Manara ni Mtanzania, na amefungiwa ndani na nje ya nchi. Najiuliza kama angefungiwa ndani ya nchi pekee na ikatokea amepata dili kuwa msemaji/mhamasishaji wa Gor-mahia ya Kenya, hamuoni kama haya makosa yake yangejirudia huko katika nchi za kigeni. Si angetutia aibu huyu. Mi naona ni sawa tu kufungiwa ndani na nje ya nchi, kwanza hana washauri wazuri, pili yeye anajiona ndio kila kitu kushinda TFF hata Serikali. Yani kajiumaarufu na vituko bwerere. Ifikie mahali tuheshimu mamlaka ya TFF. Ingekuwa Serikali ndio msimamizi wa Mpira na lingetokea hili kwa Manara kusingekuwepo na wakisema Fyoko.
Nakumbusha Manara ni Mtanzania na TFF ina haki ya kumfungia ndani ya nchi na nje ya nchi.
Kwa mfano kama ingetokea Senzo Mazingiza ndio angefungiwa, basi angefungiwa Tanzania peke yake, kwa sababu Senzo sio Mtanzania, kwakwahiyo angekuwa na haki ya kuendelea na kazi zake nje ya Tz.
Nawasisha.