Swali kwa Jaji Mkuu: Je, ni haki kwa kina Rostam Aziz kutozwa faini badala ya kifungo lakini kina Mbarikiwa kupewa kifungo badala ya faini?

View attachment 2766809
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma

Mheshimiwa Jaji Mkuu,

Tarehe 29 Septemba 2023, Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya ilimhukumu kifungo cha miaka mitatu na siku 14 jela, Mchungaji anayeitwa Mbarikiwa Mwakipesile (39), baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kuendesha huduma ya kikosi kazi cha Injili kabla ya kupata usajili kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kama sheria ya vyama vya kijamii inavyotaka.

Hukumu hiyo ilitolewa chini ya kifungu cha 25(1) cha sheria ya vyama vya kijamii. Kifungu kinatoa fursa ya kulipa faini u kifungu, au vyote kwa pamoja. Mahakama imeamua kutoa adhabu ya kifungo.

Mchungaji Mwakipesile amekuwa anaituhumu serikali kwamba inawaona wanachi kama nyani au kenge. Yeye ni baba mzazi wa Sifa Bujune, Muimbaji wa Injili anayetuhumiwa kusambaza uongo kutokana na Wimbo wake wa “Mnatuona Nyani tu”,

View attachment 2766819

Lakini, kumbukumbu zinaonyesha kwamba, Akram Aziz, mdogo wake Ristam Aziz, alikabiliwa na kesi ya mashtaka 75 ya uhujumu uchumi kwa kukutwa na nyara za Serikali, silaha za aina mbali mbali na risasi zake (tazama Kkiambatanisho hapa chini). Kesi yake iliendeshwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Mwishowe alitozwa faini, badala ya kifungo.

View attachment 2766818
Undumilakuwili huu unazitia doa mahakama za Tanzania, ambazo utendaji kazi wake unasimamiwa na Jaji Mkuu.

Mahakama inayomheshimu jangili na kumtweza mchungaji ni mahakama yanhovyo sana. Mahakama inayomheshimu mwarabu mwenye asili ya Iran na kumtweza Mbantu wa Mbeya haina haki ya kuitwa mahakama. Mahakama inayowatukuza wenye mali na kuwakandamiza kabwela sio mahakama kamwe. Mahakama inayokumbatia kanuni ya umachiveli, isemavyo kwamba "good ends may justify any means, including evil means," haitakiwi nchini Tanzania.

Hivyo, tunatoa wito kwako Mheshimwa Jaji Mkuu: tunaomba ulinde heshima ya Mhimili muhimu unaoitwa Mahakama kwa kuchukua hatua stahiki za kufuta undumilakuwili huu.

============KIAMBATANSHO KUHUSU KESI YA MDOGO WAKE ROSTAM AZIZI==================

MUHTASARI WA KESI YA MDOGO WAKE BILIONEA ROSTAM AZIZ​

Mnamo 30 Oktoba 30 2018, saa 7 mchana maeneo ya Msasani, Jijini Dar, Akram Aziz, mdogo wake Rostam Aziz, alikamatwa na vyombo vya dola akiwa na nyara mbalimbali za serikali zikiwemo Pembe za ndovu.

Ilithibika kuwa Akram (Iqram) ni jangili wa muda mrefu na upekuzi uliofanyika nyumbani kwake ulibaini kuwa Akram anamiliki silaha nyingi kinyume cha sheria, pamoja na mihuri mingi bandia ya taasisi za serikali ambapo alikutwa na “vibali feki” vya uwindaji vingi sana.

Ilifahamika kuwa amekuwa ni “Mastermind” wa ujangili nchini kwa muda mrefu sana na ndiye kinara wa mauaji ya tembo na wanyama wengine kwenye mbuga zetu.

Taarifa za uhakika zilisema kuwa mtandao huo wa ujangili ulikuwa unasimamiwa na Kaka yake Rostam Aziz pamoja na baadhi ya viongozi wengine wa vyama vya siasa na serikali katika awamu zilizopita. Hatimye Akram alitiwa hatiani na kupewa adhabu ya kulipa faili badala ya kifungo. Picha zifuatazo ni baadhi ya silaha alizokamatwa nazo:

View attachment 2766815

View attachment 2766816

View attachment 2766817

Mama Amon
Mkurugenzi Mtendaji
Dawati la Utafiti la Mama Amon (DUMA)
"Sumbawanga Town"
S.L.P. P/Bag
Sumbawanga
30 Sep 2023
Undumilakuwili huu unazitia doa mahakama za Tanzania, ambazo utendaji kazi wake unasimamiwa na Jaji Mkuu. Hivyo, tunatoa wito kwako Mheshimwa Jaji Mkuu: tunaomba ulinde heshima ya Mhimili muhimu unaoitwa Mahakama kwa kufuta undumilakuwili huu.[emoji419][emoji375]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo wewe sasa unampangia hakimu namna ya kuhukumu?
Sio kupangiwa haki ipo kwenye mizani! Lipi kosa kubwa hapa:-
Kupatikana na hatia ya ujangili adhabu= Faini.

Kupatikana na hatia ya kuanzisha kanisa kabla hujapata kibari adhabu = kifungo miaka 3 bila kufikiria kumpa adhabu ya faini
Kwa heshima na taadhima niseme tu kuwa yatupasa kuliombea Taifa.
 
View attachment 2766809
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma

Mheshimiwa Jaji Mkuu,

Tarehe 29 Septemba 2023, Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya ilimhukumu kifungo cha miaka mitatu na siku 14 jela, Mchungaji anayeitwa Mbarikiwa Mwakipesile (39), baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kuendesha huduma ya kikosi kazi cha Injili kabla ya kupata usajili kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kama sheria ya vyama vya kijamii inavyotaka.

Hukumu hiyo ilitolewa chini ya kifungu cha 25(1) cha sheria ya vyama vya kijamii. Kifungu kinatoa fursa ya kulipa faini u kifungu, au vyote kwa pamoja. Mahakama imeamua kutoa adhabu ya kifungo.

Mchungaji Mwakipesile amekuwa anaituhumu serikali kwamba inawaona wanachi kama nyani au kenge. Yeye ni baba mzazi wa Sifa Bujune, Muimbaji wa Injili anayetuhumiwa kusambaza uongo kutokana na Wimbo wake wa “Mnatuona Nyani tu”,

View attachment 2766819

Lakini, kumbukumbu zinaonyesha kwamba, Akram Aziz, mdogo wake Ristam Aziz, alikabiliwa na kesi ya mashtaka 75 ya uhujumu uchumi kwa kukutwa na nyara za Serikali, silaha za aina mbali mbali na risasi zake (tazama Kkiambatanisho hapa chini). Kesi yake iliendeshwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Mwishowe alitozwa faini, badala ya kifungo.

View attachment 2766818
Undumilakuwili huu unazitia doa mahakama za Tanzania, ambazo utendaji kazi wake unasimamiwa na Jaji Mkuu.

Mahakama inayomheshimu jangili na kumtweza mchungaji ni mahakama yanhovyo sana. Mahakama inayomheshimu mwarabu mwenye asili ya Iran na kumtweza Mbantu wa Mbeya haina haki ya kuitwa mahakama. Mahakama inayowatukuza wenye mali na kuwakandamiza kabwela sio mahakama kamwe. Mahakama inayokumbatia kanuni ya umachiveli, isemavyo kwamba "good ends may justify any means, including evil means," haitakiwi nchini Tanzania.

Hivyo, tunatoa wito kwako Mheshimwa Jaji Mkuu: tunaomba ulinde heshima ya Mhimili muhimu unaoitwa Mahakama kwa kuchukua hatua stahiki za kufuta undumilakuwili huu.

============KIAMBATANSHO KUHUSU KESI YA MDOGO WAKE ROSTAM AZIZI==================

MUHTASARI WA KESI YA MDOGO WAKE BILIONEA ROSTAM AZIZ​

Mnamo 30 Oktoba 30 2018, saa 7 mchana maeneo ya Msasani, Jijini Dar, Akram Aziz, mdogo wake Rostam Aziz, alikamatwa na vyombo vya dola akiwa na nyara mbalimbali za serikali zikiwemo Pembe za ndovu.

Ilithibika kuwa Akram (Iqram) ni jangili wa muda mrefu na upekuzi uliofanyika nyumbani kwake ulibaini kuwa Akram anamiliki silaha nyingi kinyume cha sheria, pamoja na mihuri mingi bandia ya taasisi za serikali ambapo alikutwa na “vibali feki” vya uwindaji vingi sana.

Ilifahamika kuwa amekuwa ni “Mastermind” wa ujangili nchini kwa muda mrefu sana na ndiye kinara wa mauaji ya tembo na wanyama wengine kwenye mbuga zetu.

Taarifa za uhakika zilisema kuwa mtandao huo wa ujangili ulikuwa unasimamiwa na Kaka yake Rostam Aziz pamoja na baadhi ya viongozi wengine wa vyama vya siasa na serikali katika awamu zilizopita. Hatimye Akram alitiwa hatiani na kupewa adhabu ya kulipa faili badala ya kifungo. Picha zifuatazo ni baadhi ya silaha alizokamatwa nazo:

View attachment 2766815

View attachment 2766816

View attachment 2766817

Mama Amon
Mkurugenzi Mtendaji
Dawati la Utafiti la Mama Amon (DUMA)
"Sumbawanga Town"
S.L.P. P/Bag
Sumbawanga
30 Sep 2023
Hizo picha ulizoweka ni uongo mtupu, defamation.

Nenda kaisome sheria ya "plea bargain", kama wewe a mchungaji wako mmeshindwa na hamkujuwa kuitumia, wenzenu walijuwa kuitumia.

Ndugu yako wewe akifanya kosa uhukumiwe wewe au sivyo?
 
He! Ongeza nyama kidogo
Mwishoni mwa miaka ya 80 padri Mzungu wa Mtwara alihukumiwa kwenda jela kifungo cha siku 1 baada ya kupatikana na hatia.

Siku chache zilizofata mbunge wa Songea mjini nae akala miaka 8 kwa kosa hilohilo ka kukutwa na meno ya tembo.

Kwa hiyo usishangae binadamu wote hatuko sawa na hivyo hakuna usawa
 
AWAMU ya Tano watu walisema Kuwa Magufuri alikua dictator ambaye alikua hataki akosolewe, akapita imekuja hii AWAMU hii Sasa ndo tumeshuhudia mambo mengi ya ajabu mno kama Taifa tunaenda Wrong direction, huwez funga uhuru wa watu wakati huo katiba inawaruhusu, Je! Hiyo katiba ipo kwa ajili ya masikini tu syo wanasiasa!! Na matajiri. Hivyo kwa sheria zipo kwa ajili ya masikini.

Zumaridi amepatikana na makosa ya Biashara za Binadamu Huku akichukua watoto wadogo akiwafanya mazombie!! Lakin mtu huyo baada ya mda mfupi kachiwa, Na wakina Mwamposa wanaendesha makongomano yanayo ua watu mbona hakuna sheria Inayo chukuliwa. Je! Huyo Mbarikiwa kosa lake ni lipi kudai haki yake.

Mh Sa100 haya ni ya mda kumbuka ww upo kwa ajili ya kulinda katiba pamoja na kuliongoza Taifa katka njia sahihi na siyo kuwafunika makombe wasiongee huyo siyo Uongozi Bora na siyo Democracy hiyo tunayo sema tunayo, ni Bora isiwepo tu tujue Kuwa no udikiteta hamna uchaguzi huru tunasema tuna demoracy gani hiyo??🚮🚮
 
Hizo picha ulizoweka ni uongo mtupu, defamation.

Nenda kaisome sheria ya "olea bargain", kama wewe a mchungaji wako mmeshindwa na hamkujuwa kuitumia, wenzenu walijuwa kuitumia.

Ndugu yako wewe akifanya kosa uhukumiwe wewe au sivyo?
Ndio picha zilizorushwa wakati Polisi wakitangaza kukamatwa kwake......nenda kwenye sources zote video siku ya kukamatwa.
Au polisi walituuza?
 
Kesi yeyeto ni interest na biashara pia inategemea umeingia kwa mguu gani, ukiingia 18 zao hata kama una pesa lazima wakushikishe ukuta kwanza uwe na adabu
 
Zumarid ni Pro ccm.

You are safe when you are pro ccm. Do whatever no one touch you.
Hii nchi Bora lijulikane Moja tu hatuna katiba, hatuna Democracy n Bora lijulikane Moja tu, nchi imekua ya kifalme aisee... Ujinga mtupu 🚮🚮 Yani katiba na sheria ipo kwa wale ambao siyo CCM na ambao ni masikini? Anyway ngoja tuendelee kuishi tu no way out
 
Sio kupangiwa haki ipo kwenye mizani! Lipi kosa kubwa hapa:-
Kupatikana na hatia ya ujangili adhabu= Faini.

Kupatikana na hatia ya kuanzisha kanisa kabla hujapata kibari adhabu = kifungo miaka 3 bila kufikiria kumpa adhabu ya faini
Kwa heshima na taadhima niseme tu kuwa yatupasa kuliombea Taifa.
Wewe umesomea sheria?
 
Back
Top Bottom