Swali gumu kidogo: Kwanini Urusi iliyosambaratika na dhaifu kuliko USSR inawasumbua sana NATO?

Russia licha ya kusambaratika lakini bado ana hazina kubwa ya Nyuklia duniani na bado ana Spheres of influence ambazo inajikuta mara kwa mara kimasirahi anazozana na nato....

Kuanguka kwa Ussr haikumaanisha ndio kaanza 0.....

chukulia mfano mzuri wa anguko la Britain as super power lakini bado ana sphere of influence kubwa tu......

Bahati mbaya kwa Russia ni bado ana migongano na Nato kimasirahi kuanzia Ukraine, Black Sea na pia Military alliance na China Pakistan nk
 
Good Observation,
Lakini Spheres of Influence za Urusi ya leo ni zipi hizo ?? Pia una uhakika kwamba Urusi na Pakistani wana ushirika wa kijeshi (Military Alliance)??
 
Good Observation,
Lakini Spheres of Influence za Urusi ya leo ni zipi hizo ?? Pia una uhakika kwamba Urusi na Pakistani wana ushirika wa kijeshi (Military Alliance)??
Kama umezisikiliza hotuba za Putin au waziri wa mambo ya nje wa Urusi....Sphere of influences za Urusi ni Nchi mwanachama wa Former USSr ambazo USA anajaribu zishawishi ziingie NATO au ziwe na sera kinyume na URUSI

Mfano Georgia Na Ukraine nk

Chinese Russia na Pakistan wana informer alliance ambayo in nature ni Anti American mfano inasemekana kuwa China kuna muda alikuwa anaisaidia Pakistan kuzi Shot down Drone za marekani zilizookuwa zina operate North Pakistan kuwa hunt Taliban.......na pia vyanzo vingine vinasema Taliban hupata sapoti pia kutoka kwa Russia.
 
Nature mtaalamu.Nature ya hawa watu,inawabeba hta baada ya kusambaratika wana nature ya ubabe.
Cha pili ni mfumo.mfumo wa kikomunisti ni moja ya mifumo thabiti long term.ingawa short term haikuinesh faida.long term iliwajenga kidogkidogo.
 
Si kweli
 
dah mkuu nyote kwa umoja wenu mbarikiwe sana,tunawafuatili na kuwafurahia sana,asanteni sana kwa niaba ya wenye shukrani.
Asante sana Mkuu taamu,kwa baraka zako ,lakini kiukweli hii mijadala inapanua sana ufahamu wa mambo kwa sababu tun ashirikishana,na mimi pia najifunza toka kwa wengine ikiwa ni pamoja na wewe,hata hivyo mambo haya tunayapata kwa kusoma kutoka majarida na makala mbalimbali,kutazama na kusikiliza habari za dunia, kusikia kwa walioshuhudia ,kushuhudia sisi binafsi,na udadisi binafsi .Wewe ni mdau mkuu.
 
Kuvunja muungano sio maana kuwa maadui,nadhani RF bado anawahitaji sana hawa Wasoviet wa zamani na wao bado wanamhitaji sana RF,kumbuka kuwa nchi nyingi sana za kisovieti ama zina raia wanaoongea kirusi ama raia wa urusi.
KGB ya sasa inawahitaji sana hawa wasovieti kwa sababu za kiuchumi na kuilinzi lakini muungano sio lazima.Ni kama vile USA anavyozihitaji nchi za South ama Latin Amerika.
 
Perestroika na Glasnosk,mageuzi na kujitazama,waliamua kupunguza matumizi baada ya wao kama vile Marekani kuwa na makambi dunia nzima kwa ajili ya ulinzi.Hata hivyo vita ya Afghan na USSR ni kama vile USSR alikua anapigana na NATO na nchi za Kiislam indirect,kwa sababu US, na baadhi ya nchi za NATO pamoja na mataifa ya kiislam Pakistani ,Saud Arabia yalikua yanawapa MUJAHEDEEN silaha ,ushauri vifaa na fedha.Ndani ya Mujahidini ndo walikuwamo Mullah, Osama,Abdul rashid Dostum,Sheikh Masound n.k.Hawa ni baadhi ya wababe waliopambana na USSR kwa msaada wa Marekani na wapammbe wake.
 
huyu malcolm lumumba huyu dah, safi sana mkuu kama ulisoma ulisoma kweli kweli,karo ya aliyokusomesha ilienda kihalali.
Mkuu taamu,kiukweli huyu Malcolm ni kisima cha elimu humu JF,huyu kama tungempata na jembe mwingine anaitwa DOTWORLD jukwaa hili hunoga sana,pamoja na wadau wengine wapo humu wanafuatilia mjadala unavyotililika tu.
 
Dunia hii hata Zanzibar tu ikiwa na silaha isiyozuilika na yoyote na inafika kokote itaingia G7. Nadhani nuclear power na uongozi imara wa Putin umeipa heshima na fursa ya kunawiri na maeneo mengi.
 
South korea chini ya rais park(baba wa rais aliyejiuzulu) ilikuwa ni nchi ya kidikteta na ndiye aliyesababisha uchumi wa korea kusini kukua.
 
Mkuu taamu,kiukweli huyu Malcolm ni kisima cha elimu humu JF,huyu kama tungempata na jembe mwingine anaitwa DOTWORLD jukwaa hili hunoga sana,pamoja na wadau wengine wapo humu wanafuatilia mjadala unavyotililika tu.
ndio mkuu apewe haki yake akisikia na akiwa hai na mwenye nguvu,amebarikiwa na sio mchoyo.
 
like
 
Nimeelimika sana hapa
 
Kama umezisikiliza hotuba za Putin au waziri wa mambo ya nje wa Urusi....Sphere of influences za Urusi ni Nchi mwanachama wa Former USSr ambazo USA anajaribu zishawishi ziingie NATO au ziwe na sera kinyume na URUSI
Mfano Georgia Na Ukraine nk
Sawa kabisa mkuu uko sawa,
Lakini unadhani ni sawa kabisa kwa hatma ya nchi ndogo kuamuliwa na mataifa makubwa ???

Nadhani Urusi na Pakistan wanashirikiana tu, lakini hawana umoja wa kujihami kijeshi. Nazungumza hivi kwasababu ya mahusiano makubwa ya Kihistoria baina ya India (Adui mkubwa wa Pakinstan) na Urusi. Nakumbuka vita ya mwaka mwaka 1971 baina ya India na Pakistan USSR alikuwa upande wa India huku Uchina akiwa upande wa Pakistan. Pia miaka 1970's Pakistan aliwasaidia sana Wamarekani na Mujahedeen kuua maelfu ya Warusi nchini Afghanistan. Hawa ni washirika tu lakini hawana umoja: Mwaka 2001 Iran ndiyo ilimsaidia Marekani kuvamia Afghanistan na kuwatoa Taliban lakini mwaka 2003 wakawa maadui.

NB: Huu ni ushirika wa kimaslahi tu na utapita....
 
Nchi yetu ya Tanzania ifanye nini ili iweze kuwa na kinu japo kimoja cha nyuklia?
Maendeleo huletwa na viongozi sababu wao ndio wenye maamuzi je unaona akina bashite jiwe wana weza kukuvusha mto wenye mamba wenye njaa kama ndio basi tuna weza kama hapana ujuwe ndio hivyo tena! sikio la kufa halisikie dawa Afrika tumesha tekwa tunaendeshwa kwa remote control!
kama dawa za kututibu tunatengenezewa na watu wenye matamanio na rasilimali zetu mkuu chanjo wana tupa wao toka tukiwa wadogo tusubiri kufa tu mkuu sisi ni simba wanao fugwa !
Huko Syria wamezima channel za YouTube za serekali sinazo onyesha mambo yanayo endelea huko Dunia ni kiza ila mchana upo!
 

La msingi unalotakiwa kuelewa ni kwamba hiyo iliyoitwa USSR au CCCP ilikuwa na tafsiri moja tu kuwa ni URUSI. Umoja kama unaoufikiri wewe haukuwepo.

Mfano mwepesi wa kueleweka ni hivi: URUSI katika umoja huo ilikuwa ni kichwa cha Treni, nchi nyingine washirika zilikuwa ni mabehewa tu yaliyovutwa na kichwa.

Kichwa kilipojikata mabehewa yakasimama na kukodi injini za mapajero kuvivuta. Kwa hiyo kichwa cha Treni ndicho kinachotazamana na NATO. Hapo unategemea nini?

Jingine la muhimu kwako kuelewa ni kwamba vile vyama vya kibaguzi vinavyokuwa Ulaya vinapinga vikali mpango wa kuiona URUSI kama adui. Wanahitaji washirikiane na Urusi kwa vile ni weupe wenzao. Kwa hivi sasa Amini usiamini Wabaguzi wa Urusi wanashangilia siku ya kuzaliwa kwa Adolf Hitler.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…