Swali kuhusu tabia ya kususa, kugomea au kuzira: Je, si tabia za kike, si utoto?

Binafsi walichokifanya ni sawa kama watalifikisha mwisho wake lakin watakapojirudi wenyewe afu likaisha juu kwa juu hapo ndipo kususa kunakuwa ujinga na utoto,
 
Ajabu hata mpira wenyewe hugusi yaani we unatakiwa uwepo tu uwanjani basi ukifungwa goli unachukua mpiara unaweka kati wao wanaanzisha wenyewe unafungwa goli lingine unafuata mpira unaweka kati wanaanzisha tena afu bado unaacha shughuli zako unaenda uwanjani ka sio ujinga ni nn
 
Hata chadema ikifa au turudi kwenye chama kimoja upinzani utakuwepo tu huo ndo uhalisia
 
Truth
 
I personally respect your opinions but sometimes you are completely out of scope!!
Kwa mazingira wanayopitia wapinzani ni magumu mno,kwa maoni yangu,watu wenye weledi wa kufikiri na wenye kuamini kwenye demokrasia na utawala wa sheria wangeungana na upinzani na sio kubez wala kuuliza maswali ya kinafiki(rhetoric questions)
Hakuna aliyesalama na mfumo na wala tusiwachie wapinzani??.Kwa hali ilivyo huhitaji kuhadithiwa shuruba wanazopitia wapinzani.Mimi nawaheshimu sana akina Mbowe pamoja na mapungufu yao as long wote tunamapungufu!!!
Tusibeze tukifikiri sisi hayatuhusu!!!
 
Subiri uchaguzi wa marudio bila ushiriki vyama rasmi vya upinzani kushuhudia utapeli zaidi wa ccm. Kwa akili zake mbovu chama kikongwe kitarubuni vijitu vya hovyo kabisa mitaani na kudai ndio wakilishi wa upinzani ambao wamekaidi agizo la rasmi la upinzani kutoshiriki uchaguzi.Hizo ndizo akili za master strategists wa chama kikongwe.
 
Kununuliwa siyo lazima uwe mwanachama wa chama cha siasa.Kwanza hiyo ni siri kati ya mnunuzi na mnunuliwa so usingeweza kuja hapa kukiri kununuliwa.
Pili, tume huru ni tume ya aina gani? Utakuwa kichaa kusema iliyopo Tz ni tume huru. Pascal anajitoa fahamu makusudi sijui labda anamfurahisha bwana wake. Viongozi wa Tume wameteuliwa na Raisi ambaye ni Mkiti wa Ccm wataachaje hawa kutekeleza matakwa ya aliyewateuwa. YAANI MECHI YA SIMBA NA YANGA REFA NI HAJI MANARA kisa tu eti kuna sheria 17 za soka basi Manara hawez kuwabeba simba. Ukichaa.
 
Huyu Mayalla amini usiamini kwa sasa ubongo wake uko controlled pale Lumumba. Yuko ktk mradi maalumu, kwa sasa yeye si mtanzania ni mgeni wa kinachoendelea nchini.
 
Kama kuanzia Jaji Mkuu na majaji wote wanateuliwa na rais, na bado Chadema inapata haki mahakamani, why not Tume?!. Bungeni ndani ya bunge hili kuna wabunge zaidi ya 100 wa upinzani, lakini kwenye bunge la 2020, akifanikiwa kuingia mbunge, then ni mmoja tuu Zitto!, na hii sio issue ya NEC bali Magufuli ni game changer, someni hizi nyuzi hapa chini, kitu muhimu muangalie ziliandikwa lini
Je, Kasi ya Magufuli itaua Upinzani Uchwara na Kuimarisha Upinzani Makini? - Prof. Kitila Mkumbo - JamiiForums

Trend Reading: Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je tunarejea nchi ya Chama kimoja? - JamiiForums

Swali la Ukweli Mchungu: Je, 2020 Magufuli ana mpinzani au mshindani, au Ni Magufuli tu?!. - JamiiForums

Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020? - JamiiForums

Je, CHADEMA inaweza kushinda 2020? Is it serious, credible & mature enough opposition?!. - JamiiForums

In 2015 Election, Tanzania had A Choice To Choose From. Jee Kwa 2020, Do We Still Have A Choice?. - JamiiForums

CHADEMA Chama cha Ajabu Sana!.Kwenda Mahakamani Kwa Non Issue, Serious Issue ya Katiba ni UKUTA!. - JamiiForums

Sheria ya Uchaguzi Ni Bad Law!, Kuendelea Kuitumia ni Ujinga?, Kuwabebesha Masikini Gharama za Uchaguzi ni Dhambi!. - JamiiForums

P.
 
Tunawatambua watu kwa matendo yao.kwahiyo huna haja ya kujieleza sana kwa sisi watu tuliosomea sayansi ya akili.Hayo maelezo yako yafaa uwaeleze watoto wa chekechea au vichaa.
 
U DC unanukia
 
Paschal sio hajui sababu ya cdm kugomea uchaguzi hila anachofanya ni dhihaka tu.Nashangaa hata kwanini tunacomment ujinga wake.alipaswa alete hoja ya sababu za cdm kugomea mfano Mawakala wa cdm kutolewa vituoni,kuna kituo kina voters 303 CCM wapepata 277etc but not that sarcasm.Heshima yake Paschal inashuka.
 
Kaka Pascal naelewa sana unachosema. Mbali na lugha ya udhalilishaji uliyotumia, nimeelewa hoja yako. Kinachoendelea kinaonesha wazi kuwa CDM wamekosa mbinu mbadala. Kususa au kugoma siyo suluhisho hasa kwa Viongozi wasioelewa hata maana ya demokrasia. Siasa za nchi zilizoendelea ni tofauti kabisa na za nchi zetu hizi zisizoendelea. Kuzira au kususa kisiasa havioneshi kuitishia serikali. Ni muda wa upinzani kutumia njia nyingine zinazoweza kuwapa haki zao za msingi. Hapa ndo tujadiliane njia mbadala tofauti na njia hizi zinazotumika sasa zisizo na matunda kwa wapinzani.
 
Hivi ukishaona askari ndo wanashangilia ushindi wa ccm badala ya wananchi wenyewe wapiga kura, kweli bado utaendelea kushiriki kwenye chaguzi hizo!!! Utakuwa mwehu kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…