kipindi kile ndio na balehe nilikua nasoma malangali middle school iringa. Kipindi kile ilikua kupata demu si mchezo hata changudoa ulitakiwa umtongoze kama wiki mbili hadi mwezi ndio uone ndani. Du vita ilikua ishaisha tar 30.04,45 wajerumani waliposarenda lkn wajapani chini ya mfalme wao waliomlinganisha na mungu walisema mpaka kieleweke. Ndio rais truman aliyeshika usa baada ya kifo cha fdr akamuita rubani mmoja aliyeitwa paul eliot jr akadondoshe hicho kitu cha siri walichoita little boy au mvulana mtundu. Na kweli jamaa alitokea kwenye cambi ya jeshi inaitwa whiteman akaenda na msaidizi wake kumdondosha little boy mjini hiroshima. Lilipotua ardhini kuliwaka mwanga mara mia zaidi ya mwanga wa jua, kukawa na kishindo kisichoelezeka ndio moto, kwa muda wa sekunde nusu mji wa hiroshima (zaidi ya kariakoo ) ukawa haupo tena, watu walikua wanaungua kama kuni kuanzia kwenye vidole kuelekea mwilini. Waliokufa pale pale lilipotua ni watu 140,000. Yaani kama wakazi wote wa mbeya na viunga vyake. Waliokua mbali kidogo kama kimara walikua ni nyama tupu hakuna mwenye ngozi. Waliopelekwa hospitalini ilikua balaa, watu wa tiba hawakutosha, walioungua walikua wanatoa mafunza na harufu ilikua balaa. Baada ya siku tatu truman akaagiza kitu ingine ikashushwe nagasaki hili waliliita fatman , liliua watu 80,000 elfu pale pale yaani zaidi ya wakazi woote wa singida na viunga vyake. Baada ya hilo mfalme hirohito akakubali yaishe. Truman aliamini kupiga bomu la atomic kutaokoa maisha ya wengi. Kwani vita ingeisha mapema. Ikumbukwe kabla mabomu haya hayajapigwa ndege za marekani zilidondosha vikaratasi kuwaomba wajapani wa sarende lkn wajapani walisema watu wazima hawatishiwi nyau.