Swali Fyatu la Mwezi: Wakimpa Sifa Zake, Watapunguza za Kwao?

Swali Fyatu la Mwezi: Wakimpa Sifa Zake, Watapunguza za Kwao?

Mkubwa

Ni kweli kabisa Rais Magufuli kafanya mengi, mazuri sana na mabovu sana
Tatizo lipo hapo, ni wakati gani Marehemu anatajwa na wakati gani aachwe apumzike

Nashuri waendelee kumkwepa! ili apumzike na wasifungue ''can of worms''

JokaKuu
Kwa mazuri yake msifieni na kwa mabaya yake msemeni,mnaogopa nini?...kwamba uwanja umeshainama mpaka dakika hii so bora asitajwe tu kabisaaa...basi sawa!!
 
Kumsifia jiwe kunahitaji mtu kuwa na roho ya usherani
Badala ya kujibu swali fyatu, umeenda Kutukana Jamii nzima ya Mtanzania na Mwafrika kwa Ujumla.

Haya magamba ya kondoo mnayojivika, yanaonekana waziwazi. Yaani kwa Lugha yako mtu yeyote anaemsifia Hayat Rais J.P.M ana roho ya shetani! Kwa muono wako huo tuna wanafiki wengi Nchi hii in Biblical proportion!

.....nakushauri utafute Script nyingine tu, hiyo uliyotumia sio tu haina ukweli, bali imekosa uhalali wa kutumika.
 
Kutoka moyoni kabisa, jiwe ameirudisha nchi hii miaka 50 nyuma . Ameinajisi nchi hii kiasi kwamba ktk muda wa miaka 5 amejenga nyufa za kijamii, kisiasa na kiuchumi

Matatizo ya kiuchumi tunayopitia Sasa yametengenezwa na jiwe. Aliwachukia wafanyabiashara kwa kiasi kikubwa hata akatamaka hadharani kuwa wataishi kama mashetani.

Kauli ya kishenzi na kifedhuli kabisa. Mpuunzi mkubwa huyu. Hakujua kuwa hawa ndiyo miyo ya uchumi na watoa ajira wakubwa. Ndiyo mpk leo mama anahangaika kuurejesha uchumi ktk mstari.

Kijamii na kisiasa kila mtu anajua jinsi jiwe alivyoivua nguo nchi hii. Kwahiyo siandiki kitu.

Kumsifia jiwe kunahitaji mtu kuwa na roho ya usherani
Brother utaongea yoyote lakini ukweli ulio wazi Magufuli ameacha athari chanya kubwa sana.
 
Una uhakika hawakufanya? Na kama wangekuwa hawajafanya chochote, hii nchi ingekuwepo hapa tulipo?

Unayafahamu mambo yote aliyoyafanya Nyerere tangu alipoichukua nchi kutoka kwa Wakoloni?

Tatizo mnalazimisha wote tuamini kama huyo JPM wenu alikuwa ni the best, kumbe wengine tunamuona alikuwa ni the worst.
Kuna sehemu kwenye jibu langu nimeandika wengine hawajafanya chochote? ni vyema ukapunguza MIHEMKO kwanza then ndio ujibu......hakuna anayekulazimisha umuone alikuwa 'the best' wewe endelea kuona alikuwa 'the worst' na sisi wengine tuendelee kuona alikuwa ' the best wala hakunaga shida
 
View attachment 2642893
Na. M. M. Mwanakijiji

Kuna watu ambao tunawakumbuka kwa umahiri na weledi katika kazi, vipaji au matendo yao. Michael Jordan aliichezea timu ya mpira wa vikapu ya Chicago Bulls na kujionesha kuwa ni mchezaji bora Zaidi wa mchezo huo duniani. Wengi wanalijua jina la Michael Jordan lakini ni wachache wanaweza kukutajia majina ya wachezaji wenzake wanne waliokuwa wanaunda kikosi cha kwanza. Hili pia ni kweli kuhusu mchezaji bora Zaidi wa soka duniani Pele. Wengi wanalijua na kukumbuka jinsi Pele alivyoongoza Brazili kwenye makombe ya dunia. Ni wachache sana wanaweza kukutajia wachezaji kumi wengine walioshinda na Pele kombe la dunia mara ya mwisho.

Hata hapa Tanzania kuna watu wanakumbukwa kwa umahiri wao lakini ni wachache wanaweza kukutajia majina ya watu wengine kwenye vikosi vyao. Mbaraka Mwinshehe, Marijan Rajabu, au hata Remmy Ongara. Tunajua nyimbo zao, tumewahi kuzisikia lakini tukiuliza wana bendi wenzao ni kina nani ni wachache wanaweza kutaja hata majina mawili.

Ukweli ni kuwa kuna watu wanatokea katika fani mbalimbali na wanakuwa vinara na bora kuliko wengine. Tunapowataja hawa wengine na kuwasifia haina maana tunadharau mchango wa wengine. Ukimtaja Lionel Messi kwa mfano au Cristiano Ronaldo mara moja watu watajua unawazungumzia kina nani lakini ni wachache wanaweza kukutajia majina ya wachezaji wenzao kwenye zile timu zilizokuza majina yao. Unaposema sifa za vinara haina maana unafuta sifa au unadharau sifa za wengine!

Juzi wakati wa uzinduzi wa Ikulu mpya ya Dodoma ambayo sasa inaifanya Ikulu ya Dar-es-Salaam kuwa Ikulu Ndogo kuna watu walisimama na kumwaga sifa mbalimbali. Niliamka mapema (huku niliko) niweze kushuhudia kama watakuwa na ujasiri wa kumtaja mchezaji kinara aliyewafanya wawepo pale siku ile. Bahati mbaya karibu kila aliyesimama ama alinyemelea kulitaja jina la mchezaji huyo bora au alilitaja kama kulipita tu kuwa “alikuwa ni mmoja wa timu”.

Jina la Joseph Pombe Magufuli, kinara wa marais wote waliowahi kutokea Tanzania, shujaa wa uthubutu, na mbunifu wa maono ya maendeleo ya haraka lilitajwa kana kwamba na yeye alikuwa na mchango kama wengine tu. Yote hiyo ilifanywa kwa makusudi kabisa wakijaribu kufifisha jina hilo na hawakutaka kusikia makofi na shangwe ambazo wangelitendea haki zingesikaka. Waliogopa kuona kuwa yumkini huyu bwana akiwa amelala kaburini milele kuna watu wanamkumbuka na kummiss!

Wanatuambia kuwa mpango wa kuhamishia Ikulu ulianza toka miaka ya sitini na hatimaye maamuzi yakachukuliwa na taratibu hatua mbalimbali zilianza kuchukuliwa ili kuhamia taratibu Dodoma. Jakaya Kikwete akatupa stori kuwa aliagiza watu waende Malaysia waone mambo yanavyofanyika huko na sisi tuje kuiga. Sikumbuki kwa miaka kumi ya Kikwete kama kuna siku ulifanyika mjadala hata mmoja Bungeni wa jinsi ya kuhamia Dodoma na kujenga Ikulu Dodoma na kuwa aliwaambia Watanzania kuwa ametuma iende Malaysia! Sijui hiyo timu iliongozwa nan ani! Lakini tunakubali.

Tunaambiwa kuwa viongozi wote waliotangulia wamekuwa wakifanya kama kupokezana vijiti kuliongoza taifa. Wanasahau kuwa Magufuli hakumwachia Samia kijiti; kamwachia gogo! Ni wazi Rais Samia anajitahidi kwa uwezo wake wote kuonekana anaweza kukamilisha miradi hii yote; na kweli tunaona ikimalizwa. Lakini ndugu zetu hawa wanataka tuamine kuwa kama Magufuli asingefanya alivyofanya leo tungekuwa na Ikulu Dodoma au Mji wa Serikali, au miradi hii mingine mikubwa siyo tu ya kimkakati kama inavyoitwa bali ya uthubutu uliopitiliza.

Yaani, kwa miaka Zaidi ya arobaini hawa jamaa walishindwa kuhamia Dodoma walikuwa wanalipia vipindi vya CDA hata sijui tulikuwa tunaambiwa nini. Kwa miaka arobaini walikuwa wanajipanga, na kuandaa ramani, na kuandaa warsha na semina. Kwa miaka arobaini wanaenda Dodoma, usiku usiku wanawahi kurudi Dar, kwa miaka arobaini wanaimba “Dodoma Dodoma” lakini kila wakiama ni “Dar, Dar”.

Akaja Magufuli akasema maneno matupu hayaliwi na upepo haufungwi kanga! Akawakimbiza mchakamchaka watu wazima na majasho hadi kwenye kucha; mambo yakaanza Kwenda. Yaani, yaliyowashindwa kwa miaka arobaini mtu kayaweza kuyasukuma kwa miaka mitano! Halafu wanatuambia “na sisi tulicheza”. Wanasema kweli Pele alifunga goli lakini sisi tulitoa pasi; wanasema Lionel kachukua kombe la dunia lakini sisi tulimbeba! Hatutaki kuwakumbuka!

Sasa wameamua tu kuwa hawamtaja Magufuli kwa sifa zake; hawatamtaja kwa uthubutu wa barabara, meli, mashule, madaraja. Yaani, kuna watu walijenga daraja moja kubwa kwa miaka kumi halafu anakuja mtu anajenga Matano wanajilinganisha naye! “Na sisi tulijenga barabara na sisi tulijenga daraja” msimpe sifa sana yule; alikuwa ati wa kawaida tu. Ni wivu gani huu?

Hivi kweli wakisema sifa za Magufuli kwa haki kabisa, na kusema kuwa alikuwa ni mchezaji nyota wao watapunguziwa sifa zao? Hivi watakapoenda kuwasha umeme wa Bwawa la Nyerere si wataanza kutupigisha stori tena kama za Ikulu! “Oh hili wazo lilikuwa la Nyerere, na sisi wengine tukapokezana vijiti”! Hivi mkimpa sifa Magufuli anazostahili nyinyi mtapungukiwa? Mtaonekana mnamshusha Samia? Au Samia mwenyewe anaweza kuona wivu badala ya kuona Fahari kuwa alikuwa ni sehemu ya miaka mitano ya Magufuli.

Ndio maana ile sauti anayoisikia Rais Samia haikomi. Itaendelea kumlilia na kumkumbusha kutimiza miradi lakini aifanye kwa haki isiwe kana kwamba anaona ana kivuli cha Magufuli. Magufuli akishangiliwa haina maana nay eye hatoshangiliwa; sifa za Magufuli zikiimbwa haina maana za kwake na timu yake hazitaimbwa. Ikulu ya Dodoma wangeachiwa haya ingekuja 2050! Labda wajukuu zao ndio wangeweza kuthubutu! Kama kwa miaka arobaini walichofanikiwa ni kile kilichokuwepo kabla ya Magufuli basi hawa wangeendelea kutenga bajeti ya kula tu kwa kisingizio cha kupanga makao makuu.

Hili ni swali la kwani wakimpa sifa Magufuli wao watapungukiwa naamini bado linahitaji majibu muafaka kwa wakati huu. Ni swali ambalo kama halitajibiwa vyema basi tutajikuta tunaendelea kuliuliza hata kama ni kwa kung’ong’a. Lakini kama siyo wivu, kama siyo kisirani, kama siyo kukereka na kivuli cha Magufuli basi ndugu zetu hawa waanze kuwa wa kweli; mnyonge mnyongeni sifa zake mpeni; hata kama mnaona zinawapunguzia zenu. Siyo ndivyo haki yenyewe hiyo.

Kwa hiyo basi natangaza hadharani, Ikulu na uamuzi wa kuharakisha kuhamia Dodoma sasa hivi na maendeleo yote ya ujenzi tunayoyaona ni matokeo ya uthubutu, maono, na kujituma kwa Rais wa Awamu ya Tano John Joseph Pombe Magufuli. Mchango wake haulinganishwa na Rais mwingine yeyote kabla yake na baada yake. Anayebisha asimame. Wangekuwa na uwezo na uthubutu huo; wangekuwa wamehamia Dodoma miaka 40 nyuma!

Niandikie:klhnews@gmail.com
Asante sana mwanakijiji kwa wema wako dhidi ya ukweli kuhusu hayati Magufuli,mungu akubariki sana
 
Haikua rahisi watu kama hawa kumtaja Magufuli kwa namna hii.

Hakuna jinsi kila mtu atamtaja Magufuli kila mmoja kwa wakati wake, lakini atatajikana kwa wema tu.
 
Nadhani ifike sehemu tuachane na huu mjadala wa hayati JPM. Tusilazimishane kusifia wakati kuna mambo kwenye utawala wake yalikuwa mabaya kupitiliza. Umoja wa kitaifa una thamani kuliko hayo majengo na madaraja aliyojenga. Huwezi kubomoa umoja wa kitaifa uliodumu kwa zaidi ya miaka 50 kisa unajenga daraja, barabara au majengo. Sasa hivi Rais anahangaika na maridhiano kwa kosa la aliyemtangulia kushindwa kuheshimu umoja wetu. Hakuna rais wa Tanzania aliyewahi kuwatisha wakurungenzi kwenye ishu za uchaguzi. Wote waliheshimu sana haki za wote bila kujali itikadi. Ilifika sehemu waziri anamwita Rais Mungu. Tungeendelea kuwa naye tungekuwa na majengo, madaraja, na miundombinu mizuri ila umoja wetu ungezidi kuharibika.
 
Kusema Magu ndiye kinara wa marais wote waliowahi kutokea Tz ni uongo mtupu.
Miaka arobaino ni nini bwana hata Waisraeli walitumia miaka hiyo kutoka Cairo hadi Jerusalem
 
Kutoka moyoni kabisa, jiwe ameirudisha nchi hii miaka 50 nyuma . Ameinajisi nchi hii kiasi kwamba ktk muda wa miaka 5 amejenga nyufa za kijamii, kisiasa na kiuchumi

Matatizo ya kiuchumi tunayopitia Sasa yametengenezwa na jiwe. Aliwachukia wafanyabiashara kwa kiasi kikubwa hata akatamaka hadharani kuwa wataishi kama mashetani.

Kauli ya kishenzi na kifedhuli kabisa. Mpuunzi mkubwa huyu. Hakujua kuwa hawa ndiyo miyo ya uchumi na watoa ajira wakubwa. Ndiyo mpk leo mama anahangaika kuurejesha uchumi ktk mstari.

Kijamii na kisiasa kila mtu anajua jinsi jiwe alivyoivua nguo nchi hii. Kwahiyo siandiki kitu.

Kumsifia jiwe kunahitaji mtu kuwa na roho ya usherani
Wewe ni homo sexual? Nakuelewa lazima umchukie Magufuli. Nakumbuka aliwanyanya sana nyie mashoga. Kwa kweli nakuelewa sana. Now angalau mnaishi kwa amani.
 
Back
Top Bottom