Swali chechefu: Sijawahi kumsikia Kadinali Rugambwa akitema cheche hata kiduchu tu. Kwani kuna shida?

Swali chechefu: Sijawahi kumsikia Kadinali Rugambwa akitema cheche hata kiduchu tu. Kwani kuna shida?

Nakubali, baraza la Tec lilianza vikao vyake zamani sana hata kabla ya Nyerere kuzaliwa.

Lakini haya yote ndo yamzuie Kadinali kutema cheche? Au, hana haja ya kufanya hivo kwakuwa anajua kila kitu?
Kwanza jiulize Kardinali anatoka Shirika gani ndani ya Kanisa Moja Takatifu la Mitume

Jibu utakalopata litakupunguzia tashwishwi ya kujiuliza uliza

Katoliki ni Dude kubwa Bakwata unaweza kuikuta humo humo 😂😂✔️
 
Nakubali, baraza la Tec lilianza vikao vyake zamani sana hata kabla ya Nyerere kuzaliwa.

Lakini haya yote ndo yamzuie Kadinali kutema cheche? Au, hana haja ya kufanya hivo kwakuwa anajua kila kitu?
Tatizo lako huelewi hata unachokiandika.

Hakuna miongozi mkuu wa kanisa katoliki Tanzania.

Maaskofu wote wa majimbo yote wana hadhi sawa, kwenye baraza la maaskofu wana Rais wao na Katibu wao siyk Askofu ni Padre.

Ukadinali ni mjumbe wa Conclave, haina maana kwamba Kadinali ana hadhi kuliko maaskofu wenzake, unatakiwa kufahamu Uaskofu ni cheo cha juu maana hata Padre anaweza kiteuliwa kuwa Kadinali akawa mjumbe wa Conclave na imeshafanyika kwa mapadre wa ulaya kuteuliwa kuwa makadinali lakini siyo maaskofu.

Kwahiyo Askofu ndio cheo cha juu na maaskofu wote wakatoliki wana hadhi sawa usifananishe na Lutheran kuwa na Askofu mkuu Malasusa, Kanisa Katoliki hakuna Askofu mkuu.
 
Kwa Mufti wa wenzetu kule, akina Takbiir!, unaweza kung'amua ni kwanini yupo kimya; ila kwa huyu wa kwetu, Mhashamu sana, Mkuu sana, kulikoni hasemi chochote? Mimi kwa kweli huwa naonaga picha zake tu, halafu natamani sana aseme neno, lakini simsikii kabisa kabisa akisema neno - akitema cheche!

Na sio maneno mengi wala, kiongozi mwenye ukubwa kama yeye, ni maneno kidoogo tu, baaaasi! Unaunguza mtandao mzima wa mapori tengefu, cheche!

Kumbe mimi nisingekuwa Padri mzuri, japo nilitabiriwa kuwa padri, maana napenda sana kuongea, na sio maneno matupu tu, bali, ni cheche! Najua mnajua naongea kitu gani haswa: cheche! Hata Padri Kitima alivyoshambuliwa, nilitegemea kuziona cheche!

Nikiyasema haya, linanijia jina la Laurent Mwonsengwo Pasinya, huyu alikuwa ni Padri huko Congo DRC ambaye alikuja kuwa Kadinali. Enzi za maisha yake, huyu mkuu sana, alikuwa anawatemea sana cheche na moto, viongozi wa Congo DRC waliotaka kubagaza haki za raia na demokrasia. Alimpa shuruba sana Mobutu Seko Kuku Ngwendu wa Zebanga, na pia alimtemea sana cheche Joseph Kabila alipotaka kuupora uchaguzi wa 2011 huko Congo.

Wakati utawala wa Mobutu Seko ukikaribia ukingoni, ni Mwonsengwo Pasinya aliyeaminiwa na wacongo kushika nyadhifa kubwa kwenye serikali ya mpito kama: President of the Sovereign National Conference mwaka 1991, president of the High Council of the Republic mwaka 1992, na speaker of a Transitional Parliament mwaka 1994.

Najiuliza swali: Ikiwa Kadinali wetu hatemi cheche, je, ataweza kuvivaa viatu vya Mwonsengwo Pasinya? Au, ya Pasinya tumuachie Pasinya?

Cheche zipo wapi cheche?
MC
Cheche zipi uzitarajiazoo?
 
Tatizo lako huelewi hata unachokiandika.

Hakuna miongozi mkuu wa kanisa katoliki Tanzania.

Maaskofu wote wa majimbo yote wana hadhi sawa, kwenye baraza la maaskofu wana Rais wao na Katibu wao siyk Askofu ni Padre.

Ukadinali ni mjumbe wa Conclave, haina maana kwamba Kadinali ana hadhi kuliko maaskofu wenzake, unatakiwa kufahamu Uaskofu ni cheo cha juu maana hata Padre anaweza kiteuliwa kuwa Kadinali akawa mjumbe wa Conclave na imeshafanyika kwa mapadre wa ulaya kuteuliwa kuwa makadinali lakini siyo maaskofu.

Kwahiyo Askofu ndio cheo cha juu na maaskofu wote wakatoliki wana hadhi sawa usifananishe na Lutheran kuwa na Askofu mkuu Malasusa, Kanisa Katoliki hakuna Askofu mkuu.
Lakini unajua Mungu kutupatia mdomo ni kwamba tuutumie kusema. Nakubali kwamba werevu husikiliza sana badala ya kusema. Ila angekuwa walau akizitema cheche, kidogo ingetikisa pahala fulani. Ni mtizamo wangu tu, wala sitaki awe ropo ropo kama Gwajima au Polepole!
 
Kwanza jiulize Kardinali anatoka Shirika gani ndani ya Kanisa Moja Takatifu la Mitume

Jibu utakalopata litakupunguzia tashwishwi ya kujiuliza uliza

Katoliki ni Dude kubwa Bakwata unaweza kuikuta humo humo 😂😂✔️
Duh! Unanitisha mkuu sana, ninalijua shirika hilo, kama ndilo unalolimaanisha, hakika nitaacha kuhoji habari hizi!
 
Back
Top Bottom