Kwanza pole!, pili dalili za udikiteta ni jambo moja, na Udikteta halisi ni jambo jingine!.
Kwa Tanzania mahali tulipofikia, hadi kuwa shamba la bibi, tulihitaji mtu kama Magufuli, na matokeo tumeyaona, ndani ya miaka 5, tumeuaga umasikini na kuwa nchi ya uchumi wa kati!.
Tukumpa mitano mingine, tunakwenda kuwa nchi ya uchumi wa kati mkubwa, na tukibadili katiba aendelee tuu,Tanzania tunakwenda kuwa nchi ya uchumi mkubwa, nchi tajiri, a donor country.
Fuatilieni utawala wa Tiger Nations, bila udikiteta, zisinge toka!. Sio kila udikiteta ni udikiteta mbaya, au udikiteta katili, kuna udikiteta wa kizalendo unaitwa, benevolence dictatorship!, hivyo rais Magufuli ni dikiteta Mzalendo anayefanya udikiteta kwa nia njema kulikomboa taifa!.
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!
P