Utaratibu wa sasa ni mzuri kuliko unavyotaka iwe.
Ni kweli kuna kupishana kwenye dini zetu, waislamu wataamini kile ambacho wakristo hawakiamini, hivyo pia wakristo watasema Yesu ni Mungu, ingawa waislam hawaamini hilo, lakini wanalazimika kuvumiliana.
Haya yasemwe kwenye vyombo kama hivi ili kuzidi kuimarisha tunu ya uvumilivu kwa kuwa hata mitaani tumechanganyika sana.
Kufanya ibada hizi kwenye vyombo kama TBC kunawalazimisha watu kama wewe kuzoea maisha ya kuvumilia, hasa pale unaposikia mafundisho yanayoenda kinyume na imani yako.
Kuhusu matumizi ya Lugha ya kiarabu kwenye kuendesha ibada za kiislam, hilo halikwepeki.
Moja wapo ya msingi muhimu wa ibada za waislam ni lugha.
Hakuna ibada kama haitumiki lugha ya kiarabu.
Madai ya kung'ang'ania Kiswahili pekee kwa sababu za kuimarisha umoja wetu hazina msingi.
Ndiyo maana kuna wakati hata viongozi wanatumia lugha nyingine za kigeni au za makabila yao ili kufikisha ujumbe fasaha kwa wasilkilizaji.
Vinginevyo TBC ni chombo cha walipa kodi wa Tanzania, ni haki yao kutumia chombo hicho bila kujali vyombo vingine ulivyotaja hata kama vitapewa masafa marefu zaidi.
Utaratibu huu umetumika miaka mingi, umekubalika na pande zote.
Ubaki kama ulivyo kwa afya ya umoja wetu.
Nakujibu kwa mtindo wa point counter point kama ifuatavyo:
Umesema: Utaratibu wa sasa ni mzuri kuliko unavyotaka iwe. Ni kweli kuna kupishana kwenye dini zetu, waislamu wataamini kile ambacho wakristo hawakiamini, hivyo pia wakristo watasema Yesu ni Mungu, ingawa waislam hawaamini hilo, lakini wanalazimika kuvumiliana. Haya yasemwe kwenye vyombo kama hivi ili kuzidi
kuimarisha tunu ya uvumilivu kwa kuwa hata mitaani tumechanganyika sana. Kufanya ibada hizi kwenye vyombo kama TBC kunawalazimisha watu kama wewe kuzoea
maisha ya kuvumilia, hasa pale unaposikia mafundisho yanayoenda kinyume na imani yako.
Jibu: Nimejieleza sana kwenye sehemu ya “mapingamizi tarajiwa" na majibu yake. Tunu ya uvumilivu haiwezi kutafsiriwa kuhalilisha kila kitu, kila mahali na kila wakati. Inayo mipaka. Mfano umesema, "wakristo watasema Yesu ni Mungu, ingawa waislam hawaamini hilo, lakini wanalazimika kuvumiliana." Sioni kama unaelewa vema dhana ya uvumilivu. Huwezi kuingia msikitini ukasema "Yesu ni Mungu" halafu ukavumiliwa na Waislamu. Vivyo hivyo, huwezi kuingia Kanisani ukasema "Mtume Mohammed Ndio Njia Pekee ya Kwenda Kwa Mungu" halafu ukavumiliwa na Wakristo. Lakini ukisimama gulioni ukayasema hayo, unaweza kuvumilika. Soma eneo hilo la “mapingamizi tarajiwa" na majibu yake, halafu uje na mawzo ya maboresho ambayo ni specific. Ni baada ya hapo maneno haya yanaweza kuwa na maana inayojadilika: “Utaratibu wa sasa ni mzuri kuliko unavyotaka iwe.”
Umesema: Kuhusu matumizi ya Lugha ya kiarabu kwenye kuendesha ibada za kiislam, hilo halikwepeki. Moja wapo ya msingi muhimu wa ibada za waislam ni lugha. Hakuna ibada kama haitumiki lugha ya kiarabu.
Jibu: Unachokisema hapa ndio sababu ya baadhi ya watu kuukataa Uislamu. Kwa hiyo, kuuleta Uislamu kwa njia ya TBC, chombo cha wote, ni ubabe wa kidini. Vivyo hivyo, kuna sababu zinazowafanya Wakatoliki wasiwe Walutheri, au Walutheri wasiwe Waanglikana. Kutumia TBC, chombo cha umma wote kumlazimisha mtu kusikiliza mafundisho ya dini aliyoikataa tayari ni kukiuka katiba ya nchi kifungu kile cha uhuru wa kuabudu, ibara ya 19(1).
Umesema: Madai ya kung'ang'ania Kiswahili pekee kwa sababu za kuimarisha umoja wetu hazina msingi. Ndiyo maana kuna wakati hata viongozi wanatumia lugha nyingine za kigeni au za makabila yao ili kufikisha ujumbe fasaha kwa wasilkilizaji.
Jibu: Kuhusu lugha nisema mawili. Mosi, ni suala la kitaaluma. Mwalimu yeyote anajua kuwa KUTAFSIRI ni mbinu mojawapo ya ualimu. Lakini kusoma kurani ya kiarabu kwa masaa sita mfululizo ni suala tofauti. Pili, sera ya Taifa ya lugha ya Kiswahili kama mbinu ya kujenga umoja wa kitaifa bado imesimama mpaka hapo itakapofutwa. Inapaswa kuheshimiwa na TBC. Na hilo ni jukumu la TBC kwa mujibu wa sheria ya Bunge iliyoianzisha.
Umesema: Vinginevyo
TBC ni chombo cha walipa kodi wa Tanzania, ni haki yao kutumia chombo hicho bila kujali vyombo vingine ulivyotaja hata kama vitapewa masafa marefu zaidi. Utaratibu huu umetumika miaka mingi, umekubalika na pande zote. Ubaki kama ulivyo kwa afya ya umoja wetu.
Jibu: Hoja kwamba, utaratibu huu ubaki kama ulivyo kwa kuwa umetumika kwa miaka mingi haina mashika. Historia inasema kwa makabila ya WASEGEJU na WAZIMBA kwa miaka mingi walikuwa na utamaduni wa kula watu. Hiyo pekee haiwezi kuwa sababu ya kukubali utamaduni huo uendelee. Lazima hoja nzuri ijengwe. Hujajenga hoja nzuri bado kuonyesha ni kwa nini utaratibu wa sasa “Ubaki kama ulivyo”. Usisahau kuwa kuna walipa kodi wasio na dini, na hivyo wenye haki ya kuona kodi yao haitumiki kuwahudumia wenye dini.