Swali gumu kidogo: Kwanini Urusi iliyosambaratika na dhaifu kuliko USSR inawasumbua sana NATO?

Wewe kwa akili yako GDP ndo kila kitu et??Fuatilieni habari na mfungue macho yenu....
Hawa warussi wanaparuana na muungano wa nchi 29..wao wakiwa peke yao..hilo nalo hujui unakalia kuongelea GDP....
Wamechukua Crimea....hakuna mtu alithubutu kupambana kuichukua...wakati sie hapa Idd Amin alijaribu kuchukua kasehemu tu ka Ardhi yetu kilichofuata maelfu ya waty kufa....
Hawa watu ni almost self sufficient....wewe unasema GDP?
Marekani mwenyewe analalamika...na wameanza tena kulalamika kuhusu kuingiliwa na hawa jamaa kwenye uchaguzi....embu mwambie nchi kaa Mexico au Brazil unaowalinganisha na Waruss wafanye pia uone kiyakachowapata...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Wewe ni Dr Shika Kidd??
 
Jamaa wanasumbua popote wakitaka, kiukweli kijeshi na silaha bado wako fit sana.na kulianzisha kwao ni nukta tu wanapigana hawana cha kuloose. Hapo ndo Marekani na wenzie wanaogopa.
 
Waliokua na akili urusi na Jews hawapo Tena wameondoka, ndomaana Leo hii Russia kiuchumi gdp imezidiwa mpaka na Canada, anajua urusi ni kuwekeza kwenye Vita na silaha
Sasa mbona taifa la Israeli lenye Wayahudi wengi siyo la kwanza kiuchumi duniani ?
Halafu Urusi limeanza kuwa taifa kubwa na lenye nguvu miaka gani ?
Hebu tutoe tongotongo mkuu....
 
Sasa mbona taifa la Israeli lenye Wayahudi wengi siyo la kwanza kiuchumi duniani ?
Halafu Urusi limeanza kuwa taifa kubwa na lenye nguvu miaka gani ?
Hebu tutoe tongotongo mkuu....
By economic standards Israel wapo juu Kiasi kwamba sio muda hela yao itakuwa one of world hard currencies

Kwenye akiba ya fedha za kigeni Israel unamuweka level moja na nchi kama Switzerland denoting kwamba jamaa wanajua biashara halafu kwenye kipato cha mtu mmoja mmoja Israel yuko First World huko level moja na western Europeans
 
Waliokua na akili urusi na Jews hawapo Tena wameondoka, ndomaana Leo hii Russia kiuchumi gdp imezidiwa mpaka na Canada, anajua urusi ni kuwekeza kwenye Vita na silaha
Israel wote waliondoka Urusi?


Urusi wapo pale kwa sababu ya kiongozi wao mmoja gwiji sana halafu ana akili nyingi anaitwa Joseph Stalin sio Wayahudi

wayahudi kwani hawakuwepo nchi za Slavs ambao ni wazungu masikini?
 
Vitu vingine ni mbwe mbwe tu,kombora linaenda mala 10 zaidi ya sauti we ulisibitisha vipi?wakati mwingine haya mataifa yana nguvu za maneno tu kuogopesha watu kwenye hamna,mfano rahisi Kagame aliwahi kutupiga mkwara,kwa akili yako Kagame ana uwezo wa kuvimbisha misuri mbele ya nchi yetu Tanzania?jibu la wazi ni hakuna,kwa hiyo kuleta maneno meeeengi wala haisaidii
 
Israeli hana akiba ya mali za kigeni (Foreign Currency Assets) kiwango cha kuwekwa kwenye orodha moja na nchi kama Uswisi. Mpaka kufika mwaka 2020 Israel ana mali zenye thamani ya dola za Kimarekani Billioni 145 wakati Uswisi ana mali zenye thamani dola za Kimarekani Bilioni 850. Nadhani ulikuwa unatania tu, ulivyoleta hizo takwimu zako.

Halafu jambo la pili, kuwa na uchumi mkubwa haifanyi pesa yako ikawa ndiyo Fedha ya Kibiashara za Kimataifa (International Hard Currency), inabidi uwe na mali nyingi (Reserve Assets) ambazo zinafanya fedha yako kuwa imara kuliko mataifa mengine. Kuna nchi za Uchumi mkubwa kama Saudi Arabia lakini bado pesa zao siyo Fedha za Kibiashara. Nadhani hapa napo ulikuwa uko katika utani pia.
 
Namaanisha foreign percentage to GDP ratio

Israel ana zaidi ya asilimia 20 wakati China au Japan hawana hizo asilimia
 
wale wa Saudi si ni hela ya Mafuta

Kama Singapore hela yao ni hard currency Israel sidhani kama hawatafikia
 
Kwa hiyo wewe unayepinga unatoa ushahidi gani wa kupinga. Au ndo nawe umejisikia kuongea. Hii ni technology na imepimwa kwa speed ya angani, in Mach numbers. Wanasayansi walioweka kipimo hiki hawakuwa maandazi kama wabishi wa hapa, unashangaa kombora kwenda mara kumi ya sauti. Hiyo inawezekana kwa sasa au miaka hii ya karibuni ijayo, Russia wana Zircon hypersonic missile inaenda mpaka Mach 9 (speed mara ya tisa ya sauti).
Kuhusu ndege, hizo fighters zinazoenda Mach 3 zipo tangu miaka ya 1980.
 
Hakuna siku Israel itaweka hela yao katika umuhimu wa mzungumko wa dunia. Israel hana exchange kubwa ya kumfanya awe hata regional power sembuse globally. Majirani zake kina UAE, Saudia, Qatar wanapiga biashara ndefu na hawana kelele kwenye market.
Ushawahi ona pair ya Shekel kwenye Forex? Kuna hela za India, Turkey, Russia, South Africa, Mexico, New Zealand, Australia na nyingine nyingi ambazo haziwezi kuwa na uzito kibiashara sembuse Shekel ya Israel ambayo hata hazijulikani.
Japan ambayo ina uchumi mkubwa Yen yake almost inalingana thamani na shilingi ya Kenya, hela yao inatumika sana. Ukiambiwa taja makampuni makupwa ya Japan yapo ya kutosha, ya Israel utataja yapi? Kina Rafael Defense na IAI?
 
Kuwa na Uchumi mkubwa ni kitu kimoja, na kuifanya sarafu yako kuwa fedha ya kibiashara (Hard Currency) ni kitu kingine kabisa. Kuna sababu za msingi kabisa za kiuchumi, kimkakati na kihistoria ambazo zilisaidia Fedha ya Uingereza (Pound Sterling), Fedha ya Uswisi (Swiss Francs) na Fedha ya Marekani (United States Dollars) kuwa fedha za kibiashara (Hard Currencies). Ndiyo maana nikamuuliza ndugu yangu MASAMILA swali rahisi sana: Ni sababu zipi hufanya fedha ya nchi itumike kwenye biashara za kimataifa ? Hapa ndiyo yanakuja mambo ya umiliki wa mali ambazo zinasaidia fedha yako iwe na nguvu, mali kama dhahabu.

Uchina ndiyo yuko kwenye vita kubwa sana kuhakikisha pesa yake The Renminbi inakuwa ndiyo fedha kuu ya biashara za kimataifa. Pamoja na uchumi wake wote ule mkubwa, bado ana safari ndefu maana uchumi mkubwa pekee hausaidii, inabidi atengeneze taasisi au vyombo vya kimataifa ambavyo vitamsaidia kufanya hivyo. Marekani na washirika wake walitengeneza Bretton-Woods Institutions na Monetary Institutions nyingine ambazo zilifanikisha hili zoezi zima.

Mwisho kabisa, nchi yako inaweza kuwa na uchumi mkubwa lakini hawa wakubwa wa dunia hawawezi kuruhusu fedha yako itumike kibiashara maana italeta balaa kubwa kiuchumi duniani. Leo hii mabenki ya Marekani yanapata tenda kubwa mno kwa kutengeneza dola za kimarekani ambazo dunia yetu hii inazitumia pia kusimamia mzunguko mzima. Nchi kama Uswisi fedha yake imekuwa na nguvu vile siyo tu kwasababu ya Uchumi mkubwa, bali pia nafasi ya Uswisi katika uchumi mzima wa pesa.

Sasa ukitaka fedha yako iwe moja kati ya zile zinazotumika kwenye biashara ya dunia basi jua lazima utaleta madhara na watakuminya, tena watakuminya sana tu.

NB: Ukisoma vizuri utakuja tambua kwamba kwenye hili siasa nayo ina nafasi kubwa sana. Mkuu nikushukuru sana kwa kunisaidia kuliweka hili jambo sawia kabisa.
 
Sisi tunasiasa Mbovu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama unaona ni mbwembwe basi jaribu kuwachokoza ndo utajua mbwembwe zao ziko vipi.kawaulize IS walipigwa na mabomu gani.
 
Kuhusu Singapore unayajua makampuni gani makubwa ya kisingapore?


Hela ya Singapore (Singapore dollar au SGD) ni fully convertible free floating currency kama USD na Israel ni nchi kubwa katika eneo zaidi ya mara ishirini ya Singapore
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…