Dada mi ni mkristo lkn niseme ukweli kwamba kimtazamo wang naona kama hoja yako haijakaa kitaifa bali imekaa kidini. Na ndo maana hoja hii imekosa wachangiaji wengi, hii ni kwa sababu watu wengi humu wameshachoka na hoja zenye kuleta malumbano ya kidini baina yetu kama Taifa. Wengi humu tumeoleana na kuzaliana ktk imani tofauti. Unakuta baba muislam mama mkristo, au baba mkristo mama muisilam, watoto wanaozaliwa wanapokuwa wakubwa wanaamua wenyewe imani ya kufuata nk, hapo sijaongelea mtaani, mashuleni, maofisini na sehem mbali mbali za miji na nchi kwa ujumla. Umekiri mwenyewe kwamba unafahamu kitambo kuhusu vipindi vya dini vinavyorushwa kila siku asubuh na usiku wakati wa kulala, yan muda wa kufungua vipindi na muda wa kufunga vipindi, pia umekiri kuwa kuna vipindi vya kikristo huwa vinapitishwa kila jumapili kwa ajili yetu sisi wakristo lkn haukuwahi kuja kuhoji chochote kuhusu vipindi hivyo vya jumapili, lkn leo umeona na ndugu zetu na wao wameanza kupewa muda wa kuangalia au kufuatilia vipindi vyao TBC siku ya ijumaa umekuja haraka haraka kuzungumzia habari za kodi, ila wakati walipokuwa wanarusha vya kwetu kila ijumapili bila kupitisha hiki cha ijumaa swala la kodi haukulihoji. Tupendane jamani sisi wote ni taifa moja hao waliotuletea hizi imani kwa sasa wapo mbali baada ya kupuuza mawazo ya aina hii.
Hoja yako: Dada mi ni Mkristo lkn niseme ukweli kwamba kimtazamo wangu naona kama hoja yako haijakaa kitaifa bali imekaa kidini. Na ndo maana hoja hii imekosa wachangiaji wengi, hii ni kwa sababu watu wengi humu wameshachoka na hoja zenye kuleta malumbano ya kidini baina yetu kama Taifa.
Jibu: Haya sio malumbano ya kidini. Ni malumbano juu ya sera ya Taifa kuhusu namna bora ya kutenganisha dini na dola. Kuna sera za aina mbili duniani. Sera ya KImarekani na Sera ya KIjerumani. Wamarekani hawana hii habari ya kila dini kupewa airtime kwenye luninga ya Taifa. KIla dini ina luninga yake. Wajerumani wanweza kuruhusu baadhi ya dini kwenye luninga ya Taifa kama wanavyofanya wanapotumia TRA yao kukusanya sadaka kwa niaba ya makanisa. Lakini utitiri wa makanisa yaliyosajiliwa na serikali huwalazimisha kujikuta wanabagua baadhi ya madhehebu.
Hoja yako: Wengi humu tumeoleana na kuzaliana ktk imani tofauti. Unakuta baba muislam mama mkristo, au baba mkristo mama muisilam, watoto wanaozaliwa wanapokuwa wakubwa wanaamua wenyewe imani ya kufuata nk, hapo sijaongelea mtaani, mashuleni, maofisini na sehem mbali mbali za miji na nchi kwa ujumla.
JIbu: Kuoleana na mambo kama hayo sio hoja iliyo mezani. Mkristo akioana na Mwislamu wanaishi ktk nyumba yao wawili. Hilo sio suala la umma mpana wa kitaifa. Hoja yetu hapa ni jinsi gani bora ya kutofautisha maisha ya umma wa kitaifa na maisha binafsi. Maisha ya umma mpana wa kitaifa uko shuleni, ktk ofisi za serikali, ktk vyombo vya habari vya kitaifa, ktk vyombo vya usafiri wa umma, masoko, nk.
Hoja yako: Umekiri mwenyewe kwamba unafahamu kitambo kuhusu vipindi vya dini vinavyorushwa kila siku asubuh na usiku wakati wa kulala, yaani muda wa kufungua siku na muda wa kufunga siku, pia umekiri kuwa kuna vipindi vya kikristo huwa vinapitishwa kila jumapili kwa ajili yetu sisi wakristo lkn haukuwahi kuja kuhoji chochote kuhusu vipindi hivyo vya jumapili, lkn leo umeona na ndugu zetu na wao wameanza kupewa muda wa kuangalia au kufuatilia vipindi vyao TBC siku ya Ijumaa umekuja haraka haraka kuzungumzia habari za kodi, ila wakati walipokuwa wanarusha vya kwetu kila ijumapili bila kupitisha hiki cha ijumaa swala la kodi haukulihoji.
Jibu: Kila jambo lina sababu za karibu na sababu za mbali. Kabla ya leo Rioba alikuwa anaongoza kongamano Morogoro wakiwepo viongozi wa TEF. Pale alieleza vema dhima ya vyombo vya habari na nafasi ya lugha ya Taifa katika kujenga umoja wa kitaifa. Siku moja baadaye nikaona chombo anachokiongoza kinapingana na kauli zake za siku moja kabla. Nikafanya udadavuzi na kuibuka na hoja hii. Ni hoja ambayo haiwalengi Waislamu pekee wala Wakristo pekee. Ni hoja pana zaidi. Inawahusu Wakristo, Waislamu, Wabuda, Wahindu, Wabahai, na Wa-ATR. Pia KIlatini ni lugha ya Taifa ya Italia wakati Kiarabu ni lugha ya Taifa ya Saudia. Lugha ya Taifa ya Tanzania ni Kiswahili. TBC wanawajibika kukuza lugha ya Taifa la Tanzania na sio vinginevyo. Tujadili hoja niliyoweka mezani.
Hoja yako: Tupendane jamani sisi wote ni taifa moja hao waliotuletea hizi imani kwa sasa wapo mbali baada ya kupuuza mawazo ya aina hii.
Jibu: Njia bora zaidi ya kupendana ni kukubaliana kuhusu njia bora ya kisera katika kutekeleza matakwa ya kikatiba yanayosaema kuwa serikali ya Tanzania haina dini hata kama watu wake wana dini. TBC ni chombo cha umma kinachosimamiwa na serikali hiyo. Mjadala uendelee.