenye serikali ya mpito kama: President of the Sovereign National Conference mwaka 1991, president of the High Council of the Republic mwaka 1992, na speaker of a Transitional Parliament mwaka 1994.

Najiuliza swali: Ikiwa Kadinali wetu hatemi cheche, je, ataweza kuvivaa viatu vya Mwonsengwo Pasinya? Au, ya Pasinya tumuachie Pasinya?

Cheche zipo wapi cheche?
MC
Mtu mzito huyo, hahangaiki na takataka za katibu mnyaturu-kitima
 
L

🤣🤣🤣 lkn ukipewa kifuu ukavunje njia panda au yanapogeuzia magari kwamba maisha yako yatakuwa kitonga utapandishwa cheo unaenda mbioooooooo
Sipo huko kabisa mkuu ,mimi siwezi kuishi maisha ya Giza ,mimi ni msomi!! Naamini katika scientific research over, itakuwa wewe ndo unavunja vifuu ndo unafikiri na wengine pia??🤔🤔
Mwakani utaenda kwenye ibada ya kumtupia mawe Shetani??🤣🤣🤣

Yaani mawe yaleyale, mnatupia sehemu ileile, na mwakani mnauziwa Tena mawe yaleyale 🤔🤔🤣 ama kweli ujinga ni mzigo Mkubwa sana 🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Mtu mzito huyo, hahangaiki na takataka za katibu mnyaturu-kitima
Watu hamjaelewa cheche ni nini. Cheche ni cheche! Cheche sio maneno maneno.

Yeye aongee ya kwake sio lazima arudie ya Kitima.
 
Sipo huko kabisa mkuu ,mimi siwezi kuishi maisha ya Giza ,mimi ni msomi!! Naamini katika scientific research over, itakuwa wewe ndo unavunja vifuu ndo unafikiri na wengine pia??🤔🤔
Mwakani utaenda kwenye ibada ya kumtupia mawe Shetani??🤣🤣🤣

Yaani mawe yaleyale, mnatupia sehemu ileile, na mwakani mnauziwa Tena mawe yaleyale 🤔🤔🤣 ama kweli ujinga ni mzigo Mkubwa sana 🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Hahahahaaa wewe hujui huku usomini watu ndo wanaongoza kupigana makombora 🤣🤣🤣 uliza utapewa story lukuki
 
Back
Top Bottom