Swali kuhusu tabia ya kususa, kugomea au kuzira: Je, si tabia za kike, si utoto?

Mwanamke wa kususa susa ni mtamu sana.... unakuta kamesusa na kasura kake kazuri... unakabembeleza mpaka raha... utasikia usirudie tena kwa kasauti ka aibu aibu...
Katikati ya utamu anabana pua ".....lakini we huwa unaniudhi, usirudie baby....". Huu uchaguzi wa kurudiwa,kwani ni lazima mzee wa 'sawasawa' awe mshindi? Wagombea wa nafasi zingine kwa nini nao wasuse? Wanatetea utamu wa mtu moja,ila jamaa alikuwa anakamua kama makamu I wa Rais,wakati wengine wanasota,huko anang'ang'ania hamtambui Shein kama Rais. Utalii wa ndani,hakuna haja kwenda serengeti.
 
Pasco. Hili ni jukwaa la siasa lakini sioni chambe ya siasa bali social matters ambayo ungeweka kwenye jukwaa la hoja mchanganyiko.
Mkuu , mada yangu imeanza na kususa general, ingeishia kwenye kususa generally ningeiweka kwenye Jukwaa la Hoja Mchanganyiko, lakini hii mada ya kususa, nikuwa more specific kwenye kususa kisiasa, hivyo hapa kwenye Jukwaa la Siasa ni mahali pake stahiki.

Tunazungumzia kususa kwenye context ya kisiasa nikiuliza the motive behind na the the expected outcome, na sio kususa uli mradi kususa!, this is pure politics.

Pasco
 
Asante kwa viambatanisho,
 
Pasco kiukweli unatia huruma ! maana huku si kushuka wala kuporomoka , yaani sijui niseme umeserereka ? kwa ujumla hoja zako za sasa zinatia aibu , shida nini , njaa ?
Ukitimia akili za kushikiwa itakuchukuwa miaka angalau 20 kuelewa,ila ukiwa huru kifikra ni punde tu utaelewa,kususa uchaguzi si takwa la wanaCUF wa kawaida bali ni makubaliano ya Seif,EL,watu wachache ndani ya CUF na CCM.
 
Ukitimia akili za kushikiwa itakuchukuwa miaka angalau 20 kuelewa,ila ukiwa huru kifikra ni punde tu utaelewa,kususa uchaguzi si takwa la wanaCUF wa kawaida bali ni makubaliano ya Seif,EL,watu wachache ndani ya CUF na CCM.
Huna lolote , baraza kuu limeamua na mkutano mkuu umeridhia halafu unaleta uongo hapa ? shame !
 
Pasco, kususa (boycott) hapa inahusisha tu taasisi au nchi (sio hayo mambo ya kitoto na kike). Kususa ni silaha yenye nguvu kubwa inayotumika kuonyesha kutokuridhishwa na ukiukaji wa misingi ya kiimani, kifalsafa na hata kitamaduni uliofanywa na taasisi au nchi dhidi ya taasisi au nchi nyinyine. Mfano, 1976 Tanzania iliongoza nchi zingine za Kiafrika kususia michezo ya Olympic ya Montreal, Canada kutokana na kitendo cha kamati ya Olympic ya kimataifa (IOC) kukataa pendekezo la Tanzania la kutaka New Zealand iuzuiwe kushiriki michezo hiyo baada ya kuruhusu timu yake ya rugby kufanya ziara Afrika Kusini na kucheza na timu ya Makaburu. Gharama zipo! Wakati huo Tanzania ilikuwa na wanariadha mahiri waliokuwa kwenye kilele cha ubora wao ambao wangeipatia nchi angalau medali nne za dhahabu. Bayi alikuwa anashikilia ubingwa wa dunia mbio za 1500m na maili moja. Nyambui alikuwa bingwa wa Afrika 3000m. Kutoshiriki Afrika kulifanya michezo ikose msisimko na dunia kujifunza kuwa ushirikiano na Makaburu haulipi!
 
Mkuu Nginana, kwanza asante kwa elimu hii kuhusu boycott, kwenye maelezo yangu awali nilisema boycott ya watoto ni to seek attention, na boycott ya wanawake ni kutaka kubembelezwa!. Tanzania tuliposusa, zile zilikuwa ni enzi za 'cold war', sasa tuko kwenye era nyingine na dunia nyingine!. Huu sasa ni wakati wa 'result oriented decisions', na sio wakati wa kususa tuu kutaka attention, then what?, kususa bila ku achieve anything tangible is a waste!. Jee unaweza kunisaidia Tanzania tuliposusa, tuliachieve nini?!.

Politics is a game, na rules of the game zinaeleweka, kama mechi imepangwa, usipopeleka timu uwanjani, aliyepeleka timu, anapewa ushindi wa mezani!. Nimeuliza huku kususa kisiasa, kususia uchaguzi halali, lengo lake ni nini?!, what do they want to achieve?!.

Paskali
 
Ha ha
ha ha ha wengi wanatamani kutokee machafuko kisha waovu wajifiche kwenye migongo ya wananchi bila kujua serikali ina mkono mrefu na huko The Hague ni rahisi kupelekwa wao na kutengenezwa ushahidi utakao watia hatiani na ndipo ninaposema wasemaji,waamuzi,viongozi wakuu ukawa ni mawakala wa CCM...kifupi kwa sasa Cuf,Chadema nk ni matawi ya CCM.
 
Mkuu y cam, nafuatilia huku kususa kupya kulikotangazwa jana.

P.
 
Naifuatilia hoja hii.

Paskali
 
Me naona twende kibabe dawa ya moto ni moto kama mbwai mbwai kususa hakuna maana mfano upo zanzibar,kenya watu wamesusa wengine maisha yanaendelea
 
Huyu naye ameshafika bei lkn anajitahidi kuandika amufurahishe mkulu. Muda si mrefu mahusiano yake na ccm yatadhihirika. Kafulila alifiwa kule jimboni akafika bei, Mayala lilifafanuliwa maana yake kwa kisukuma nahisi naye amefika bei.
 
Mkuu ninaamini kuwa ukiingia vitani kwenye mapambano yasio kuwa na faida, ni busara kujitoa kwenye mapambano hayo ili usipoteze muda wako na resources zako. Haswa ikiwa ni dhahiri kuwa kwa namna yoyote utakavyopambana hutapata ushindi. Ni mpumbavu tu ambaye ataingia kwenye vita ambayo ana uhakika kuwa hawezi kushinda. Kujitoa kwenye mapambano inakupa muda wa kujijenga upya, kwa maana ya kudai fair play katika nyanja zote za mchuano, pasipo na mshiriki yoyote kubebwa na msamamizi au chombo chochote cha dola. Kudai mazingira kamili ya usawa kwa washiriki wote wa mchuano kwenye uwanja wa mapambano. Kususa kwa maana niliyoielezea huwezi kuiita ni tabia ya kitoto au ya kike. Kususa kwa maana yako mkuu kuna lenga zaidi, kugomea jambo, kwa sababu umeudhiwa, japo jambo hilo huwa mara nyingi na faida kwako, na hayo hufanywa na watoto na labda wakina dada kama ulivyoeleza. Hivi mkuu unaweza kuingia darasani na kufanya mtihani ambao dhahiri unajua kwamba hutafaulu? Si utapoteza energy yako na muda wako bure. Ni vema kutafakari kwa undani sababu za mtu kujitoa au kususia jambo fulani, kuliko kukimbilia kumhukumu.
 
Kumsusia mwanamke(yaani mke wa ndio) ni adhabu kubwa kwake kuliko kumpiga, sisi wahenga mke akikuletea za kuleta unampa pesa yake ya matumizi lakini wewe hauli chakula chake ni adhabu kubwa sana kwa mwanamke, ikibidi hata kumsusa yeye mwenyewe kwa muda fulani, hizo ni adhabu za wake. Tatizo vijana kujifanya kujua kwingi kutoa vipigo ndio maana ndoa hazidumu siku hizi
 

Mkuu paskali wewe ni mmoja wa great thinker mkongwe tunakueshimu sana ,umenizidi kila kitu mimi nimesoma chuo cha kata vya kuunga unga,wewe mkuu nasikia umesoma chuo nambari one Tanzania UDSM i respect you,sasa embu sema ukweli na Mungu akuone usiwe biased kuna kauli kua wakurugenzi wameambiwa wasiwatangaze wapinzani wakishinda,tumeona uchaguzi wa madiwani police wanakamata mawakala wa upinzani ndani ya chumba cha kupigia kura,wakuregenzi na ccm wanatengeneza technically kasoro ili tu kuwakomoa mawakala wa upinzani,mkurugenzi wa uchaguz mfano ubungo siku mbili kajificha ili asisaini barua za mawakala wa cdm,na akijua kua bila saini yake hawaruhusiwi kusimamia kweli hayo ndo mazingira ya uchaguz huru?ok tukubali ndio labda fomu za wakala zina upungufu kwann Nec kama msimamizi asiwaite before kuwaambia warekebishe wajaze upya then wasubmitt kuliko hii kuviziana na kuwekeana mitego,mnapowakosoa cdm kususia waambieni na ccm na nec yake wawe fair basi hata police
 
Mleta mada eti naye anajiita great thinker duh!.....

Mkuu jadili hoja, na usimjadili mleta hoja. Hoja hapo si mleta hoja kama ni GT au sio GT. Ni wapi kwenye uzi wake mtoa hoja kajiita GT? Mkuu kama wewe unajiona ndio great thinker tupe maoni yako, unaonaonaje hili swala la watu kususia jambo. Acha dharau zako za kipuuzi mkuu.
 
Mkuu Pasco acha stereotype kuhusu wanawake , wanawake ni mama zetu na generalization sio poa
 
Hivi we paskali!we hujawahi kususa au kugoma
Ndomana kuna wengine huwa wanagoma kula ilimradi matakwa Yao yatimizwe!hata Mugabe aligoma kula?tena alikuwa mwanasiasa nguli,
So kususa ni kawaida.....

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…