Swali Fyatu la Mwezi: Wakimpa Sifa Zake, Watapunguza za Kwao?

Swali Fyatu la Mwezi: Wakimpa Sifa Zake, Watapunguza za Kwao?

Shida ni low intelligence na underperformance ndiyo maana wanaiba na kupora kazi na jasho la wengine, unajiuliza Tanzania ni nchi inayoendelea kuna mambo mengi wanaweza kufanya sasa hivi na kujivunia lkn hawafanyi chochote daraja la Salenda walisema ni wao, hata la Busisi wanasema ni wao wamejenga, Stiegler ilikuwepo miaka yote hakuna aliyethubutu kujenga kaja mwamba kajenga leo hii wanajisifia wanasema ni wao wamejenga, shida ni hiyo hapo juu hawaoni kingine wanachoweza kufanya wanaishia kupora kazi za wengine, Mgufuli alikuwa anaibua mambo ambayo watu hata walikuwa hawaelewi, aliwezaje? Jibu ni intelligence, hiyo ndiyo tofauti, …
 
View attachment 2642893
Na. M. M. Mwanakijiji

Kuna watu ambao tunawakumbuka kwa umahiri na weledi katika kazi, vipaji au matendo yao. Michael Jordan aliichezea timu ya mpira wa vikapu ya Chicago Bulls na kujionesha kuwa ni mchezaji bora Zaidi wa mchezo huo duniani. Wengi wanalijua jina la Michael Jordan lakini ni wachache wanaweza kukutajia majina ya wachezaji wenzake wanne waliokuwa wanaunda kikosi cha kwanza. Hili pia ni kweli kuhusu mchezaji bora Zaidi wa soka duniani Pele. Wengi wanalijua na kukumbuka jinsi Pele alivyoongoza Brazili kwenye makombe ya dunia. Ni wachache sana wanaweza kukutajia wachezaji kumi wengine walioshinda na Pele kombe la dunia mara ya mwisho.

Hata hapa Tanzania kuna watu wanakumbukwa kwa umahiri wao lakini ni wachache wanaweza kukutajia majina ya watu wengine kwenye vikosi vyao. Mbaraka Mwinshehe, Marijan Rajabu, au hata Remmy Ongara. Tunajua nyimbo zao, tumewahi kuzisikia lakini tukiuliza wana bendi wenzao ni kina nani ni wachache wanaweza kutaja hata majina mawili.

Ukweli ni kuwa kuna watu wanatokea katika fani mbalimbali na wanakuwa vinara na bora kuliko wengine. Tunapowataja hawa wengine na kuwasifia haina maana tunadharau mchango wa wengine. Ukimtaja Lionel Messi kwa mfano au Cristiano Ronaldo mara moja watu watajua unawazungumzia kina nani lakini ni wachache wanaweza kukutajia majina ya wachezaji wenzao kwenye zile timu zilizokuza majina yao. Unaposema sifa za vinara haina maana unafuta sifa au unadharau sifa za wengine!

Juzi wakati wa uzinduzi wa Ikulu mpya ya Dodoma ambayo sasa inaifanya Ikulu ya Dar-es-Salaam kuwa Ikulu Ndogo kuna watu walisimama na kumwaga sifa mbalimbali. Niliamka mapema (huku niliko) niweze kushuhudia kama watakuwa na ujasiri wa kumtaja mchezaji kinara aliyewafanya wawepo pale siku ile. Bahati mbaya karibu kila aliyesimama ama alinyemelea kulitaja jina la mchezaji huyo bora au alilitaja kama kulipita tu kuwa “alikuwa ni mmoja wa timu”.

Jina la Joseph Pombe Magufuli, kinara wa marais wote waliowahi kutokea Tanzania, shujaa wa uthubutu, na mbunifu wa maono ya maendeleo ya haraka lilitajwa kana kwamba na yeye alikuwa na mchango kama wengine tu. Yote hiyo ilifanywa kwa makusudi kabisa wakijaribu kufifisha jina hilo na hawakutaka kusikia makofi na shangwe ambazo wangelitendea haki zingesikaka. Waliogopa kuona kuwa yumkini huyu bwana akiwa amelala kaburini milele kuna watu wanamkumbuka na kummiss!

Wanatuambia kuwa mpango wa kuhamishia Ikulu ulianza toka miaka ya sitini na hatimaye maamuzi yakachukuliwa na taratibu hatua mbalimbali zilianza kuchukuliwa ili kuhamia taratibu Dodoma. Jakaya Kikwete akatupa stori kuwa aliagiza watu waende Malaysia waone mambo yanavyofanyika huko na sisi tuje kuiga. Sikumbuki kwa miaka kumi ya Kikwete kama kuna siku ulifanyika mjadala hata mmoja Bungeni wa jinsi ya kuhamia Dodoma na kujenga Ikulu Dodoma na kuwa aliwaambia Watanzania kuwa ametuma iende Malaysia! Sijui hiyo timu iliongozwa nan ani! Lakini tunakubali.

Tunaambiwa kuwa viongozi wote waliotangulia wamekuwa wakifanya kama kupokezana vijiti kuliongoza taifa. Wanasahau kuwa Magufuli hakumwachia Samia kijiti; kamwachia gogo! Ni wazi Rais Samia anajitahidi kwa uwezo wake wote kuonekana anaweza kukamilisha miradi hii yote; na kweli tunaona ikimalizwa. Lakini ndugu zetu hawa wanataka tuamine kuwa kama Magufuli asingefanya alivyofanya leo tungekuwa na Ikulu Dodoma au Mji wa Serikali, au miradi hii mingine mikubwa siyo tu ya kimkakati kama inavyoitwa bali ya uthubutu uliopitiliza.

Yaani, kwa miaka Zaidi ya arobaini hawa jamaa walishindwa kuhamia Dodoma walikuwa wanalipia vipindi vya CDA hata sijui tulikuwa tunaambiwa nini. Kwa miaka arobaini walikuwa wanajipanga, na kuandaa ramani, na kuandaa warsha na semina. Kwa miaka arobaini wanaenda Dodoma, usiku usiku wanawahi kurudi Dar, kwa miaka arobaini wanaimba “Dodoma Dodoma” lakini kila wakiama ni “Dar, Dar”.

Akaja Magufuli akasema maneno matupu hayaliwi na upepo haufungwi kanga! Akawakimbiza mchakamchaka watu wazima na majasho hadi kwenye kucha; mambo yakaanza Kwenda. Yaani, yaliyowashindwa kwa miaka arobaini mtu kayaweza kuyasukuma kwa miaka mitano! Halafu wanatuambia “na sisi tulicheza”. Wanasema kweli Pele alifunga goli lakini sisi tulitoa pasi; wanasema Lionel kachukua kombe la dunia lakini sisi tulimbeba! Hatutaki kuwakumbuka!

Sasa wameamua tu kuwa hawamtaja Magufuli kwa sifa zake; hawatamtaja kwa uthubutu wa barabara, meli, mashule, madaraja. Yaani, kuna watu walijenga daraja moja kubwa kwa miaka kumi halafu anakuja mtu anajenga Matano wanajilinganisha naye! “Na sisi tulijenga barabara na sisi tulijenga daraja” msimpe sifa sana yule; alikuwa ati wa kawaida tu. Ni wivu gani huu?

Hivi kweli wakisema sifa za Magufuli kwa haki kabisa, na kusema kuwa alikuwa ni mchezaji nyota wao watapunguziwa sifa zao? Hivi watakapoenda kuwasha umeme wa Bwawa la Nyerere si wataanza kutupigisha stori tena kama za Ikulu! “Oh hili wazo lilikuwa la Nyerere, na sisi wengine tukapokezana vijiti”! Hivi mkimpa sifa Magufuli anazostahili nyinyi mtapungukiwa? Mtaonekana mnamshusha Samia? Au Samia mwenyewe anaweza kuona wivu badala ya kuona Fahari kuwa alikuwa ni sehemu ya miaka mitano ya Magufuli.

Ndio maana ile sauti anayoisikia Rais Samia haikomi. Itaendelea kumlilia na kumkumbusha kutimiza miradi lakini aifanye kwa haki isiwe kana kwamba anaona ana kivuli cha Magufuli. Magufuli akishangiliwa haina maana nay eye hatoshangiliwa; sifa za Magufuli zikiimbwa haina maana za kwake na timu yake hazitaimbwa. Ikulu ya Dodoma wangeachiwa haya ingekuja 2050! Labda wajukuu zao ndio wangeweza kuthubutu! Kama kwa miaka arobaini walichofanikiwa ni kile kilichokuwepo kabla ya Magufuli basi hawa wangeendelea kutenga bajeti ya kula tu kwa kisingizio cha kupanga makao makuu.

Hili ni swali la kwani wakimpa sifa Magufuli wao watapungukiwa naamini bado linahitaji majibu muafaka kwa wakati huu. Ni swali ambalo kama halitajibiwa vyema basi tutajikuta tunaendelea kuliuliza hata kama ni kwa kung’ong’a. Lakini kama siyo wivu, kama siyo kisirani, kama siyo kukereka na kivuli cha Magufuli basi ndugu zetu hawa waanze kuwa wa kweli; mnyonge mnyongeni sifa zake mpeni; hata kama mnaona zinawapunguzia zenu. Siyo ndivyo haki yenyewe hiyo.

Kwa hiyo basi natangaza hadharani, Ikulu na uamuzi wa kuharakisha kuhamia Dodoma sasa hivi na maendeleo yote ya ujenzi tunayoyaona ni matokeo ya uthubutu, maono, na kujituma kwa Rais wa Awamu ya Tano John Joseph Pombe Magufuli. Mchango wake haulinganishwa na Rais mwingine yeyote kabla yake na baada yake. Anayebisha asimame. Wangekuwa na uwezo na uthubutu huo; wangekuwa wamehamia Dodoma miaka 40 nyuma!

Niandikie:klhnews@gmail.com
Mpango mzima wa kuhamisha makao makuu ya serikali kwenda Dodoma, pamoja na kujenga Ikulu mpya, ni White Elephant Project.

Yani tumetatua tatizo ambalo halipo, wakati matatizo yaliyopo mengi tu bado hatujayatatua.

Sasa hapo kuna kipi cha kusifia?
 
Wazo na mpango wa kuhamishia makao makuu Dodoma lilikuwa moja ya makosa makubwa ya Mwl. Nyerere. Hayati Magufuli akaongeza ukubwa wa kosa kwa kutumia rasilimali za nchi (na madeni juu) kukimbilia Dodoma.

Time will tell....and prove that they were both deadly wrong. Tuombe uzima 10-15yrs from now turudi hapa kujadili faida na hasara za Dodoma kwa nchi, uchumi na hata siasa za Tanzania from actual/experiential view stand.

Tunajaribu sana kutumia hisia na propganda kupingana na ukweli rahisi lakini Dodoma - ikulu, makao makuu nk ile ni sunk cost!
 
Wazo na mpango wa kuhamishia makao makuu Dodoma lilikuwa moja ya makosa makubwa ya Mwl. Nyerere. Hayati Magufuli akaongeza ukubwa wa kosa kwa kutumia rasilimali za nchi (na madeni juu) kukimbilia Dodoma.

Time will tell....and prove that they were both deadly wrong. Tuombe uzima 10-15yrs from now turudi hapa kujadili faida na hasara za Dodoma kwa nchi, uchumi na hata siasa za Tanzania.

Tunajaribu kupingana na ukweli sana lakini Dodoma - ikulu, makao makuu nk lakini ile ni sunk cost!
Sijui watu wanasifia nini ujinga huu.

Kibaya zaidi watu wanaongeza gharama kwa safari zisizoisha za Dar - Dodoma, mpaka wamemfanya Jenerali Ulimwengu aseme mji mkuu wa Tanzania ni barabara ya kati ya Dar na Dodoma!
 
Sijui watu wanasifia nini ujinga huu.

Kibaya zaidi watu wanaongeza gharama kwa safari zisizoisha za Dar - Dodoma, mpaka wamemfanya Jenerali Ulimwengu aseme mju mkuu wa Tanzania ni barabara ya kati ya Dar na Dodoma!
Pamoja sana Kiranga.

Wanashabikia mambo yanayoliumiza taifa, maisha yao, watoto wao na yasiyo na tija kabisa! Ni wazimu mtupu!

Let's hope, one day maybe, time will teach them something
 
Hakuna aliyeweza kuhitimisha na kujibu kwa ufasaha na busara kama Mzee wetu, Rais mstaaf.....nanukuu



"...Nilipata matatizo sana ya fikra, utadhani Kijana hafi...."

"...Miongoni ya mambo aliyotuachia:Jambo la kwanza, nalo ni kubwa ni pale alipofanya kijana huyu, alipoamua kutekeleza maagizo ya Baba wetu wa Taifa Marehemu Mzee Nyerere..."

'...amewaza na kuamua tuhamie Dodoma, nakutekeleza hilo kwa miaka miwili, jambo ambalo sisi wengine tulichukua miaka arobaini, bado hatujatekeleza, amefanya jambo kubwa sana!..."


~Ali Hassan Mwinyi, Raisi mstaafu wa Tanzania.
Huyu mzee ndio maana anaishi umri wa kutosha. Ni mkweli wa dhati!
 
Mpango mzima wa kuhamisha makao makuu ya serikali kwenda Dodoma, pamoja na kujenga Ikulu mpya, ni White Elephant Project.

Yani tumetatua tatizo ambalo halipo, wakati matatizo yaliyopo mengi tu bado hatujayatatua.

Sasa hapo kuna kipi cha kusifia?
Mjadala sio faida na hasara za kuhamia Dodoma, bali watu kujivisha sifa wasizostahili kabisa. Bora wangesema ni white elephant za Magufuli tuelewe kuwa wanamalizia miradi kwavile hawana jinsi.
 
Mjadala sio faida na hasara za kuhamia Dodoma, bali watu kujivisha sifa wasizostahili kabisa. Bora wangesema ni white elephant za Magufuli tuelewe kuwa wanamalizia miradi kwavile hawana jinsi.
Huyo Magufuli na warithi wake wote wanaendeleza ujinga ule ule tu.

Sioni wapi unaanza kusifia.

Tatizo tunaendekeza siasa za team hii au ile.

Yani hata kama suala zima ni ujinga mtupu, tutashindana nani apate sifa.

Sifa za nini? Za kukamilisha ujinga?
 
Una uhakika hawakufanya? Na kama wangekuwa hawajafanya chochote, hii nchi ingekuwepo hapa tulipo?

Unayafahamu mambo yote aliyoyafanya Nyerere tangu alipoichukua nchi kutoka kwa Wakoloni?

Tatizo mnalazimisha wote tuamini kama huyo JPM wenu alikuwa ni the best, kumbe wengine tunamuona alikuwa ni the worst.
Tuko nyuma sana na mambo mengine ni ya kawaidi sana kwa viongo kuamua.
 
Kutoka moyoni kabisa, jiwe ameirudisha nchi hii miaka 50 nyuma . Ameinajisi nchi hii kiasi kwamba ktk muda wa miaka 5 amejenga nyufa za kijamii, kisiasa na kiuchumi

Matatizo ya kiuchumi tunayopitia Sasa yametengenezwa na jiwe. Aliwachukia wafanyabiashara kwa kiasi kikubwa hata akatamaka hadharani kuwa wataishi kama mashetani.

Kauli ya kishenzi na kifedhuli kabisa. Mpuunzi mkubwa huyu. Hakujua kuwa hawa ndiyo miyo ya uchumi na watoa ajira wakubwa. Ndiyo mpk leo mama anahangaika kuurejesha uchumi ktk mstari.

Kijamii na kisiasa kila mtu anajua jinsi jiwe alivyoivua nguo nchi hii. Kwahiyo siandiki kitu.

Kumsifia jiwe kunahitaji mtu kuwa na roho ya usherani
Huo uchumi upo wapi jpm kawaachia karobu 5b usd leo mmezikopa kila mahalai ni ufisadi halafu mnakuja kusema eti pesa zimeongezeka
 
Wapwani si unawajua tena na korosho zao, wanahisi wakimtaja mwamba huyu hawana chao tena japo wanajisahauliaha na kujivika miwani ya mbao wakidhani kumuua JPM kutawafanya watanzania wamtoe mihoyoni mwao ....never ever!
 
Siasa za Africa sehemu nyingi zina tatizo kubwa sana la ku revolve around personalities kuliko ku revolve around policies.

Halafu Waafrika wengi hawawezi fikra dhahania, wanataka vitu vya kuona.

Ndiyo maana watu hawawezi kuongelea fiscal responsibility, lakini ni warahisi sana kuongelea nani kajenga nini.

Ndiyo uwezo wa watu wengi ulipoishia.
 
Back
Top Bottom